Itakua sharti kwa 'international schools' kufunza Kiswahili na historia ya Kenya

MK254

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2013
Posts
32,408
Reaction score
50,809
Historia ya Kenya na lugha ya Kiswahili zitafunzwa kwenye shule za kimataifa Kenya na itakua sharti.
Hivyo hata watoto wa mabalozi itabidi wafunzwe tamaduni zetu.
---------------------------------------------------

International schools in Kenya are set to start teaching Kiswahili and Kenyan history effective September, 2017. The introduction of the two subjects follows a government directive stipulating that international schools should incorporate 8-4-4 basic education in their curriculum.

Speaking during the 20th Annual Presentation at Braeside High School, Education Cabinet Secretary, Dr. Fred Matiang’i, said students will be taught the two subjects up to Grade 9, which is the equivalent of form two.
Dr. Matiang’i added that International Schools admit many children of Kenyan descent, and it is essential for them to be acquainted with their history and also Kiswahili being an official language of communication.

Further, Dr. Matiang’i said that international schools must ensure that their teachers are duly registered and accredited by the Teachers Service Commission (TSC).

“We want to ensure that all schools have teachers who have been well trained to handle children,” Dr. Matiang’i.

He promised that government will simplify the process of approving expatriate teachers once applications are made.
https://citizentv.co.ke/news/intern...ications&utm_campaign=onesignal_notifications
 
Kwani Waafrika wana tamaduni? Majina yenu yenyewe Lawrence, Abdallah, Hassan, Wycliff n.k yanaonesha watu weusi ni watu waliochanganyikiwa bila utamaduni wowote.
 
La majina mbona unatuonea Waafrika maana hata Wachina wenye tamaduni zenye umri zaidi ya miaka 500 wapo wanaotumia majina hayo ya wenzetu kutoka Ulaya. Kwa mfano Jackie Chan, David Wang, Jessica Long n.k.
 
Hasa Tz tamaduni zetu ziko Mob hivo kitambo zilitutupa mkono sana..
 
La majina mbona unatuonea Waafrika maana hata Wachina wenye tamaduni zenye umri zaidi ya miaka 500 wapo wanaotumia majina hayo ya wenzetu kutoka Ulaya. Kwa mfano Jackie Chan, David Wang, Jessica Long n.k.
wanahesabika sana tofauti na sisi ambapo majina ya kiarabu na kimagharib yameshakuwa kwenye tamaduni mpya za kiafrika
huku bongo sijajua kwa kenya, ukimwita mwanao hata jina la kawaida kama Ngekewa ambayo humaanisha bahati, atachekwa hadi kuchukia jina lake tofauti na wenzetu wa asia au wazulu mbali na kuishi na makaburu
 
ila niwape pongezi wakenya kwa hatua mliyofikia angalau mmethubutu kuonyesha thamani ya uenyeji
kuna siku nilikuwa nimepita karibu na shule aga khan kule upanga dar si salama nikawakuta watoto wa kihindi wanaongea kiingereza tu na kihindi, nikajiuliza hivi kweli hawa hata wimbo wa taifa wanaujua kweli?
halafu kesho tunaambiwa hawa ni watanzania wenye asili ya asia, upuuzi
 
Hehehe!! Nakiri kwa kweli hilo la majina ni tatizo Afrika, tangu tukiwa wadogo tulikua tunawacheka watu wenye majina fulani fulani ya Kiafrika kama vile Wepukhulu, Wagatonye, Muringiti, Kibiingoti, Shirandula n.k.
 
La majina mbona unatuonea Waafrika maana hata Wachina wenye tamaduni zenye umri zaidi ya miaka 500 wapo wanaotumia majina hayo ya wenzetu kutoka Ulaya. Kwa mfano Jackie Chan, David Wang, Jessica Long n.k.

