ITIKAFU ni nini?

ITIKAFU ni nini?

Status
Not open for further replies.
Mbona ajafa sasa, kwa maana hiyo we dont need to worry what such nonsensical ritual entails, huyu Mr.President na hizi irrational thinking zake wakati mwengine, no wonder ghorofa lina anguka we unasema kazi ya mungu how about uzembe?

By the way muhusika huko angani kama unapita kuchunguliaga JF im only joking, we una nguvu lakini si hawa masheikh uchwara wanaotaka kukufanyia kazi yako ya kuchukua roho ya mwanadamu, ajabu yenyewe Mr President kaogopa ama nayeye mshirikina.
pigia mstari hilo suala,mpaka amelizungumzia ina maana iko hivyo
 
Zile ni dua watu wanasoma. Ni kama Novena katika Kanisa Katoliki,ambayo ni sala ya baraka,inasomwa kila siku,kwa siku tisa mfululizo.
Kwa hiyo kama watu wanakutana kila jiono,wanakuomnbea mabaya,halafu wanarudia tena kesho,wanaendelea wiki nzima,wanaendelea wiki mbili,wanaendela zaidi ya wiki mbili,huo ndio ushirikina,utabakia kumtumaini Mungu kwamba hayo mambo hayana nguvu katika kuathiri maisha yako.
sasa mkuu wakifanya watu wa kanzu mnasema wanaabudu majini wakifanya wavaa magauni haizumzwi sana hili limekaaje
 
WAKRISTU nao wana yao inayoitwa NOVENA ya siku SABA
Hakuna novena ya kumuombea mtu afe au adhurike! Waisilamu hapa hawajasingiziwa, kwani ametamka mwisilamu mwenzao, tena kiongozi wa nchi kuwa katika uisilamu kuna kuombeana kufa, na kwamba yeye ameombewa afe katika misikiti mitatu tofauti. Angeyasema hayo rais mkristu nadhani ijumaa hii kungekuwepo maandamano kuelekea Ikulu
 
.JK amechanganya mambo, kuna kitu huitwa 'MUBAHALA'. Mubahala ndio hutumika rasmi kuamua NGUVU ya Muumba ichukue hatua. Tena Mubahala huwa ni wazi ambapo mshitaki na mshitakiwa wote hupeana taarifa rasmi (kubainisha muongo na mkweli), (apokelewaye dua na asiyepokelewa dua). Mubahala hutoa idadi ya siku maalum hukumu ya Muumba kuwa imetolewa.

Asante sana kwa hii ilmu......huu MUBAHALLAH ni njia muafaka kabisa katika kutatua matatizo kati ya wanadamu
 
non sense,nadhani ameiabisha dini yake,waislam wanazidi kutia aibu.
 
Sina haja ya kumensheni, tuliona dunia nzima bwana...hata hapa kwetu walikutana waislamu viwanja vya mnazi mmoja...kama unataka tarehe siku mwezi....hio sasa shauri yako na ubishi wako wa kwenye mihadhara ya kina Magezi...!!
Ha ha ha kuliwahi kufanyika ITIKAFU katika viwanja vya mnazi mmoja!

Btw nilikuwa nikizungumzia dua ya QUNUUT.
 
1994 baada ya kadhia ya Mabucha ya Nguruwe Mrema alisomewa juilize alipo, Ali Ameir Mohamed alisomewa baada ya Mauaji ya Mwembechai hivi sasa yupo kama hayupo, Askof Lwambano baada ya kusomewa kafumaniwa kafukuzwa Kanisani Mburahati, Chenge baada ya kupitisha sheria ya Ugaidi akasomewa muda mfupi baadae likafumuka la vijisent akaporomoka kutoka kwenye uwaziri, Sofia kawawa kwa watu wazima wanaijua kadhia ya 1988 habari yake muulize Vita kawawa, hii kitu ni maombi ya kumshtakia Mwnz mungu kama huna hatia hakuna neno ila kama kwenye Dhulma ya Waislam wakapatikana kweli wachamungu lazima upate khabar yake, Kama jakaya anadhulumu waislam kweli ajiandae!

japokuwa sifahamu mambo ya itikafu na mengine yanayo fanana na hayo ila nilitaka kusahihisha tu kuwa father Camilius Lwambano hakuwa askofu ni hilo to basi
 
mimi nadhani kama hilo linawezekana kwanini wasiwasomee majambazi wote wanaolisumbua jiji kumbe kuna wataalamu wa hiyo kitu
 
Ha ha ha kuliwahi kufanyika ITIKAFU katika viwanja vya mnazi mmoja!

Btw nilikuwa nikizungumzia dua ya QUNUUT.

Ila mkuu hayo mambo ya kumwombea mtu mabaya hadi yampate...sio ushirikina kweli?...Tuthibitishea kuwa majibu yanatoka kwa Mungu wa kweli?
 
Na suleyman Rushdie si alisomewa hiyo kitu?baada ya satanic verses lakini hadi leo anakula bata states,mambo ya kutishana tu,kiboko yenu ni yule mtoto wa mbagala tu.

