Itanichukua muda gani kuhitimu mafunzo ya kuongea kingereza fasaha?

Itanichukua muda gani kuhitimu mafunzo ya kuongea kingereza fasaha?

Inategemea na implication yako, unataka kumaanisha nini? Lugha hii sio kama kiswahili, mtu anaweza kusema sentence moja ila ikawa na implications tofauti.

Hiyo ni kauli mbiu yetu , ndio maana nkaja kwa wataalam. Nina hamu kwenda Davos mwaka huu
 
Nauliza wadau;

Ni muda gani inaweza kunichukua kusoma na kuhitimu kwenye taasisi kama British Council na kuhitimu uelewa wa lugha ya kiingereza cha kuniwezesha kuwasilisha hoja katika hadhara yoyote hasa za kimataifa?

Nahitaji kuingia chimbo kidogo, hiki cha "This is Musa, who is this? na This time tomorrow" naona vinaniangusaa
Tafuta na usome vitabu vingi vya tamthilia unazozipenda kwa lugha ya Kiingereza. Hata kama ni comic books. Viwe vyenye hadith fupi fupi na za kufurahisha.

Kwa kuvisoma hivi vitabu vitakuongezea msamiati wako na vitakuonesha namna maneno ya Kiingereza yanavyotumika.

Kujifunza kwa kuizungumza lugha kunasaidia kama upo sehemu ya wenyeji wa lugha unayojifunza.
 
Shukrani mkuu, nitajitahidi kufuata ushauri wako na wa wengine ili ndoto yangu itimie
 
Huo muda haujulikani, kuna wengine wanaizoea lugha ndani ya miezi 6 na kuna wengine wamesoma mpaka PhD lakini kuunda hata sentensi ni mtihani mgumu sana.
 
Ras Simba hapo amenyoosha mikono, jamaa lina kichwa kizito ni mwisho wa maneno! Kumbe zile takwimu lilizokuwa linatumwagia ni za uongo, iweje lishindwe kutema yai muda wote huo?
Hahahaa aisee
 
Kwa rasi simba anafundsha miez mitatu tu 150000 usipoelewa anakurudishia ada yako[emoji3]

Hivi ya kurudishiwa pesa huwa ni kweli au moja ya promo tu ya Ras Simba, hivi kuna shuhuda yoyote aliwahi rudishiwa pesa nacho jua ktk kujifunza kitu tunatofautiana muda wa kushika sasa wale 'slow learners' inakuwaje kwa huyu mkuu Ras au ndo kanuni zake hashindwi mtu
 
Hio ni promo tu. Maana ninaweza kujifunza kwake afu niseme sijaelewe japo nimeelewa, ili mkwanja wangu urudishwe
 
Hivi ya kurudishiwa pesa huwa ni kweli au moja ya promo tu ya Ras Simba, hivi kuna shuhuda yoyote aliwahi rudishiwa pesa nacho jua ktk kujifunza kitu tunatofautiana muda wa kushika sasa wale 'slow learners' inakuwaje kwa huyu mkuu Ras au ndo kanuni zake hashindwi mtu
Sijajua kama ni kweli mana hata mi sijawahi kusikia alierudisha ada[emoji23]labda wote huwa wanaelewa[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Hahahaha! Kifyatu Uko Sahihi Lingala Ndiyo Asili Yangu Tulihama Kisangani 1967 ndiyo kuhamia tanzania mkoani mwanza na tumetoka huko tukiwa wadogo
 
Nauliza wadau;

Ni muda gani inaweza kunichukua kusoma na kuhitimu kwenye taasisi kama British Council na kuhitimu uelewa wa lugha ya kiingereza cha kuniwezesha kuwasilisha hoja katika hadhara yoyote hasa za kimataifa?

Nahitaji kuingia chimbo kidogo, hiki cha "This is Musa, who is this? na This time tomorrow" naona vinaniangusaa
Itategemea juhudi zako na fursa utakazopata la msingi shule kama hiyo ya British Council inakujenga na kukutayarisha. Hivyo usikatishwe tamaa na mtu. Go, go, go, utafanikiwa.
 
