Itakuwaje kama Ali Kiba na Diamond wataamua kuwa Juma Nature na Inspekta Harun wa zama hizi?

Itakuwaje kama Ali Kiba na Diamond wataamua kuwa Juma Nature na Inspekta Harun wa zama hizi?

GadoTz

JF-Expert Member
Joined
Nov 20, 2014
Posts
370
Reaction score
636
Juma Nature na Inspekta Harun ni wasanii wa muziki wa kizazi kipya waliofanikiwa kuwa na ushawishi mkubwa sana kwenye tasnia ya bongo fleva kipindi fulani kilichopita. Ni wasanii ambao kila mmoja kwa nafasi yake walifanikiwa kuandika rekodi mbalimbali zilizowafanya kuwa juu sana kimuziki.

Juma nature alifanikiwa kuweka rekodi ya maudhurio makubwa katika maonyesho ya uzinduzi wa album zake za ‘Nini Chanzo' na ‘Ugali'. Pia alifanikiwa kwenye mauzo ya album zake na kuweza kufanya show nyingi sana ndani na nje ya Tanzania.

Inspekta Harun akiwa kama solo na memba wa kundi la ‘Gangwe Mob' walifanikiwa kujaza watu wengi sana wakati wa uzinduzi wa album yao ya ‘Simulizi la Ufasaha' na kuweka rekodi ya kipekee. Kupitia kundi lake waliweza kumiliki design za nguo zao zilizokwenda kwa jina la Gangwe Gear na website yao vitu ambavyo ni vikubwa sana kwa nyakati izo kufanywa na msanii wa kibongo na Afrika ya mashariki.

Inspekta Harun anakumbukwa kwa vibao vyake vilivyotamba kama ‘mtoto wa geti kali', ‘Maisha ya uswazi', ‘Asali wa moyo', ‘Pamba nyepesi' na vingine vingi alivyoimba mwenyewe au kwa kushirikishwa.

Juma Nature anakumbukwa kwa hits zake kama ‘Mgambo', ‘Sitaki demu' ‘Inaniuma sana' ‘Hakuna kulala', ‘Kighetogheto' na nyinginezo.

Juma Nature na Inspekta Harun walikuwa ni wasanii wanaoshabiiana mambo mengi, kuanzia uhandishi wa nyimbo zao unaoelezea maisha halisi ya uswahilini na kiasi kikubwa namna ya kughani ambapo walitumia staili iliyojulikana zaidi kama ‘rap katuni', pia maeneo wanayotokea ambayo ni ya uswahilini haswa, na hata pilika zao wakati wanaanza muziki inasemekana walishawahi kuangaika pamoja kwa namna moja au nyingine.

Kushabihiana huku kulipelekea washabiki wao kujaribu kuwalinganisha na kuwapima uwezo wao wa nani ni zaidi ya mwingine. Hii ilichochea kuibua mtafaruku baina ya wasanii wawili, wakatofautiana mpaka wakaunda makundi kwa washabiki wao ambao walikuwa wanajaribu kuwashindanisha . Mgogoro ukakuwa zaidi ukichochewa na vyombo vya habari pamoja na vijembe walivyorushiana kwenye nyimbo zao.

Baada ya ushindani na mgogogro uliofukuta baina yao kwa muda mrefu, wakaaamua kuweka chini tofauti zao na kufanya kazi ya pamoja chini ya mtayarishai nguli P Funk Majani.

‘Mzee wa busara' ni kazi waliyofanya pamoja Inspekta Harun na Juma Nature, kazi iliyopokelewa vizuri sana na washabiki wa bongo fleva, na ikageuka kuwa gumzo kila kona ya Tanzania. Ni kazi iliyowaunganisha pamoja hawa mahasimu wawili wakageuka kuwa marafiki, na pia ikawaunganisha pamoja na mashabiki wao kwa ujumla. Lengo ilikuwa kufanya albam ya pamoja kitu ambacho hata hivyo hakikufanikiwa. Nachoweza kusema ‘mzee wa busara' ni moja ya nyimbo zilizosaidia kuisukuma tasnia ya muziki wa kizazi kipya kwenda mbele zaidi.

jnbc.jpg

Kina-na-Diamond.jpg

Leo hii ukizungumzia muziki wa bongo fleva, watu wanausimamisha ni mastaa wawili Ali Kiba na Diamond Platnumz. Diamond na Ali Kiba ni wasanii ambao kila mmoja amefanya mambo makubwa na kujizolea mashabiki wengi. Ni wasanii wanaofanya kazi nzuri na zinazopendwa ndani na nje ya Tanzania.