Anakula bata? hivi sasa ni kipovu anaishi katika jumba la malkia fuatilia habari ujue
 
Kama ITIKAFU ingekua inafanya kazi ingeanza na Mafisadi kwanza. Acheni kumtisha Rais wetu after all anaongoza Taifa lisilo na dini "Circular State".

Rais wetu usiogope sisi raia na wananchi wako tunakuombea Kinga kutoka kwa Mungu aliyeumba hata hao wasomi wa Itikafu usiku na mchana.
 
Anakula bata? hivi sasa ni kipovu anaishi katika jumba la malkia fuatilia habari ujue

Na yule Rais mstaafu wa Zanzibar aliyepoteza uoni mlimsomea pia? Acheni hizo watu wanapata matatizo kwa amri ya Mungu na umri wao kufika hata wewe usijekuta leo unalala mzima kesho unaamka vingine, acheni kutishana sote ni wapitaji hakuna mkaaji milele.
 
Ila mkuu hayo mambo ya kumwombea mtu mabaya hadi yampate...sio ushirikina kweli?...Tuthibitishea kuwa majibu yanatoka kwa Mungu wa kweli?
Sio ushirikina.

Ama kuhusu kumuombea mtu mabaya hili linataka upambanuzi:
Mtume salalahu alayhi wasallam anasema (tafsiri): Dua ya mja hukubaliwa maadamu katika dua ile haombi mambo ya madhambi na kuvunja undugu..." sahihi Bukhari

Vilevile mwenye kudhulumiwa anaruhusiwa kuomba dua dhidi ya aliyemdhulumu.

...funguka zaidi katika swali lako.
 
Itikafu ni "kujifunga" ....kilugha

Ama kisheria, itikafu ni kujifunga katika sala na ibada nyengine katika kumuomba Muumba

Ombi hilo linaweza kuomba ubarikiwe afya, mji upate mvua, na mengineyo

Kwahiyo hata Mukulu haijui imani yake.
Maajabu. Mbona hujamsaida?!
 
Sio ushirikina.

Ama kuhusu kumuombea mtu mabaya hili linataka upambanuzi:
Mtume salalahu alayhi wasallam anasema (tafsiri): Dua ya mja hukubaliwa maadamu katika dua ile haombi mambo ya madhambi na kuvunja undugu..." sahihi Bukhari

Vilevile mwenye kudhulumiwa anaruhusiwa kuomba dua dhidi ya aliyemdhulumu.

...funguka zaidi katika swali lako.

Kwahiyo Jakaya, rais wetu amewakosea nini hao waliotaka kum restisha inpisi?
 
Kwahiyo Jakaya, rais wetu amewakosea nini hao waliotaka kum restisha inpisi?
Kwa kweli mimi binafsi sina taarifa zozote za watu kukaa Itikafu na kumuombea JK afe.

Itikafu ni ibada inayofanyika siku 10 za mwisho wa mwezi wa Ramadhan kama ulivyofahamisha huko nyuma.
 
Itikafu=ITIQAF.Neno hilo ni lakabu ya kiarabu. Itiqaf, ni ile hali ukaayo mahsusi kumuomba na kumlilia Mwenyezi Mungu juu ya yote yanayokusibu au kuomba msaada. Mara nyingi Itiqaf hufanyika katika zile siku 10 za mwisho wa mfungo wa mwezi wa Ramadhani. Ambapo wachamungu wa kweli hukaa misikitini pasipo kujihusisha na masuala mengine yeyote ya kimaisha au kidunia wala kuongea na waaminio waingiao kusali zaidi ya 'Assalaam alaikhum' pekee. Kwamba waaminio wanaokaa Itiqaf basi muda wao wooote wa hizo siku 10 hutumika katika ibada tu, yaani kuongea na Mwenyezi Mungu tu. Mwisho huwa ni mwezi unapoandama na kuthibitishwa kuwa siku inayofuata ni Eid.JK amechanganya mambo, kuna kitu huitwa 'MUBAHALA'. Mubahala ndio hutumika rasmi kuamua NGUVU ya Muumba ichukue hatua. Tena Mubahala huwa ni wazi ambapo mshitaki na mshitakiwa wote hupeana taarifa rasmi (kubainisha muongo na mkweli), (apokelewaye dua na asiyepokelewa dua). Mubahala hutoa idadi ya siku maalum hukumu ya Muumba kuwa imetolewa.JK kachanganya kati ya 'itiqaf' na 'mubahala', anapaswa aingiliapo masuala ya dini awahusishe wanazuoni wa kiislam kumpatia tafsiri yenye tafsida nzuri kwa umma.Rock City.

ni tofauti na albadiri?
 
Sio ushirikina.

Ama kuhusu kumuombea mtu mabaya hili linataka upambanuzi:
Mtume salalahu alayhi wasallam anasema (tafsiri): Dua ya mja hukubaliwa maadamu katika dua ile haombi mambo ya madhambi na kuvunja undugu..." sahihi Bukhari

Vilevile mwenye kudhulumiwa anaruhusiwa kuomba dua dhidi ya aliyemdhulumu.

...funguka zaidi katika swali lako.

Japo huyo uliemnukuu mie simwamini kabisa!...
Ila naomba niuleza swali, kumwombea mtu kifo..sio kati ya haya? (ile haombi mambo ya madhambi na kuvunja undugu)
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom