Itolewe Amri, uchafu kukutwa kwenye eneo lako, faini elfu 50

Kuna wabaya wetu watatupa uchafu barabarani kisha upepo unasukumia kwetu
 
ELFU 50 watalipa na uchafu utaendelea kuwepo. Muharobani ni kuwa kukikutwa uchafu, muhusika ahamishwe hilo eneo, asionekane. Akionekana kifungo gerezani! Uone kama uchafu utaonekana.

Rude but helpful kufanya awareness campaign ya kuzuia uchafu.

Sahihi kabisa.
Ila 50k kwa wabongo wengi ni parefu
 
Uchafu ulioenea mitaani na mijini ni indicator ya ufanyaji kazi wetu kama serikali iliyopo. Kama hata usafi unashindwa kufuatiliwa sijui mengine ni vipi

Hatari sana. Yaani kuna wajumbe, kuna wenye viti, kuna watendaji, kuna maafisa afya, lakini hakuna anayewajibika
 
Arusha siku hizi pamekuwa pachafu Sana, hakika panatisha🥵🥵
 
Tunapenda Sana kulaumu wenzetu Ila hatupendi Sana kujicriticise wenyewe.

Toka umezaliwa mkuu Hadi sasa hivi umelipa taka taka miezi mingapi? Kwanini kila kitu iwe Serikali?

Sisi mikoa yetu kaskazini most of time ni misafi, ukija Tanga Mjini, Moshi etc utakuta majiji Yana uafadhali, sio kwamba Serikali inafanya kazi vizuri Bali raia wanaji organize na wanalipa,

Hapa Tanga tulikua tunalipa 500 Tu sasa hivi imeongezeka hadi 1000, ni hela ndogo Sana Ila inaweza ikawa utofauti baina ya kila unapopita unapishana na jalala ama unapita kwenye mitaa misafi. Pia Tu sio kulipa kuna siku za kufanya usafi ambazo kila raia anahusika kusafisha maeneo yake ya nje.

Dar watu wengi hawataki hata kusikia hela ya takataka, sehemu kama kkoo ni Jambo la kawaida kukuta Rundo la taka ukicheki Aina za hizo takataka hakuna hata mmoja alielipa MTU kuja kumuondolea.

Hizo Sheria za 50K zipo siku nyingi Tu ila hazitekelezeki mpaka kila MTU either awe responsible ama alipie wengine iwe Ajira Yao kumuondolea hizo taka taka.
 

Mkuu umeongea jambo zuri sana kuhusu pesa za Taka. Ambazo nafikiri kwa maeneo mengi Dsm ni 3000 kwa nyumba na 6000 kwa wenye biashara

Wapo wanaotoa na wapo wasiotoa. Na wapo wanaotoa kwa kusuasua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…