KwetuKwanza
Member
- Mar 13, 2023
- 82
- 150
Juzi watumishi Kada ya ualimu na Afya katika Wilaya za Rombo na Sikonge walilalamika kutolipwa stahiki zao ambazo ni fedha za kujikimu.
Hivyo hivyo kadhia hiyo imetukumba sisi watumishi katika Wilaya ya Itilima Mkoani Simiyu, ambao ni wapya, tunalalamika kutolipwa fedha zetu toka mwezi Juni, 2023 walipiajiriwa.
Uongozi wa Halmashauri, Umeshindwa kutulipa stahiki zetu, tumekuwa tukiulizia kwa wahusika na kuhaidiwa kuwa watapigia simu malipo yakiwa tayari.
Baada ya kuripoti Halmashauri, tuliambiwa twende Moja kwa Moja vituo vya kazi, na malipo ya fedha ya kujikimu tutalipwa baadaye, lakini toka mwezi Juni, 2023 hatujalipwa, na hakuna Majibu yeyote yanayoashiria kuwa tutalipwa
Mpaka sasa hakuna mwekekeo wa uhakika unaonyesha kama tutalipwa stahiki zetu, au ndiyo tumedhulimiwa, walisema turipoti kwanza kwenye vituo vyetu, Kisha malipo yatakuja ndani ya muda mfupi, lakini mpaka leo hakuna mwelekeo wa hayo malipo.
Pia soma: Watumishi Ajira Mpya (Sikonge na Rombo) hatujalipwa Fedha za Kujikimu, tunapigwa danadana
Waziri Mchengerwa aagiza Fedha za Kujikimu za Ajira Mpya zilipwe kabla 30 Oktoba, 2023