Itakuaje siku Diamond akiwaomba radhi clouds TV?

Nitajia media nyingine iliyotengeneza msanii mwenye ela au msanii tajiri?
Mziki wa Tanzania now walau kidogo ndo umeanza kullpa awali ulikuwa hauna ela ya maaana mtu show anapiga kwa laki tatu ela itoke wapi?
Halafu media nyingine zinafail wapi katika kutengeneza wasanii wapya hapo ndipo uwa nashangaa maana ukisikiliza hata hizo media nyingine ngoma zinazo trend huko ni wale wale wasanii wa clouds.
 
Naona na ww utakua shabik wa Ally kiba
 
Humu Kuna wadau wanadai Diamond platnumz mafanikio yake yametokana na wao sasa nikawauliza mbona wanashindwa kwa barnaba ambaye ni multi talented, mbona wameshindwa kwa THT na kuhusu media CMG wapo karibu na wasanii kuliko media yoyote, ili kipindi cha Fiesta wa wanyonye kwa kigezo cha kuwapa promo. Kuhusu mziki zamani haukuwa na hela na mimi na kupinga (washika dau waliamua kutuaminisha hivyo na wasanii walikuwa hawajitambui wao walikuwa wanataka nyimbo zao zipigwe tu) , kipindi cha nyuma Kilimanjaro baada tu ya tuzo zao kuisha, wanakuwa na tour karibia mikoa yote na list ndefu na kama hujui Kilimanjaro walikuwa wanalipa hela ndefu kuliko Serengeti FIESTA, Sasa jiulize kwa nini Kilimanjaro waweze, Serengeti ndio washindwe. Fiesta pamoja na kuwa na msululu wa wadhamini lkn wanashindwa kuwalipa wasanii vizuri na kama hujui Dully aliwahi kuwachomolea Clouds sababu ya show za kilimanjaro (Ushawahi kuwasikia wasanii wakiwalalamikia Kilimanjaro kuwabana) . Ila sasa hivi kitu kinachowapa hela wasanii ni Social networking na digital platform na si hela kutokana na show kama za FIESTA (show nyingi tokea zamani zinaendeshwa kishikaji mpaka sasa hivi ) na Mondi ni mkazaji anakuambia bila milioni 10 basi sawa Harmonize na Rayvany kuja kwenye show yako. Alafu sikiliza ndugu mimi nipo katika field hii ya telecom na hata kazi yangu ya kwanza ilikuwa ktk power, kampuni za telecom zinatumia hela nyingi sana ktk marketing na power, nina uhakika Tigo wakatoa hela ndefu sana, ila CMG wanabana hapo bado Kuna msululu wa wadhamini wadogo. Alafu Fiesta walitumia hela mwanzoni ilipoanza na ilipokuwa kubwa,ila badaye kampuni zikawa zinadhamini kila kitu ili kutangaza bidhaa zao. Ushawahi msikia madam Rita anakuambia alitumia hela nyingi BSS mwanzoni, ila sasa hivi brand imekuwa kwa yy hatumii hata shillingi, sababu wadhamini wanaona kupitia brand ya BSS wanaweza tangaza brand yao. Mwisho clouds wanatengeza hela ndefu sana, ila wanaamua kuwa bana wasanii, kwa kutumia kigezo cha promo ktk media zao, alafu usitumie kigezo cha kutengeneza msanii alafu baadaye unamnyonya, baadaye anakuwa apeche alolo, bora ungemwacha tu.
 
Kupiga tour mikoa yote haimaanishi kuna ela ushajiuliza walikuwa wanalipwa kiasi gani.
Ok tuseme CMG wanawanyonya wasanii ni kwanini media nyingine hazianzishi event kubwa kuliko Fiesta?
Mavoko kaondoka WCB kwa kigezo kile kile cha kunyonywa hapo unasemaje?
Hulipwi ullicho fania kazi unalipwa ulichopatana hiyo ndiyo formula katika dunia ya kibepari, mtu akiwaga wino halafu baadae aanze kulalama mimi uwa simwelewi.
Kuhusu Barnaba kwanini hawajaweza kumtengeneza kama Diamond, ni sawa na team ya mpira hata kocha we mtaalamu vipi hawezi watengeneza wachezaji wote wawe na kiwango kama cha Christian Ronaldo hata aapply njia zile zile za ufundishaji, maana achilia mbali kuimba, pia vision na kujituma na baraka za Mja zina changia.
Haitotokea wasanii waache kulalamika kuibiwa, hata hao wasafi wakianzisha wasafi festival waka include wasanii wengi kama fiesta, utaanza sikia wanalalamika kuwa wanawanyonya.
Hiyo promo EFM na TV wanashindwa wapi, East Africa, Magic, Radio One, na mitandano yote hii. Maana utaskia kila mtu anaiponda clouds na kudai haisikilizi lakini bado mnadai promo promo promo, sa kitu kisicho sikilizwa kitakukoseshaje promo?
 
Kumtengeneza msanii alafu ukashindwa kumlipa, utakuwa una mdhalilisha. Hivi ushawahi kuwaona hawa wasanii wa zamani walivyo na hali ngumu mf PNC, 2015 kafukuzwa na mwanamke aliyekuwa anakaa nae ktk gheto lake akawa anamtegemea jamaa yangu fundi gereji, anaogopa kupanda daladala kutwa yupo ndani ni si hao wapo wengi,mtengeneze mtu ili baadaye wote mfaidike. Hivi mpaka sasa ushasikia wasanii wangapi wanawalamikia FIESTA. Kuhusu mavoko, kama umemfuatilia hii lebo ya tatu anazinguana nayo (Papa misifa, Kings record, WCB ), hata alivyotoka hii mimi siku shangaa, mpaka sasa huwezi ukaconclude kwamba mavoko wanamnyonya kwani hata BASATA, wamepeleka mikataba yao kwa waziri mwakyembe itazamwe. Narudia tena redio hizo hawana program ya kutengeneza wasanii sababu ya kwanza hawana matamasha ya mara kwa mara lkn ukiachia mbali na hapo hawabagui kwamba huyu msanii tuna mtumia au hatumii wote wanapewa promo sawa. CMG lazima watengeneze wasanii sababu wana FIESTA, after skull bash na hiyo haitoshi pale kwa mwaka kila mtangazaji ana event yake so wanatumia kigezo cha promo ili kuwabana wasanii (kwa mwaka msanii anaweza akapiga show zaidi ya 30 sasa za CMG) , hizi redio nyingine kazi yao kupokea nyimbo za msanii yoyote na kuzipiga basi.Jiulize kwa nn wasanii wa walalamikie FIESTA na si KTM au kwanini wasanii walikuwa hawalamiki show zilizokuwa zikiandaliwa na Kwa fujo dj, jiulize wasanii tofauti wote wanalalamika kitu kile kile huoni kuwa Kuna wa lakini au labda nawe mfaidika.
 
Tatizo la usanii ni kuishi maisha ambayo hayana uhalisia.
Kuna watu kupitia hiyo hiyo sanaa na hicho hicho kidogo waliwekeza na sasa hivi bado wanaendelea na maisha mengine.
Wasanii wengi walikuwa wanataka kuishi maisha walliyokuwa wanayaona kwenye TV ya akina Lil Wayne, hata huko mbele wasanii kama akina Jay Z wamewekeza mbali na mziki ni wajasiriamali, Sean Coms ni mjasiriamali.
Narudia tena nipe jibu linalo jitosheleza media nyingine zimeshindwa nini kutengeneza events zinazoeleweka zikawalipa hao wasanii ela nzuri? Maana wasanii wanalalamika, mashabiki mnalalamika lakini hakuna kinachotokea ,wapi wanapofail? Kuna EFM kuna Wasafi kwaninni wasianzishe tour na events ambazo watawalipa wasanii pesa ya maana?
Ruge alliwahi uliza Tanzania kuna zaidi ya redio stations 100, sasa kwanini lawama za promo zitupiwe clouds tu? Sometimes inasemekana kuwa clouds inatengeneza wasanii fake kwa promo, swali kwanini kam ni fake media nyingine zinadandia hapo hapo na kuendelea kuwapa promo hao wasanii fake?
 
Binafsi nna maswali kibao....
1.ugomvi huu hasa chanzo ni nini?
chanzo ni maslahi binafsi ya Magodfather wa mziki wa bongoflava.
2.Mkubwa Fella yuko upande upi?
Yupo upande wa Joseph kusaga
3.tv ya WCB ni yao wao au wana sponsor?
TV NA WCB WEBSITE NI YA CLOUDS MEDIA GROUP
sponsor wao ni nani?
Sponsor wao ni JOSEPH KUSAGA
4.Ruge na Salaam wana bifuu lingine la personal?Salaam anaandaliwa na kKUSAGA kua the next RUGE MUTAHABA na JOSEPH KUSAGA.
5.mikataba ya Diamond kwenye karanga na perfume itakuwa canceled ?Mikataba ipo pale pale kama vile JOTI anavyotangaza Chama ndo Diamond anavyotangaza karanga za SMART INDUSTRY na CHIBU PERFUME ya mke wa KUSAGA
6.victims wa beef hili watachagua upande?.Victim n wale washinda INSTA wanaojua tukanana hata kazi hawataki..