Ali Kiba ana hit songs kama ‘Cinderela', ‘Nakshi nakshi', ‘Hadithi', ‘Far way', ‘Single boy' ‘mwana' na nyinginezo. Kiba amefanikiwa kufanya maonyesho kwenye nchi mbalimbali za Ulaya na Marekani, amefanikiwa kufanya kazi moja na mwanamuziki nguli wa Marekani R Kelly.

Diamond Platnumz, amefanikiwa kutengeneza nyimbo zilizotamba sana kama ‘Kamwambie', ‘Mbagala', ‘Mawazo','Nitarejea','Kesho' na ‘Number one' ‘Mdogo mdogo'. Amefanikiwa kufanya maonyesho makubwa ndani na nje ya nchi pia amefanya kazi na wasanii wakubwa wa Afrika kama D Banj, Davido, Iyanya na wengineo.

Inspekta na Nature walifanya wimbo wa pamoja ukawa gumzo, ila hawakufanikiwa kutoa album. Itakuwaje kama Ali kiba na Diamond watafanya sio tu wimbo wa pamoja bali album nzima? Naamini itaweka rekodi ya aina yake ambayo haijawahi tokea kwenye muziki wa kizazi kipya. Kisha baada ya hapo tuwaone kwenye ziara ya pamoja sehemu mbalimbali. Tuwaone na mashabiki wao ambao ni wengi sana wakiunganika kuwaunga mkono kwenye kazi zao za pamoja. Na kuzidi kuusukuma mbele muziki wetu wa Tanzania kimataifa.

Muziki wa sasa ni biashara kubwa na kwenye biashara hakuna uadui wa kudumu. Penye fursa watu wanaojua biashara uweka tofauti zao kando na kutumia fursa kutengeneza faida. Nje ya kutengeneza faida Diamond na Kiba wana nafasi ya kutengeneza historia mpya na ya kipekee kwenye muziki wa nyumbani na kuzidi kuupa nguvu na ushawishi muziki wetu.

Naamini hakuna kinachoshindikana.
 
Ukichunguza kwa makini hao wasanii wa zamani wa tmk yaani nature na haroun ni waswahili. Hata kiba na diamond wote waswahili. Hilo ndiyo shida, makelele mengi yasiyokuwa na maana. Hao wasanii ni waswahili kinoma, washamba sana hao tandale, k/koo mpaka temeke.
 
Hadi sasa baada ya kufanya uchunguzi nimegundua kwenye hii sintofahamu kati ya Alikiba na Diamond nimejiridhisha kuwa Alikiba ndio mwenye tatizo na ana nufaika na hii inayoitwa sintofahamu kati yao na Diamond!
 
Ukichunguza kwa makini hao wasanii wa zamani wa tmk yaani nature na haroun ni waswahili. Hata kiba na diamond wote waswahili. Hilo ndiyo shida, makelele mengi yasiyokuwa na maana. Hao wasanii ni waswahili kinoma, washamba sana hao tandale, k/koo mpaka temeke.

kuna Pont Unataka Kuiongea Hapa!
 
Hadi sasa baada ya kufanya uchunguzi nimegundua kwenye hii sintofahamu kati ya Alikiba na Diamond nimejiridhisha kuwa Alikiba ndio mwenye tatizo na ana nufaika na hii inayoitwa sintofahamu kati yao na Diamond!