Inategemea na level uliyopo kama ni beginner, intermediate au advanced learner. Wao watakupima kwa test kujua level uliyopo then utaanza kusoma...Miezi 3 unaweza kuanza kusikiliza hotuba za Trump km upo serious ktk kujifunza in case km ni advanced learner.
Noo,
Trump asimsikilize.
Zaidi kashfa na mitusi halina jipya lile zee.
 
Nauliza wadau;

Ni muda gani inaweza kunichukua kusoma na kuhitimu kwenye taasisi kama British Council na kuhitimu uelewa wa lugha ya kiingereza cha kuniwezesha kuwasilisha hoja katika hadhara yoyote hasa za kimataifa?

Nahitaji kuingia chimbo kidogo, hiki cha "This is Musa, who is this? na This time tomorrow" naona vinaniangusaa
It's not about time, it's all about how passionate are you about learning English. The key to mastering any language is to open your mouth and speak that language without having to pay much attention on grammar. Otherwise, you will learn English for the rest of your life and still not being fluent.
 
Hakuna kitu kama hicho Tanzania, ukitaka kujifunza lugha ni lazima uende mahali ambapo lugha hiyo inaongewa, na ndiyo maana wote wanaojitapa wanajua Kiingereza hapa Bongo ni waongo, hawajui chochote!

Hivyo ukitaka kujifunza lugha ni lazima uiongee, hivyo nenda nchi wanaoongea kiingereza kila siku kama Uganda au hata Kenya na kwa Kenya ukifika huko usiongee Kiswahili!

Au kwa hapa Bongo tafuta rafiki mgeni asiyejua Kiswahili!
It's a big lie. I know many folks who went in the UK and US and stayed there for over 5 years but when they came back to Tanzania their English was just like they had never been to English speaking countries.
My point is, you don't have to go to UK to become fluent in English, I personally went to British council and learn English for 10 weeks. After that my English is as good as that of Queen. Remember this, being fluent in English doesn't mean you won't be making grammatical mistakes, even native English speakers makes lots of grammatical mistakes.
The key to becoming fluent in any language is
1. SPEAK
2.SPEAK
3.SPEAK
4.OTHERS
 
*JIFUNZE KINGEREZA KWA KISWAHILI*
Anza masomo nami mwezi huu 2018.wa pili kwa gharama nafuu kabisa, *jifunze kingereza kwa kiswahili* kupitia WhatsApp pekee tutajifunza kwa video, voice note, picha nk kwa ufasaha..hata kama hujui hata a.
Wasiliana nami *mwalimu wa kingereza 0753093869 baada ya kuelewa *kingereza fasaha* tutakula ajira ukihitaji katika shule yetu ya *Juarez academy* au ajira za online,
ya kuhitimu vizur na ajira papo hapo. Huu ndo mfano wa masomo yetu, karibu saana.
Kumbuka: ujuapo kingereza fasaha utaweza kufanya kazi kwa kujiamin kwa taaluma uliyonayo popote duniani.
Pia uki SHARE kwa group 10 ,utafundshwa buree kwa mwezi 1
*ada kwa mwezi ni sh.20000 tu,watu 30 wa kwanza mtapTap na kitabu*

Somo la 1

(SECTION A; TENSES IN THE ACTIVE VOICE )

(A)Simple Tenses :

1. Simple Past Tense ( ‘li’)
- Wakati huu huongelea jambo lililofanyika na kukamilika mara moja wakati uliopita.
Mifano ; tulikuja ,walitembea, alicheza.
- Wakati huu huashiriwa na silabi ‘li’ ambayo hufanya tutambue kuwa tunaongelea jambo lililofanyika mara moja na likamalizika kufanyika katika wakati uliopita. Hii silabi ‘li’ ni lazima iunganishwe na kitendo moja kwa moja kabla ya kitendo. Mfano ; ‘Tuliimba’, tofauti na ‘Tulikuwa tunaimba’ ambapo ‘li’ imefuatiwa na kifungu ‘kuwa’ na sio kitendo. Katika maneno ‘tulikuwa tunaimba’, kitendo ‘imba’ kimetanguliwa na ‘na’ na sio ‘li’ kwa hivyo maneno hayo hayapo katika wakati huu wa Simple Past Tense, ‘li’.

