Robert Heriel Mtibeli
Platinum Member
- Mar 24, 2018
- 40,153
- 93,069
ITOLEWE AMRI, UCHAFU KUKUTWA KWENYE ENEO LAKO, FAINI ELFU 50.
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli
Hii nchi unaweza ukadhani haina viongozi. Unaweza ukadhani haina Wasomi.
Unaweza ukadhani haina Watu wazima. Unaweza ukadhani haina wanawake wanaosifika kwa usafi.
Kuna mambo ukiyafikiria yanaweza kukuacha mdomo wazi. Kukusikitisha kabisa.
Leo nitazungumzia suala la usafi wa mazingira. Aiseeh! Ukisema Watanzania ni wachafu ninaweza kukamatwa hapa na kufichwa kwanza nifundishwe adabu.
Lakini vipi, nitakuwa nasema uongo?
Oooh! MTIBELI unatutukana, Mtibeli unatukana mpaka wazazi wako ujue. Hapana! Hatuwezi kuacha kusema ukweli hata kama unatugusa sisi wenyewe. Ili tubadilike lazima ukweli usemwe waziwazi. Lakini hatua stahiki zichukuliwe.
Ukitaka ujue Hii nchi inawatu wachafu.
Pita barabarani huko.
Utakuta uchafu kila kona. Makaratasi, takataka zimetupwa hovyohovyo.
Mji unanuka hujapata kuona.
Ajabu sio kunuka. Ajabu ni watu wake. Yaani ni kama hakuna kinachoendelea. Kama hawasikii hizo harufu.
Kuna haja ya kuitisha kampeni kubwa ya usafi wa mazingira. Kubwa sana.
Kisha sheria za mazingira zifuatiliwe hata kwa kiwango cha nusu ufuatiliaji.
Huwezi fikiria vitu vya maana kama unakaa sehemu chafu.
Mimi nimefanya chunguzi zangu, ila sio rasmi. Nawe unaweza kufuatilia;
Angalia mtu anayetoa maneno machafu mitandaoni au mitaani alafu kaangalie anapoishi au eneo analoishi.
Nilibaini kuwa watu wenye midomo michafu, matusi wengi wao wanatoka pia Maeneo yenye uchafu mwingi. Ukibisha nitakuletea ushahidi ukitaka.
Ndio maana humu mitandaoni matusi yamejaa kila kona. Ukienda huku matusi. Ukirudi huku takataka, ukirudi huku mavimavi. Uchafu kila kona kama tupo vilabuni.
Kadiri mazingira yanavyokuwa safi ndivyo akili ya mtu huwa safi na tulivu. Hata mazungumzo huwa masafi. Sio rahisi. Nakuambia sio rahisi mazingira masafi usikie lugha chafu sio rahisi. Hilo nimefuatilia kwa yakini.
Katika Saikolojia, usafi unachangia kwa sehemu kubwa mtu kufikiri na kusema kiungwana.
Sasa basi, msije sema Mtibeli ninawatukana, msije mkataka kunirushia ngumi. Au kunificha. Kwanza tutafichana. Pili siwaogopi watu wachafu. Tatu tunatakiwa kubadilika.
Haiwezekani mtoto aone kawaida kuona mauchafu huko barabarani.
Watoto wanatakiwa watuone kama wazazi na viongozi tunaojitambua.
Unakuta jitu linakula chungwa au ndizi barabarani. Sio jambo baya. Ila ubaya unakuja pale ambapo hana pakutupia Ganda au takataka yake. Anatupa barabarani. Huo ni uchafu. Hizo tabia za kimamavi sio nzuri.
Inatakiwa mtu akutaka kutupa takataka anasikia aibu au anapata hofu kwamba nikikamatwa hapa kazi ninayo.
Mimi sio mtaalamu wa mazingira. Na hiyo hainizuii kusema lolote kuhusu usafi wa mazingira.
Nini tufanye?
1. Tamko la Faini ya 50k kwa nyumba itakayokutwa uchafu.
Vibao vinatakiwa vijae mitaani usitupe taka hapa.
2. Anayetupa taka faini atoe 100k
Wewe ukiona mtu anatupa takataka popote Dai 100k, akikataa peleka serikali za mitaa Kisha polisi.
3. Ipigwe marufuku kuchoma choma vitu. Mitaani.
Kama mtu anataka kuchoma aombe kibali serikali za mitaa.
Anayekaidi iwekwe faini.
4. Sheria za sauti zifuatiliwe na kusimamiwa. Kama ni muziki wa kibinafsi yaani nyumbani kwa mtu itangazwe wazi unatakiwa uwe chini ya volume kiasi fulani.
Muziki wa Bar zilizo mtaani volume ziwe kiasi kadhaa.
Kwenye nyumba za ibada volume kiasi kadhaa.
5. Kupikapika sijui nyama choma, mama ntilie watumie dhana za kisasa au teknolojia isiyoleta moshi mitaani.
Kuna Majiko yale ya kienyeji ambayo ile sehemu ya kutolea moshi inapeleka Bomba juu moshi unatokea juu ya anga huko na sio kuingia mitaani.
6. Ipigwe marufuku bodaboda kupiga mamiziki. Faini iwekwe 50k.
7. Wajasiriamali wanaotumia vipaza sauti kwa kutangaza sumu ya panya, dawa mba,n.k wapewe Vibali maalum vya kupiga kelele hizo. Wanaweza kulipia kwa mwaka 20k
8. Wacheza ngoma, au sherehe kama watafanya sherehe zao nje waombe kibali serikali za mtaa kwaajili ya kupiga kelele na kusheherekea kwa kutumia vipaza sauti na muziki.
Sherehe ni kwako au kwangu lakini kwa wengine unawapigia kelele. Alafu unapiga kelele burebure.
Misiba ni tukio la asili halitahitaji kibali cha kulia au kupiga mayowe. Ila kama kuna kuweka muziki, maspika sijui kwaajili ya mahubiri sijui mawaidha hayo mambo sio ya asili ni anasa. Watu watapaswa waombe kibali cha kuweka muziki.
Gharama za matukio muhimu kama misiba na sherehe za harusi gharama zake zitaangaliwa lakini ni muhimu ziwepo.
Ni muhimu pia pawepo na kifungo walau cha miezi mitatu kwa wale wakaidi waliobobea. Au wanafanya kwa makusudi.
Kufikia hapo sina la ziada.
TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam