Itakuwaje siku Muungano ukivunjika?

Na uvunjike,
Raia walio na nafuu ya muungano ni wazanzibar
Acha wajitegemee
-Jeshi litapata kazi ya kufanya badala ya kudeal na upinzani
Mimi si muuminiwa muungano kwa namna navyowaona na kuwachukulia wazenji wanaojihisiwao ni waarabu,masharti kibao mbongo anapoenda kwao lakini wakija huku wanajisahau
 
Simba na Yanga wakicheza mvua ya mawe itamwagikaaa
 
Tutafanya sherehe ya kufa mtu!
 
Na uvunjike tu, kwani una faida gani kwa mtanganyika?
 
Huenda mabadiliko yanayozuiwa leo ikawa ni mwanzo wa mabadiliko ya kweli.
 
Siku hiyo Zanzibar itakufa kifo cha mende ndembendembe
 
Siku hiyo jw litawapiga polisi na hapo ndipo ccm nayo itatoka madarakani maana jw linatakuwa limexhoja uonevu wa polisi kwa wananchi
 
Muungano ukivunjika, Hakutakuwa na sherehe za Muungano kwenye kalenda.
 
Badala ya kujadili hoja wewe umepaniki. Mmoja wa waasisi wa huu muungano aliwahi kusema muungano ni sawa na koti tuu likikubana unalivua. Mzee mwingine aliwahi nukuliwa akisema angekuwa na uwezo kisiwa hiki angelikisogeza mpaka katikati ya bahari ya hindi. Sasa wewe mwenzangu na miye uliyetoka huko Kipindimbi ndani ndani, mipovu inakutoka 🀣🀣...mleta uzi amehoji tuu kwamba "kama" yaani just assumption, wewe povu kama lotee..
 
Tanganyika itayumba sababu itakuwa Haina Rais alipo ni Rais wa Tanzania hivyo TZ ikifa Tg itayumba!
Zenj haita yumba sababu Wana Kila KITU KUITWA Taifa.
Tatizo history hamfuatilii mko bize na mipira Vs Mondi na Kiba. Umewahi kufuatilia Tanzania iliundwaje baada ya muungano? Ukiacha kuchanganya udongo na mengineyo ukweli ni kwamba vitu vingi vya iliyokuwa inaitwa TANGANYIKA vilibadilishwa na kuwa TANZANIA...
 
Asante kwa kunisaidia kulielewesha hilo
 
Ndio umebishia Nini??
Yaani mpaka mishipa ya shingo inakutoka πŸ™„πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†
 
Wait kwanza tukitengeneze hiki kisiwa kiwe Dubai ndogo, then ukuta Kwa Berlin utavunjwa tu iwe isiwe

Nchi ya mazuzuland watabaki wanapambana na madeni yao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…