Itawezekana Rais kukatwa kodi ya kiinua mgongo bila kubadili kifungu cha 43(2) cha Katiba?

tatizo hapa nahisi unachanganya "lini analipwa" na "mchakato wa kumlipa" ni vitu viwili tofauti,kuanza kwa mchakato mapema hakumaanishi ndio ameanza kulipwa mapema hapana,tunaangalia lini atastaafu........
Unachosema ni sawa kabisa na hata mimi nimekiona lakini ni bora zaidi kifungu hiki cha 43(2) kingeweka wazi jambo hili kuondoa kile kinachoweza kuitwa oversight katika sheria.

Yaani pamoja na kubadili sheria kuruhusu Raisi kukatwa kodi,kifungu hiki cha katiba ambacho kiliandikwa wakati kiinua mgongo cha raisi hakikatwi kodi ingekuwa vizuri zaidi kama kingebadilishwa kwa kuongeze shariti hili jipya baada ya uamuzi huu wa bunge.
 
"Mshahara na malipo mengine yote ya Raisi havitapunguzwa wakati Raisi anapokuwa bado ameshika madaraka yake kwa mujibu wa Katiba hii." Kiinua mgongo kinalipwa wakati Raisi ameisha staafu. Hivyo kifungu hicho hakitahusika wakati huo.
Tujaribu kuwaza haya...

1. Chukulia, katika kipindi cha pili cha uraisi baada ya yeye kumaliza muda wake, kashinda mtu mwingine, vipi wakiamua kumlipa kile kipindi kabla mteule hajaapishwa..??

2. Halafu inakuwaje kama kipindi cha pili akashinda yeye? Kiinua mgongo cha kipindi cha kwanza hawezi kukichukuwa wakati yuko madarakani kwa kipindi cha pili..??

3. Kwani nini hayo ya kukatwa kodi KIINUA MGONGO cha hao waliokuwa wamesamehewa kwa mujibu wa katiba, kusemwe tu kwa maneno..?? HAYO MANENO SIYO KUVUNJA KATIBA..??
 
ndomana nikauliza ni lini walipinga bajeti ya serikali yao??miaka yote wabunge wanakosoa na bado inapita kama kawaida labda uniambie miaka yote walikuwa wanapitisha pia kishingo upande??au this time,wamezidisha kunyonga shingo zao maana kiinua mgongo chao kitaenda mrama??
 

Tamko la raisi ni sharia tosha, soma vifungu vyote katika katiba.
 
Jitahidi uwe mwelewa
Hapa kinachozungumzwa ni kiinua mgongo ambacho kimsingi hulipwa baada ya mtu kuwa ameshatoka kwenye ajira yake
Acha kukurupuka kijana
 
Ingekuwa ni bora kama Katiba ikataamka moja kwa moja kuwa Raisi atakatwa kodi ya kiinua mgongo maana mchakato wa kumlipa Raisi kiinua mgongo sidhani kama huwa unaanza baada ya Raisi kustaafu.
Halafu hata kama huo mchakato utaanza kabla au baada, KIBAYA NI KUWA Lini mchakato unaanza, LIMEACHWA KWENYE UTASHI WA MTU MMOJA AU WATU FULANI, hawabanwi na katiba... wanaweza wakaanza leo na leo hii hela zikafika kwenye akaunti ya muhusika... UKIZINGATIA RAISI NI BOSI WA WOTE
 
swali lako la kwanza kasome sheria upya,hakuna kitu kinaitwa wakiamua,sheria inasema mpaka astaafu,na anastaafu rais mwingine akishaapishwa
swali la pili waulize wabunge wako,wanachukuaga kiinua mgongo wakimaliza kipindi cha kwanza cha ubunge hata kama wamechaguliwa tena kuendelea??
swali la tatu,hayo maneno ndo amendements zenyewe katika katiba
 
Ndugu wana jf tuwe wazalendo tunapo jadili suala la msingi kama hili na tuache kujadili kwa kutetea maslahi ya chama badala ya kuangalia maslahi ya taifa kwa ujumla
 
Duh kwa hiyo tamko la Raisi kutokulipa kodi ni takwa la Kikatiba.
Basi bila kubadiri katiba tamko la Waziri ni tamko la kisiasa tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…