Wasafi

DEVELOPER WAKE NI

Home setuplimited.

AMBAO SETUPLIMITED WAPO AFFILIATED NA

About Us - Clouds Media Group CLOUDS MEDIA GROUP

WANAOELEWA WAELEWE HIYO INAITWA FORENSIC AUDIT...OR FOLLOW THE MONEY STRATEGY
 

.Kwa hiyo wewe unamsaidia msanii ili baadaye aje kuwa mjasiliamali ? ,kwa hiyo huna mpango wa kuimlipa msanii,unajua tu akiwa maarufu hela zinakuja,sasa atakuwa vip mjasilia mali wakati hela ambayo unapasa kumlipa kuwa kama mtaji wake unashindwa.Mlipe mtu hela alafu baadaye ndio umlaumu kwa nini hujawa mjasilia mali .Hao akina Dr Dree,Lil wyne,Snoop ,P.diddy walilipwa hela na ndio maana leo hii wana mitaji ya kufungua biashara.

"Narudia tena nipe jibu linalo jitosheleza media nyingine zimeshindwa nini kutengeneza events zinazoeleweka zikawalipa hao wasanii ela nzuri? Maana wasanii wanalalamika, mashabiki mnalalamika lakini hakuna kinachotokea ,wapi wanapofail? Kuna EFM kuna Wasafi kwaninni wasianzishe tour na events ambazo watawalipa wasanii pesa ya maana?"

Jibu la hili swali hili hapa nishakujibu "CMG lazima watengeneze wasanii sababu wana FIESTA, after skull bash na hiyo haitoshi pale kwa mwaka kila mtangazaji ana event yake so wanatumia kigezo cha promo ili kuwabana wasanii (kwa mwaka msanii anaweza akapiga show zaidi ya 30 za CMG) , hizi redio nyingine kazi yao kupokea nyimbo za msanii yoyote na kuzipiga basi". na mfano wa event nimekupa Kilimanjaro Tour na Event za kwa fujo.Ukae ukijua sio wasanii wote wa Bongo fleva walitengenezwa na CMG ,kizazi cha kwanza cha Bongo fleva kimetengezwa na Radio one (Dj abubakar sadiki,Misanya bingi,John dilinga nk).

Clouds inatupiwa lawama sababu ya malipo wanawalipa kidogo ,nilikuuliza mbona hujasikia lawama hizi kwa KTM na kwa Fujo dj na walishaandaa show nyingi huko nyuma japokuwa KTM imesimama,kwa fujo kila mtu ana issue zake.(Hujanijibu).Narudia tena Jiulize kama mtu mzima,kwa nn wasanii wa walalamikie FIESTA tu na si KTM au kwanini wasanii walikuwa hawalamiki show zilizokuwa zikiandaliwa na Kwa fujo dj, jiulize wasanii tofauti tofauti kwa mda tofauti wote wanalalamika kitu kile kile kimoja ,huoni kuwa Kuna walakini au labda nawe mfaidika.
 
I need reference from BRELA.Kuna mdau mmoja humu alifungua uzi akatuonyeshea shareholder wa EFM na data kutoka TCRA,wewe zako zipo wapi.Tokea lini CMG ikamiliki website ya WCB and how.
 
Narudia tena in the capitalist world hulipwi unachostahiri bali ulichopatana.
Ofcourse bila kuwa mjasiriamali lazima msanii atafail maana mziki mara nyingi ni kipaji ambacho lazima ifike muda ushuke,
Sasa kumbe wana uwezo wa kutengeneza wasanii tena wakatengeneza wasanii ambao wana hit redio zote na Tanzania nzima. Basi ni haki yao ku rule the game kama hao wenfine wanashindwa. Katika ubepari, bepari siku zote anatazama faida na hasa akiwa monopoly. Sasa kumbe hao wengine wameshindwa kuwatengenezea wasanii platform inayoweza kushindana na clouds? Nini kinawafanya wengine washindwe na clouds waweze? So unakubari kwamba CMG ni master mind ya music industry ya TZ?
KTM iliishia wapi kama unasema walikuwa wanalipwa sana? si ilijifia mbali na shamra zake hazikuwa kwa kiwango cha clouds.
Kelele hazisaidii kwa zaidi ya miaka kumi watu wanapiga kelele lakini ikifika tu FIESTA kila msanii ndipo anaanza achia ngoma hata ambaye mwaka jana alikuwa anadai anaonewa.
Nipe jibu wengine wamefail wapi kutengeneza platform sawa na ya Clouds ambapo wasanii watapata promo na malipo yanayoeleweka? Kwanini wameshindwa?
 