Kanuni za kutumia Simple Past Tense ‘li’

a) Sentensi za taarifa/kutoa taarifa
Katika wakati huu, huwa tunapoelezea jambo tunatanguliza mtendaji wa jambo, (I/We/You/They/He/She/It) kisha tunafuatisha kitendo moja kwa moja kikiwa katika umbo la wakati uliopita.
Mfano ; - kitenda ‘enda’ ni ‘go’. Umbo lake la wakati uliopita, yaani ‘-lienda’ ni ‘went’. Tutatanguliza mtendaji wa jambo kisha tufuatishe neno ‘went’.

Sentensi za mifano;
- Juma alienda. ………. Juma went.
- Tulienda. ……… We went.
- Basi liliondoka. ……. The bus left.
- Nilicheza. ……. I played.
- Uliimba. ….. You sang.
- Walikimbia. ….. They ran.
- Maria alipika. ……. Maria cooked.
NB : Hatuweki kitu chochote katikati mwa mtendaji na kitendo.

b) Kuuliza maswali katika Simple Past Tense

- Maswali katika wakati huu huanzia na neon ‘did’. ‘Did’ ikitumika ni lazima kitendo kiwe katika umbo la kawaida kwa sababu ‘did’ ina ‘li’ ndani yake hivyo ‘li’ nyingine haihitajiki. Ina maana hiyo ‘did’ tayari imeshawakilisha wakati uliopita.
- ‘Did’ hufuatwa na nafasi inayouliziwa swali.
Mifano ya tafsiri :
- ‘Did Juma _______ ?’ …….. ‘Je, Juma ali______?’
- ‘Did they _______ ?’ ………. ‘Je, wao wali______ ?’

Sentesi za mifano :

1. Did Juma go?
Je, Juma ali enda ?

Jibu ; ( Hapana, hakuenda)…..( Kukanusha)
No, he didn’t go.
Au ; ( Ndio, alienda)…. Kukubali
Yes, he went.

2. Did she cook?
Je, alipika?

Jibu ; ( Hapana, hakupika)…..Kukanusha
No, she didn’t cook.
Au ; Ndio, alipika….. (Kukubali)
Yes, she cooked.

NB ; Tukiongeza neno ‘did’ katikati mwa jibu la kukubali, huwa ni kuweka msisitizo kama vile ambavyo kwa Kiswahili huwa tunaandisha sauti ili kuweka msisistizo ila sasa kwa Kingereza sauti haipandishwi ila msisitizo upo pale pale.

Mifano ; 1. Did Juma go ? …… Je, Juma alienda?
- Yes, he did go. ….. Ndio, alienda! (KWA MSISITIZO)

2. Did they cook? …….. Je, walipika?
- Yes, they did cook. …… Ndio, walipika! (KWA MSISITIZO)

NB ; Tunapokanusha sentensi kwa kutumia ‘did not’/ ‘didn’t’ , huwa hatutumii kitendo kikiwa katika umbo la wakati uliopita maana ile ‘did’ inakuwa imeshawakilisha wakati uliopita (‘li’ ambayo kinume chake ni ‘haku’) kwa hivyo hatuhitaji wakati uliopita kwa mara ya pili. Tukitumia umbo la wakati uliopita pia kwa kuuliza swali lililoanzia na ‘did’ pia tunakuwa tumeweka ‘li’ mbili katika sentensi, jambo ambalo sio sahihi.

Mifano ; 1. She didn’t went yesterday. ( Badala ya ‘She didn’t go yesterday.’)
Haku lienda jana. ( Badala ya ‘Hakuenda jana.’)no

ViAu; 2. Did she went yesterday?
( Badala ya ‘Did she go yesterday?’)

- Je, yeye ali lienda jana?
( Badala ya ‘Je, yeye alienda jana?)
 
Back
Top Bottom