Itaje hapa shule ya Msingi ya Serikali inayotoa elimu kwa lugha ya kiingereza (English medium) iliyopo mkoani kwako

Itaje hapa shule ya Msingi ya Serikali inayotoa elimu kwa lugha ya kiingereza (English medium) iliyopo mkoani kwako

Manzile

JF-Expert Member
Joined
Apr 23, 2020
Posts
701
Reaction score
1,900
Habari zenu wanabodi,

Kuna watu wengi hawafahamu kama serikali inazo shule zake za msingi za mitaala ya kiingereza (English medium) kwa gharama nafuu, Tusaidiane kufahamu majina na zilipo kwa kila eneo/mkoa hizi shule. Naanza

1. Olympio - Dar Es Salaam
2. Diamond - Dar Es Salaam
3. Magufuli - Mbeya
4. Mapinduzi - Gangilonga Iringa
5. Mkapa - Mbeya
6. Oysterbay primary school - Dar
7. Nyasa primary school - Kyela, Mbeya
8. Arusha primary school - Arusha
9. Angaza - Mbeya
10. Nuru - Mbeya
11. Iringa primary school - Iringa
12. Lupilisi - Ruvuma
13. Tanga Primary school - Tanga
14. Kisimani - Arusha
15. Azimio - Mbeya
16. Chato primary school - Geita
17. mkoani primary school-kibaha pwani
1. Duce primary School - Dar
19..........................

20.....................................


Karibuni wakuuu
 
Arusha hapa karibu na tanesco... Nyuma ya arusha hotel...
 
1594899931955.png
1594899988294.png
1594900032434.png
 
WIZARA ya Elimu, Sayansi na Ufundi imetoa waraka wa elimu kuhusu elimumsingi bila malipo na kutoa orodha ya shule za msingi 11 za Serikali ambazo hazihusiki na utoaji wa elimu bure uliotangazwa na Rais John Magufuli.

Elimumsingi inajumuisha elimu ya awali, ya msingi na sekondari ambayo itaanza Januari mwakani.

Katika Waraka Elimu Namba 6 wa Mwaka 2015 kuhusu utekelezaji wa elimu bure kwa shule za msingi na sekondari, wizara hiyo imetaja shule hizo kuwa ni Shule ya Msingi Olympio (Dar es Salaam); Shule ya Msingi Diamond (Dar es Salaam); Shule ya Msingi Oysterbay (Dar es Salaam); Shule ya Msingi Iringa (Iringa) na Shule ya Msingi Mkapa (Mbeya).

Nyingine ni Shule ya Msingi Angaza (Mbeya); Shule ya Msingi Nuru (Mbeya); Shule ya Msingi Lupilisi (Ruvuma); Shule ya Msingi Tanga (Tanga); Shule ya Msingi Arusha (Arusha) na Shule ya Msingi Kisimani iliyoko mkoani Arusha.

Wizara hiyo pia imesema waraka huo hauzihusu shule zinazomilikiwa na mashirika ya umma ama taasisi za umma ambazo zinaendeshwa kwa taratibu sawa na shule za binafsi.

Katika waraka huo, wizara hiyo imetoa majukumu yanayotakiwa kufanywa na Wizara hiyo, Tamisemi, wakurugenzi wa manispaa na halmashauri ya wilaya, wakuu wa shule, bodi za shule, wazazi na wananchi.
 
Back
Top Bottom