Itakuwa sahihi CHADEMA kushiriki mazungumzo na Rais Samia huku Mwenyekiti wake akiwa ndani kwa kesi ya kubambikiziwa?

Teyari tumesikia taarifa juu ya Rais Samia kukutana na viongozi wa vyama vya siasa hapa nchini katika siku na tarehe ambayo bado haijawekwa wazi kwa umma huku mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Bwana Freeman Mbowe akiwa mahabusu kwa kesi inayolalamikiwa kuwa ni ya kubambikiziwa.

Kwa hali ilivyo, ni wazi mkutano huo utafanyika huku Mwenyekiti huyo wa CHADEMA ndani kwani si rahisi atoke mapema unless kuwe na maahikinikizo makubwa ya ndani na nje ya nchi kwani danadana za kesi yake tayari zimeshaanza na bila shaka zitaendelea.

Swali ni je, katika mazingira haya, itakuwa sahihi kwa CHADEMA kushiriki katika hayo mazungumzo huko mwenyekiti akiwa ndani kwa kesi inayodaiwa kuwa ni ya kubambikiziwa?

Au itakuwa ni busara kwa CHADEMA kugomea mazungumzo hayo kama shinikizo la kutaka Mbowe atendewe haki katika hiyo kesi au kwa sharit la kutakai kes hiyo ifutwe kama haiwezi kuendesha.kwa haki?

Binafsi naamini kitendo cha Mbowe kuongoza harakati za kudai katiba mpya pamoja na yeye kufunguliwa hii kesi inayopingwa Karibu kila kona ya hii dunia, ni moja ya mambo yaliyoisukuma serikali kukutana na wapinzani katika harakati za kujisafisha mbele ya.umma wa watanzania na dunia kwa ujumla, hivyo ushirika wa CHADEMA katika mazungumzo haya ni muhimu sana.

Sasa narudia swali langu hili:
Je, CHADEMA washiriki hayo mazungumzo wakiwa na agenda ya kutaka Mbowe afutiwe hiyo kesi inayodaiwa kuwa ni ya kubambikiziwa au wasishiriki kabisa kama shinikizo la kutaka Mbowe aachiwe au atendewe haki katika hiyo kesi?

Nawasilisha.
Mazungumzo yasito jikitankwenye Katiba Mpya na Tumr huru ya Uchaguzi ni mazungumzo Fake.
 
Inategemea format ya mazungumzo yenyewe. Kama yatakuwa ya vyama vyote kwa jumla chini ya uongozi wa Shibuda na Msajili wa Vyama ni bora wasiudhurie maana hawatapata nafasi ya kutoa dukuduku zao kwa kikamilifu. Aidha, wataipa serikali kisingizio cha kusema kuwa pamekuwa na mazungumzo na wapinzani.

Kama format itakuwa ya wao peke yao na serikali au wao pamoja na vyama vya ACT Wazalendo, CUF, NCCR Mageuzi ( pengine na CHAUMMA)mazungumzo yatakuwa na tija zaidi na hivyo itakuwa busara wakihudhuria.

Amandla...
Hahahaa Vyama vinginr ni Raba stamp ya Mtungi
 
Mtoa mada wewe ni fala kama mafala wengine, kwahy chama cha siasa ni chadema tuu.? Nyie nyie mnasema polisi wanaingilia kazi za mahakama halafu tena nyie nyie wanachadema mnasema mbowe amebambikiwa kesi sasa hapo napo sio kuingilia mahakama.?
Natamani huo mkutano uwepo hata Leo ili tuone wanaume mkisusa kama wanawake, makamu mwenyekiti c yupo bc yeye aje.
Mataga mwenye stress zake🤣🤣
 
Mkuu, tusisahau kuwa kuna vyama vya "upinzani" ambavyo mgombea wao wa Urais alikuwa ni wa CCM. Vyama kama hivyo unategemea kweli vitadai Katiba Mpya au vitaweza kuona mapungufu ya serikali iliyopo?

Amandla...
Ili mkutano wao ukubalike ndani na nje ya nchi, ni lazima watatoa mwaliko kwa CHADEMA na hapo ndipo CHADEMA watatakiwa kupima kwa makini maamuzi yao ya ama kukubali au kuukataa huo mwaliko.
 
Teyari tumesikia taarifa juu ya Rais Samia kukutana na viongozi wa vyama vya siasa hapa nchini katika siku na tarehe ambayo bado haijawekwa wazi kwa umma huku mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Bwana Freeman Mbowe akiwa mahabusu kwa kesi inayolalamikiwa kuwa ni ya kubambikiziwa.

Kwa hali ilivyo, ni wazi mkutano huo utafanyika huku Mwenyekiti huyo wa CHADEMA ndani kwani si rahisi atoke mapema unless kuwe na maahikinikizo makubwa ya ndani na nje ya nchi kwani danadana za kesi yake tayari zimeshaanza na bila shaka zitaendelea.

Swali ni je, katika mazingira haya, itakuwa sahihi kwa CHADEMA kushiriki katika hayo mazungumzo huko mwenyekiti akiwa ndani kwa kesi inayodaiwa kuwa ni ya kubambikiziwa?

Au itakuwa ni busara kwa CHADEMA kugomea mazungumzo hayo kama shinikizo la kutaka Mbowe atendewe haki katika hiyo kesi au kwa sharit la kutakai kes hiyo ifutwe kama haiwezi kuendesha.kwa haki?

Binafsi naamini kitendo cha Mbowe kuongoza harakati za kudai katiba mpya pamoja na yeye kufunguliwa hii kesi inayopingwa Karibu kila kona ya hii dunia, ni moja ya mambo yaliyoisukuma serikali kukutana na wapinzani katika harakati za kujisafisha mbele ya.umma wa watanzania na dunia kwa ujumla, hivyo ushirika wa CHADEMA katika mazungumzo haya ni muhimu sana.

Sasa narudia swali langu hili:
Je, CHADEMA washiriki hayo mazungumzo wakiwa na agenda ya kutaka Mbowe afutiwe hiyo kesi inayodaiwa kuwa ni ya kubambikiziwa au wasishiriki kabisa kama shinikizo la kutaka Mbowe aachiwe au atendewe haki katika hiyo kesi?

Nawasilisha.
Negotiate while advancing
 
Back
Top Bottom