Itakavyokuwa Simba SC 1 - 1 Jwaneng galaxy

Itakavyokuwa Simba SC 1 - 1 Jwaneng galaxy

mwehu ndama

JF-Expert Member
Joined
Nov 12, 2019
Posts
630
Reaction score
2,151
Katika uzi huu maridhawa najaribu ku prognosticate / bashiri kile kitakachotokea katika pambano la Jumamosi baina ya Kolozidad na Galaxy ya Botswana.

Mbumbumbu fc wataingia katika mchezo huu wakiwa na kibri na majivuno makuu, huku wakichagizwa na wingi wa madunduka yatakayokuwa yameupamba uwanja wa mkapa kwa rangi nyekundu na nyeupe. Nyuma ya pazia ujasiri wa kolozidad utakuwa unapewa nguvu kubwa na kikosi chao cha walozi kutoka ujiji kigoma na bariadi simiyu ambao wao watakuwa Vip B wakichochea kuni nakurusha maruani hovyo uwanjani.

Kwa upande wao jwaneng galaxy watakuwa na utulivu mkubwa na umakini wa juu kabisa kwa lengo la kutetea ahadi ya dola laki 2.5 waliyopokea toka kwa wydad AC ikiwa watafanikiwa kupata walau sare na kuleta taharuki miongoni mwa madunduka katika katika dimba la mkapa. Lakini tayari walozi wa kujitolea toka viunga vya twiga na jangwani nao wamepewa taarifa juu ya hili na katika kulitazama kwa mapana tayari mashabiki wa matawi ya wananchi wameshatuma nauli katika kambi kuu za ulozi za wanayanga kule ubena zomozi na safu za milima ya uluguru ili kuwasafirisha walozi hao mpaka Lupaso kuwazima vigagula wa kolozidadi. "kwa kifupi hii mechi imeshaisha nje ya uwanja". Matokeo tunayo na hapa ipo!!

Mechi itaanza kwa kasi, na mbumbumbu watafanya mashambulizi yao mengi kupitia katikati lakini katika mshangao wa wengi, Jwaneng galax watafanya pressing kidogo nakuupata mpira kisha watapigiana pasi fupi fupi za haraka na kwenda kulitoboa tundu la wanasimba. Baada ya hapo watakaa nyuma na kufanya low block mpaka dakika ya 88, ndipo kolozidad watakapo chomoa na mechi kumalizika kwa, matokeo ya sare ya moja moja.

Baada ya hapo jiji la daslam litajaa simanzi na taharuki, huku nderemo na vifijo zikitawala mitaa ya twiga na jangwani pekee, Vilio vya madunduka vitasikika kuanzia Lupaso hadi mkulanga, watu wa kibaha watalia pamoja nao. mbumbumbu watamkataa Mangungu hadharani, na wao kwa wao watachapana Makonde. Chama ataambiwa awaachie timu yao, Saidoo ataitwa mzee na mwisho wa siku wale mashabiki wao mazuzu kama mzaramo wa simba, pasi million, kisugu na wengine wapenda camera watapotea kunako yuotube na kurudi katika kichaka cha historia.

Niko nimekaa paleeeeeee[emoji117]
 
Mtawaua Hawa Mbumbumbu/Wamatopeni/Kolouzidad Maana Hadi Sasa Wamechanganyikiwa
 
Back
Top Bottom