Hao wengi ni Wachina waliokuwa brainwashed kwa kuishi uzunguni, ama wengine ni wa kutoka nje ya China mainland kama Hong Kong na Taiwan.

Waafrika ndio jamii pekee duniani inayochukia dini zake, tiba zake, majina yake na kila kitu cha Kiafrika. Huwa saa nyingine tunakuwa wanafiki kwa kujifanya tunajali kuhusu Uafrika lakini sio kweli.

Waafrika wanatakiwa kuitwa majina kama Maina Njenga, Jakaya Kikwete, Raila Odinga, Thabo Mbeki n.k. Huu ulevi uliotamalaki wa John Pombe, Michael Kalonzo, Hassan Joho ni kielelezo cha uzwazwa wetu.
 
ila niwape pongezi wakenya kwa hatua mliyofikia angalau mmethubutu kuonyesha thamani ya uenyeji
kuna siku nilikuwa nimepita karibu na shule aga khan kule upanga dar si salama nikawakuta watoto wa kihindi wanaongea kiingereza tu na kihindi, nikajiuliza hivi kweli hawa hata wimbo wa taifa wanaujua kweli?
halafu kesho tunaambiwa hawa ni watanzania wenye asili ya asia, upuuzi
Hahaha ndio mana manji hajui kuongea kiswahili hata cha dakika tatu
 
Uzungu na Uarabu nao ni janga waafrika tunakumbatia style za hawa watu utazani wao wana time na zetu.

Though we are all humans lakini tunatakiwa tulinde uafrika wetu.
 
Historia ya Kenya na lugha ya Kiswahili zitafunzwa kwenye shule za kimataifa Kenya na itakua sharti.
Hivyo hata watoto wa mabalozi itabidi wafunzwe tamaduni zetu.
Hatua nzuri ya kuelekea kwenye kuutambua utu wa Mkenya, Mwafrika Mashariki na Uafrika kwa ujumla...
 
Ukenya huwa tumeutambua na huwa tupo makini sana kwenye kudumisha tamaduni zetu ikiwemo lugha zetu za asili, ila hapa tunawalazimisha hawa wanaokwenda kwenye shule za kimataifa lazima na wao waongee na kusoma Kiswahili.
 
Vizuri sana! Natamani siku moja wa Africa tuongee lugha moja "KISWAHILI"
 
Hahaha ndio mana manji hajui kuongea kiswahili hata cha dakika tatu
Duuh kumbe manji hajui kuongea kiswahili? kweli hili ni janga nilikuwa sijui
ila nimewahi kumsikia Mo Dewji mara kadhaa anaongea vizuri na bado sijajua kwa huyu nyangumi wa IPTL, Harbinder Singh Seth, hawanaga uzalendo kabisa na nchi mana hata mali zao wanachuma bongo ila hazina wanapeleka uingereza, india na canada
 
Nadhani sio Mtanzania
 
Singa singa si ni mkenya ama?[emoji13] [emoji13] [emoji13]
 
Yes i like this Visited some people of mine in Nairobi and i was suprised hawajui kuongea kiswahiki hata kidogo and they were born in Nairobi
 
Hao wengi ni Wachina waliokuwa brainwashed kwa kuishi uzunguni, ama wengine ni wa kutoka nje ya China mainland kama Hong Kong na Taiwan.

Waafrika ndio jamii pekee duniani inayochukia dini zake, tiba zake, majina yake na kila kitu cha Kiafrika. Huwa saa nyingine tunakuwa wanafiki kwa kujifanya tunajali kuhusu Uafrika lakini sio kweli.

Waafrika wanatakiwa kuitwa majina kama Maina Njenga, Jakaya Kikwete, Raila Odinga, Thabo Mbeki n.k. Huu ulevi uliotamalaki wa John Pombe, Michael Kalonzo, Hassan Joho ni kielelezo cha uzwazwa wetu.

Mkuu Uhuru Kenyatta muweke hapo kwenye orodha![emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom