Itakuwa sahihi CHADEMA kushiriki mazungumzo na Rais Samia huku Mwenyekiti wake akiwa ndani kwa kesi ya kubambikiziwa?

Huo ni mkutano wa Wenyeviti wa vyama vya siasa. Yeye akiwa M/kit wa CCM ambacho ni chama tawala. Je kwa Chadema kitakuwaje ambacho ni chama kikuu cha upinzani??
 
Utaratibu uliopangwa inaonekana watakutana kupitia umoja wa vyama chini ya Shibuda.
 
Utaratibu uliopangwa inaonekana watakutana kupitia umoja wa vyama chini ya Shibuda.
Bora wasihudhurie. Mkutano utageuka wa wakina TLP, TADEA, ADC n.k. kuonyesha jinsi wasivyokubaliana na agenda za Chadema. Itakuwa ni kupoteza muda kama ilivyokuwa kushiriki katika uchaguzi wowote chini ya mfumo tulionao sasa hivi. Vichwa vya habari vitakuwa " wapinzani wasema kuwa Katiba Mpya sio priority na serikali isiingilie uhuru wa Mahakama".

Amandla...
 
Umeona mbali!
 
Hakuna mazungumzo ya chadema yanaweza fanyika Ili Hali Mwenyekiti yupo ndani,
 
Wewe jamaa huwa nakushangaa sana!Dikteta Samia akisema kuwa anataka akutane na vyama vya upinzani huwa anamaanisha kuwa anataka akutana na vile vyama ambavyo ni mapandikizi ya CCM na vyama rafiki wa CCM kama vile ACT wazalendo,TLP,CUF na kadhalika na siyo chama pendwa cha wananchi-chadema.

Kwani hukumsikia hata alipokuwa anahojiwa na Kikeke kule BBC aliiponda sana chadema?
 
Huo mkutano wao utapuuzwa tu maana CHADEMA ndio wanaoaminika zaidi kama wapinzani
 
Ili wakamwombe msamaha au,kwani hajui kuwa hawatendei haki wapinzani?
KUSHIRIKI MAZUNGUMZO HAYO NI UWOGA

Sent from my TECNO CA7 using JamiiForums mobile app
 
Wewe umeandika utopolo,kishabiki,kiccm,kidikteta

Sent from my TECNO CA7 using JamiiForums mobile app
 
Tutatuma barua kwenye kikao hicho kwamba Mjumbe wetu kwenye mazungumzo hayo ni Freeman Mbowe , sasa kwa vile yuko jela basi hatutakuwa na mwakilishi , FULL STOP
 
Hii ni pasua kichwa,hapa kinachohitajika ni busara na hekima ili kulimaliza jambo hili,bila hekima hili jambo haliwezi kuisha kwa sababu CHADEMA hawana dola na waone matukio ya uonevu kutoka chama tawala yanavyoiandama chadema kama vile kufungwa bila sababu,kupigwa risasi Tundu Lissu na kuvuliwa ubunge,kutekwa tekwa ovyo na kubambikiziwa kesi,kunyang'anywa wabunge na kuwaapisha kupitia Ndugai,hivyo inabidi busara ya hali ya juu na hekima vitumike.
Kukutana na rais wakati mheshimiwa Mbowe akiwa ndani haipendezi hata kidogo,lakini kwa namna ya kipekee ni jambo jema kufumba macho na kuziba masikio ili kukutana na rais ili kueleza yote bayana na kutafuta ufumbuzi wa maswala haya yanayosumbua siasa za Tanzania,ili kuleta na kujenga umoja na mshikamano pamoja na upendo wa dhati kwa Watanzania wote.
 
Kwa kweli nitashangaa mshangao wa kunitoa roho.
CHADEMA watashiriki vipi huku wamefungwa pingu mikono, miguu na kufungwa kutambaa machoni?
CHONDE CHONDE CHADEMA msituue kwa pressure.
Sikiliza hasira hasara kumbuka ccm hawana cha kupoteza wenye shida ni sisi hivyo inabidi tujishushe tuwasikilize na tujadiliane nao hasa kesi ya Mbowe na wale Wabunge kumi na tisa,busara itumike kumaliza hii changamoto.
 
Safi sana hapo nimekuelewa mkuu.
 
Sikiliza hasira hasara kumbuka ccm hawana cha kupoteza wenye shida ni sisi hivyo inabidi tujishushe tuwasikilize na tujadiliane nao hasa kesi ya Mbowe na wale Wabunge kumi na tisa,busara itumike kumaliza hii changamoto.
Unajadilia nao nini sasa kwa mfano?
Kama polisi wanatumika kuvunja sheria na katiba si bora kushughulika na hao mapolisi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…