I need reference from BRELA.Kuna mdau mmoja humu alifungua uzi akatuonyeshea shareholder wa EFM na data kutoka TCRA,wewe zako zipo wapi.Tokea lini CMG ikamiliki website ya WCB and how.
Yaleyale ya kumuuliza mjomba kwanini anatembea kwa miguu kama hujaweza hata kufollow the link unataka uelekezwe nn tena...inaweza kua nmekupa somo la chuo we bado sekondari
 
"Ofcourse bila kuwa mjasiriamali lazima msanii atafail maana mziki mara nyingi ni kipaji ambacho lazima ifike muda ushuke" Kumbe unajua sana msanii anahitaji hela ,ila unajitoa ufahamu.Siku zote hela humsaidia msanii kama mtaji wa kufungua biashara ili akishuka aweze kusurvive,sasa wewe msanii mnambana ata survive vip siku akiporomoka ndio wanishia kutangatanga, kwani hamna msani atakayekuwa no1 yy kila siku,wapeni hela ili siku wakishindwa kuwa wajasilia mali ndio tuwalaumu,hawa wasanii wanahitaji hela na huu ndio muda ya kupewa hela.

Nimekupa jibu mbona au hujalielewa,rudia paragraph la kwanza.Kumbe umekubari jamaa mabepari.CMG zamani walikuwa kweli ma mastermind lakini sio sasa KTK ulimwengu huu wa Social networkings (Insta,fb,twitter,Youtube etc ) na digital platform zina nguvu kuliko redio na TV (kasome tafiti uangalie rapidly growth ya social network ilivyoathiri wasikilizaji wa Radio na watizamaji TV).Kila siku graph ya CMG ina decay exponentially ,waangalie hawa WCB wanahit na kusurvive sababu wanajua kuitumia hizi social networkings,sasa fanya comaparison ya msanii wowote amabaye anapewa na promo na CMG na wasanii wa WCB in term of no views on Youtube,Boomplay chart from tanzania,trending ktk insta,fb na twitter,mauzo ya Itunes Kenya au chart za mtandao wowote ambayo nyimbo huweka watu wanadownload hapo utagundua jamaa influence yao ina decay vibaya sana.

Kilimanjaro sio sababu eti hawkuwa na mtaji bali ,wao wenyewe hawakulizika na uendeshwaji wa tuzo baada ya siasa za mateam kingia ktk mziki na wameamua kujitoa.

Wasanii wanaoachia ngoma si ndio hao wajinga mnaowapa promo kwa kigezo cha kuja kuwatumikia free ,baadaye wakifulia mnaanza kuwacheka na kuwachora ktk kipindi chenu cha SHILAWADU .Natamani nikujue ili niweke kidau na wewe ila nakuhakikishia baada ya miaka 3 .CMG watakuwa na hali mbaya sana tena sana (hifazi hii comment) na mimi yako nahifadhi na nitakutafuta baada ya miaka mitatu ,kwani ni uhakika 100%.
 
Yaleyale ya kumuuliza mjomba kwanini anatembea kwa miguu kama hujaweza hata kufollow the link unataka uelekezwe nn tena...inaweza kua nmekupa somo la chuo we bado sekondari
Acha stori za wauza kahawa,kuwa kama msomi,weka reference hapa,sio unaleta habari za zamani binadamu alikuwa nyani,hii ni jf watu wapo open kuongea chochote,mwaga hapa tuone hiyo WCB ni kampuni ambayo ipo registered.
 
Makampuni yote ni ya kibepari hakuna anayeanzisha kampuni ili kukunufaisha wewe huo ni uongo wa kiwango cha standard gauge,
Sasa kama si mastermind tena si ma monopoly kelele zote za kazi gani?
kwa mtazamo wangu bado ni bado wanashikiria mziki maana tofauti na WCB hakuna mwingine ambaye ameweza kusurvive na mbaya zaidi WCB hata vyombo vyao vya habari havijaweza kwasaidia wasanii wengine nje ya WCB hata habari za kituo chao zina revolve around diamond's family na WCB, kitu ambacho kinaweza kisiwe mwarobaini in the long run.
Inshort CMG bado inaushikiria mziki maana WCB ni 0.001% ya wasanii wa mziki walioko tanzania,
EFM ilisemekana itakuwa mbadara wa CMG lakini mpaka leo imeshindwa fanya hilo, mpaka sasa mbadara wa fiesra hajapatikana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…