SUBMAC
Member
- Apr 12, 2024
- 11
- 11
Habarini!
Kama tujuavyo, Rais Samia yumo nchini Korea ya Kusini akiendelea na ziara take ya kikazi. Suala moja nimeshindwa kuling’amua kiasi cha kuhitaji msaada wa ufafanuzi na kueleweshwa kuhusu protokali ya bendera ya nchi pindi Rais wetu awapo ziarani katika nchi nyingine.
Nimekuwa nikiona marais wageni wanaozuru Tanzania kikazi, wakisimama mbele ya bendera za nchi zao katika matukio rasmi ya mazungumzo, picha hata press briefings.
Kwavile Rais wetu ndiye mwenyeji, atakuwa na bendera ya Rais (kuonesha mamlaka yake) pamoja na bendera ya taifa (kwa uwakilishi wa nchi), huku Rais Mgeni akiwa na bendera ya nchi yake (state, not presidential) na mara kadhaa nimeona ikiongezeka na bendera yetu ya Taifa, sambamba na bandera ya taifa ngeni husika katika upande wa Rais Mgeni aliyetembelea nchini, mfano ni ziara ya Makamu wa Rais wa Marekani, Kamala Harris, nchini Tanzania.
View attachment 3006423
Nilochokiona nchini Korea ya Kusini ni tofauti kidogo. Bendera ya nchi hiyo imewekwa upande wa Rais wetu (Tanzania) huku bendera yetu ikikaa upande wa Rais wa Korea ya Kusini. Ndivyo ilivyo pia katika tete-a-tete na bilateral talks.
Naomba ufafanuzi na kuelimishwa juu ya hili.
Nawasilisha!