binafsi, siamini kama Dr Slaa atashinda mwaka huu,maana Chadema hawakuwa wamejiandaa au kumwandaa slaa kimkakati agombee urais, na kama maelezo yanayotolewa kuwa alilazimishwa ni sahihi basi timing ya yeye kuingia kwenye kinyang'anyiro ilikuwa somehow too late. hili linatokana na kuwa asilimia kubwa ya watanzania wanakaa vijijini,bado hawana ufahamu wa kutosha na pia hawamjui kiundani slaa, achana na wale walio kwenye miji midogo yenye maingiliano ya kibiashara na kuwa na makabila mchanganyiko, huko upinzani una nguvu.
lakini binafsi naamini bado uamuzi wa dr slaa kugombea mwaka huu ulikuwa sahihi maana anajitangaza zaidi ili come 2015 awe anafahamika zaidi,pia iwapo atashindwa urais na kubakia kuwa kiongozi wa chama,naamini atajitahidi kujenga chama kiwe na nguvu zaidi kwenye grassroot kuliko juu tu,naamini atajitahidi kuelimisha watanzania kupitia operesheni mbalimbali. kwenye operesheni zilizopita mbowe alikuwa ndio akiziongoza lakini hajagombea urais so naamini iwapo operesheni zijazo akiziongoza slaa kisha yeye mwenyewe akigombea 2015 ukijumlisha kuwa mwaka 2015 sidhani kama CCM watakuwa na kiongozi madhubuti anayechagulika kuwa rais ,basi ushindi unaweza kuwa wa upinzani
Acha kutokujiamini,
Mkapa alijiandaa vipi?? Aliiingizwa tu na Mwalimu Nyerere? Mwinyi aliajiandaa vipi? JK je? Tatizo la WaTanzania ndiyo hilo; all the time hawajiamini. Factors zipo very open:
1. Pamoja na Mkapa kusaidiwa kwenye kampeni na Nyerere lakini Mrema alifikisha karibu Kura 40%. Na unajua factor ya Mwalimu na impact yake.
2. WAtu wa Vijijini; vijiji vya wapi? Sasa hivi siasa zipo kanisani, misikitini kote huko watu wanajadili haya, ndugu zao nao wapo kwenye mitandao; simu za mikono ndiyo hizo; sms hadi Tunduru.
3. Kikwete kaboronga mno; na sasa waTanzania wengi washakuwa hawana sympathy, nae, hata aanguke mara kumi;
CCM wana-chance moja tu; kubuni kuiba kura October 31st.
4. Vyama vyenye nguvu vipo vitatu sasa hivi, CCM, Chadema, na CUF. CCM na CUF ina wanachama ambao wanaitwa 'base"; yaani wale wa kudumu. Chadema base ni ndogo sana lakini wanategemea zaidi independent kama sisi. Base ya Chadema ni wasomi, Liberals na independent kwa mwaka huu.
Conservatives wengi wako CUF na CCM; lakini wale wenye rogho nyepesi wengi washaingia CHADEMA nao ndiyo Chadema atawavuna.
Kama uchaguzi utafuata haki, CCM, CHADEMA na CUF kunawezekana kabisa kisitokee chama kitakachofikisha 51% ya kuwa na Rais.
Therefore Dr. Slaa ana nafasi kubwa sana hasa kuchukua wanachama wengi wa CCM kupigia kura yeye.