Itel kuongeza idadi ya watumiaji wa smartphone Tanzania

Itel kuongeza idadi ya watumiaji wa smartphone Tanzania

Joined
Mar 5, 2020
Posts
18
Reaction score
28
Hivi karibuni serikali kupitia wizara ya Habari Mawasiliano na Teknolojia ilitoa takwimu za watumiaji wa simu janja/smarthpone na kusema ni 27% tu ya Watanzania wanaotumia smartphone.

Pengine mtu anaweza kujiuliza kwanini kiwango hiki ni kidogo sana ukilinganisha na idadi ya watu waliopo. Sababu zipo nyingi za idadi hiyo kuwa ndogo ambazo ni pamoja na watu kutokuwa na elimu ya kutosha kuhusu matumizi ya simu hizi za kisasa, wengine walishaambiwa kuwa simu hizi zina gharama kubwa hata baada ya kuzinunua kwa maana ya huduma za internet lakini kubwa zaidi ni kuhusu bajeti ya kununua simu hizi dukani hasa ukilinganisha na vipato vya wengi ni vya chini.

Sasa kwanini tunasema itel itaongeza idadi ya watumiaji wa smartphone Tanzania? Katika sababu zote zilizotolewa itel ina uwezo nazo.

Kuhusu suala la bajeti ya kununulia smartphone, itel imekuwa rafiki wa wote ndio maana kuna matoleo ya A'Series kwa wasiofahamu kwanini ni A, ni kwamba A inasimama badala ya Android, sasa A' series slogan yake ni "Android For Everyone" Yaani Android kwa wote. Hapa utapata smartphone kuanzia Sh. 85,000 mpaka 150,000/= tu. Hapo ni bajeti iliyozingatia uchumi wa kila mwenye umri wa kutumia Smartphone huku simu zikiwa na kila kitu kinachohitajika. Matoleo haya ni pamoja na A56, A14Plus, A25Pro pamoja na toleo la hivi karibuni la A58.

1.png

itel A58

Kwa upande mwingine kuhusu gharama za internet ni kwamba itel kwa kushirikiana na google ina bidhaa za google maalumu kwa kutotumia data kubwa mtandaoni, bidhaa hizo zimekuwa pre-installed ambazo ni pamoja na Google Go, You Tube Go, Android Go na nyinginezo. Hizi ni maalumu kwa kubana matumizi ya data za internet hivyo mtumiaji ataweza kumudu gharama za bando huku akila raha mtandaoni.

Kama una maswali, maoni ama ushauri karibu kwenye jukwaa hili ama tembelea kurasa zetu za Instagram, Facebook ama twitter kwa jina la itel Tanzania.
 
Hii mipango inatekelezwa lini?
Maana Kuna Hawa halotel walikuja na sera ya kutoa internet bure kwa taasisi za serikali pamoja na kuuza simu kwa bei nafuu lkn yooote zzzzzzzz
 
Hii mipango inatekelezwa lini?
Maana Kuna Hawa halotel walikuja na sera ya kutoa internet bure kwa taasisi za serikali pamoja na kuuza simu kwa bei nafuu lkn yooote zzzzzzzz
Tayari imeshaanza kutekelezwa ukihitaji tujuze.
 
Back
Top Bottom