Itolewe Amri, uchafu kukutwa kwenye eneo lako, faini elfu 50

Mkuu leo ngabu, namshangaa anatoa matusi hatari nasisi tunataka kujifunza kupitia hawa wakonge.tunabaki kushangaa.

Ndio tabia za wazee waliokuwa wahuni zamani. Kuna saa zinafyatuka. Msamehe tuu. Atakaa sawa
 
Kodi zako unazolipa zinafanya nini? Kama mfumo wa ulipaji wa sasa umeshindwa kwa nini mnaung'ngania? Si mtumie kodi zinazokusanywa? By the way tukijipanga vizuri taka ni bidhaa inawezekana kuzinunua na kuuza
 
Naunga mkono hoja, Kuna ,aujinga ,engocsana ya kiuchafu yanaendelea Huku mitaani Kwakweli.
 
Maandishi meeengi hujui SERIKALI ndio wachafu? Pita masokoni ambalo wanachukua ushuru wa taka utaelewa!
 
Kodi zako unazolipa zinafanya nini? Kama mfumo wa ulipaji wa sasa umeshindwa kwa nini mnaung'ngania? Si mtumie kodi zinazokusanywa? By the way tukijipanga vizuri taka ni bidhaa inawezekana kuzinunua na kuuza
Excuse ya wabongo hii kila siku.

Shilingi 7 Hadi 9 katika kila sh 10 inayokusanywa inalipa mishahara na madeni, haitoshi kufanya chochote sembuse kuja kusafisha kwako. Ni ujinga hata kulifikiria Hilo kwamba uzalishe takataka kwako ukatupe nje halafu mwanaume mwenzako akalipe Kodi zije zikusafishie, serious?
 
Upo sahihi. Mimi nipo kwenye nyumba ya kupanga (dsm). Gari la uchafu halipiti, nitaupeleka wapi?
 
Mwanaume gani tena? Wewe tumia akili mimi hizo taka nikizikusanya nitazipeleka wapi. Hoja yangu kama wengi hawalipi serikali ilipe halafu iweke utaratibu tofauti wa kulipa. Mfano kwenye wanywa energy drinks na kwenye pampas za watoto etc. Siyo unakaa ofisini unalipwa hela hufikirii chochote kama afisa mazingira
 
Barabara zenyewe mnazojenga mchanga haufagiliwi

Aise rwanda wako clean usafi wao kufanya siyo wa kihemuko kama malawi

Ova
 
Ukilipa kwa kampuni inayokuja kuzoa then inatosha, wewe responsibility yako kusafisha kwako na wao watachukua kuanzia hapo. Wasipofanya KAZI Yao Nyie kama mtaa ama kijiji mnatafuta mwekezaji mwengine, munamuwajibisha asiefanya KAZI yake vizuri.
 
Ukilipa kwa kampuni inayokuja kuzoa then inatosha, wewe responsibility yako kusafisha kwako na wao watachukua kuanzia hapo. Wasipofanya KAZI Yao Nyie kama mtaa ama kijiji mnatafuta mwekezaji mwengine, munamuwajibisha asiefanya KAZI yake vizuri.
Huu utaratibu wako ulishafeli. Watu wengi hawapo nyumbani pindi wakusanya kodi ya taka wanapokuja. pili wakusanyaji hawakusanyi hata wakichukua hela. Ni wajibu wa serikali kuhakikisha taka zinakuwa disposed safely (hili nimeliandikia sana humu JF). Kutoku-dispose taka safely tunahatibu udongo ambao ungetumika kwenye kilimo. Pia tunaharibu vyanzo vya maji etc, sijui kwa nini nyie watu wa serikali hamuelewi.
Sijui level yako ya understanding lakini taka mtaani si tatizo la binafsi ni tatizo letu kama nchi.

Umefuatilia compliance ya kulipa upande wa wananchi na compliance ya ukusanyaji taka upande wa serikali. Kama upo Dar mbezi stendi ya daladala lie dampo mliloweka pale nyuma ya choo linafanya nini? Na kwenye stendi ya daladala za segerea pana dampo mmeweka. Aibu tupu kwa serikali
 
Mimi nyumbani Tanga naishi pia Dar sehemu zote watu wanakusanya na mazingira ni masafi, so tatizo sio utaratibu Bali culture ya watu.

Na Nani amekuambia ukiwa haupo nyumbani basi taka hazichukuliwi, ama unafkiri hio mikoa misafi watu hawafanyi KAZI?

Ni utaratibu Tu mkijiwekea basi kila kitu kinawezekana, ukiwa huna lengo na Nia ya kukaa Eneo safi Basi excuse ni rahisi Sana kuzitoa, utalaumu watu wote Bilioni 8 Duniani kabla ya kuja kuona tatizo linaanzia kwetu wenyewe.
 
Wewe ni sehemu gani unaishi dar ambayo siyo chafu? Dar yote chafu. Taja hapa sehemu safi kwa dar
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…