Kuna ukweli
 
Diamond mjanja sana hawezi kumshirikisha ali kiba kwa siaizi maana yupo juu kuzidi kiba,ikitokea wameimba pamoja, basi kiba ndio ata-gain lakini diamond hatanufaika kivile, ni sawa na kile kipindi diamond alivyoimba na davido kwenye number one, kile kipindi davido alikuwa juu kitu kilichofanya na diamond alikuwa chini mno, ngoma ilivyotoka status ya diamond ipande huku ya davido ikiwa pale pale, SIKU ZOTE MTU WA JUU AKIFANYA KAZI NA MTU WA CHINI, WA CHINI ATAONGEZEKA WA JUU ATABAKI PALE PALE
 
Mshaona Nasibu hakamatiki tena mission zenu zakumshusha zmeshindikana mnaanza collable.....TO HELL......Yan tena Ally Kiba akae mbali na Nassibu kama ilivo Mashariki na Magharibi.Labda amuombe amuonganishie kwa fally ipupa.
 
Nnachoamini mimi mameneja wa Nassibu watamtupa mbaaaali kabisa kama hyo itakuwepo.
 
Usnitch uliofanyika ile siku fiesta kwa Nasibu kuzomewa..wengi wanaomsapoti Ally Kiba walitaka ile hali iwe endelevu na hata Ally mwenyewe alitaka hivohivo lakini Zito Kabwe akampiga break.Siku zote snitch mungu anamuumbua.Tunangoja DIAMONDS ARE FOREVER aje na watu wake wazomee tena.Hakuna COLLABLE na SNITCH.
 
kuna Pont Unataka Kuiongea Hapa!

Kiongozi nimegundua nchi hii kuna tabaka la wajinga na hao hao wajinga wanajiona wajanja na wana akili. Amini kiongozi wangu, waswahili ndiyo wapo hivyo hivyo hawawezi vitendo wakatulia kimya, wanapenda maneno zaidi
 
Mawazo chanya itakuwa project kubwa ila ukimalizka unafiki wa wapambe kutumia neno washahili mimi linanipa shida kidogo.
Wapatikane wenye busara wakae nao mambo yatakwenda ila kuna wale watu waitwao mbuzi wa mbele hatari hao mapovu huwatoka na hata wanavyotoa comments utadhani ndo wasanii wenyewe au wasemaji wao.
 
Mshaona Nasibu hakamatiki tena mission zenu zakumshusha zmeshindikana mnaanza collable.....TO HELL......Yan tena Ally Kiba akae mbali na Nassibu kama ilivo Mashariki na Magharibi.Labda amuombe amuonganishie kwa fally ipupa.

Tofauti za wasanii zinachagizwa wakati mwingine na fans wao (either kwa kuanzishwa ama kuchochewa).

Ulichoandika hapa ni kama kutia kuni zaidi kwenye tofauti zao na ni kama unakereka sana kuona wanaungana unapenda hali iendelee hivi hivi. Wewe kama shabiki ama mdau wa muziki what do you benefit from this kind of conflict tena kwa watu ambao wako kwenye industry moja ya muziki?

I concur na mdau mmoja aliyewahi kuleta thread hapa kwamba kwa kiasi kikubwa bifu la wasanii hawa wawili linachagizwa sana na fans wao, mara team fulani na team fulani...hebu tujitafakari steps zetu jamani kwa nia njema ya kuendeleza hii fani ya muziki positively.
 
Diamond mjanja sana hawezi kumshirikisha ali kiba kwa siaizi maana yupo juu kuzidi kiba,ikitokea wameimba pamoja, basi kiba ndio ata-gain lakini diamond hatanufaika kivile, ni sawa na kile kipindi diamond alivyoimba na davido kwenye number one, kile kipindi davido alikuwa juu kitu kilichofanya na diamond alikuwa chini mno, ngoma ilivyotoka status ya diamond ipande huku ya davido ikiwa pale pale, SIKU ZOTE MTU WA JUU AKIFANYA KAZI NA MTU WA CHINI, WA CHINI ATAONGEZEKA WA JUU ATABAKI PALE PALE

Kwahiyo Ally Kiba alipoimba na R Kelly alimzidi Kelly? Watu maskini siyo wakukaa nao karibu maana hata mawazo yao ni umaskini mtupu.
 
Back
Top Bottom