GoldDhahabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2023
- 7,189
- 10,375
Ukiacha tabia za utekaji zilizoibuka nchini hivi karibuni na kasoro zinginezo ambazo zimekuwepo kwa miaka mingi, Tanzania bado ni kati ya nchi ambayo naamini Raia wa Congo wanatamani nchi yao ingekuwa na amani kama ya Tanzania.
Kama ikitokea kwa mfano, Baraza la Mawaziri la Congo DRC likapitisha azimio la kuisalimisha nchi yao ya DRC kwa Tanzania, kwamba Congo DRC iwe nchi moja na Tanzania, kwamba Rais wa Congo na mawaziri wote wa Congo wapangiwe majukumu mengine na Rais wa Tanzania, unafikiri ingekuwaje?
1. Tanzania ingekubali kuchukua nchi ya Congo DRC iwe sehemu ya ardhi yake ilhali ina migogoro lukuki?
2. Raia wa Congo wangelipokeaje hilo?
3. Machafuko ya Congo yangeweza kuisha?
4. Kama madai kuwa vurugu za Congo DRC zinachochewa na PK na M7 zina ukweli, wangeacha kufanya hivyo baada ya DRC kuwa ardhi ya Tanzania?
5. Wewe kama wewe ungekubali Congo DRC. iwe sehemu ya ya Tanzania? Kwamba Wakongo wawe raia Tanzania kama wewe ulivyo raia wa Tanzania?