Itunze ndoa yako

Itunze ndoa yako

Milionaire Mind

New Member
Joined
May 25, 2017
Posts
1
Reaction score
0
Itunze ndoa yako..

Omba msamaha ukikosa

Sema asante kwa kile utakachopewa kiwe kikubwa au kidogo.

Jali mahitaji ya mwenza wako, ya mwili na roho..

Kila mara mkumbuke hata akiwa bize, piga simu..

Penda kumbusu au kumkubatia kila ukijisikia..

Ogopa maeneno mabaya wala usiyaweke moyoni, haya huharibu tabia njema..

Mke mkaribishe mumeo kwa upendo atokapo kazini, mpokee mizigo yake, usiruhusu house girl awe ndiye wa kumpokea mumeo..

Pendelea kupika chakula ambacho wote mnakipendaa kwa namna ile ifaayo.

Usisahau zawadi hata iwe ndogo huleta kumbukumbu fulani.. Pipi nayo huamsha upya penzi.

Mtoe out mwenza wako na mfanyie surprise, hii huamsha upya mapenzi.. Out zisiishie uchumba tu.

Wakati mwingine mechi za uwanja mmoja huchosha, tembelea viwanja vingine, nenda nae hata hotel siku moja siyo mbaya..

Msifie kwa mazuri anayokufanyia. Akifanya jema usiacha kumsifu.

Mshirikishe mipango yako na kila tatizo lako, ninyi ni mwili mmoja..

Mke usipende sana uvivu, usipende sana majukumu ya msingi kumpa house girl. Hata kitanda chenu atandike yeye? Ipo siku atakilalia na usilalamike..

Usisahau kumsifia kila akipendeza, msifie kwa uzuri wake, mnunulie nguo unazoona akivaa zinaleta mshawasha...

Nyumba ni yenu hata kama ni ya kupanga kusiwe na ratiba ya mechi wala uwanja, mechi za kustukuza na uwanja wowote huwa tamu kama wote mpo tayari... Utamu wa muwa aujua mtafunaji..

Yaelewe madhaifu ya mwenza na uyabebe kifuani. Kumbuka huyo ni wako hivyo kumuelewa ni muhimu..

Kamwe usimseme mwenza akikosea ukiwa na watu, ndgg nk. Umuambie hayo baadae watu wakitoka. Linda heshima yake..

Ukitokea ugomvi, kutoelwana na kupishana kwa kauli sharti na muongee kwa upendo. Yakiwashinda subirianeni kwa siku kadhaa kabla ya kupeleka kwa watu. Watu hupoteza muelekeo, labda wataalamu wa mahusiano ndio wanaweza shauri vema..

Ukiondoka aga, omba ruhusu kufanya jambo. Kumbuka kuwa kuondoka bila kuaga na dhana ya kiburi na majivuno.. Kama utachelewa kwa sababu ya ratiba ya kazi kubadilika mwambie mapema.

Wapendeni watoto wenu zawadi mliyoipata toka kwa Mungu. Waleeni vema sio kwa kuwadekeza. Kumbuka utawacha siku moja, ulimwengu mbaya..

Pateni muda wa kukaa pamoja na kuongea juu ya maisha yenu, pata muda wa kukaa na mwenza kujadili mipango yenu.

Kila mwisho wa mwaka wekeni kikao cha bajeti ya familia. Wekeni mikakati ya mwaka ujao... Mipango madhubuti huleta maendleo..Wekeni malengo ya kila mwaka. Kila mmoja ayafanyie kazi na hakika baraka zitatiririka kwenu.

Ili kuleta maendeleo, ni vema kukawa na kikao cha familia, baba mama na watoto. Makaongea pamoja..

Mtoto akikua (akibalehe) mueleze changamoto zitakazo mkabili. Dunia imebadilika watoto wanaharibikiw kwa sababu wazazi hatusemi tukijua eti mila au atajua mwenyewe. Kumbuka akileta mjukuu na kukatisha masomo ni hasara. Kama huwezi sema tafuta mtu awaelekeze. Okoa jahazi mapema...

Baba na mama msisahau kuangalia mienendo ya wanenu. Angalia mabadiliko ya tabia zake. Ikitokea umepata taarifa ya mwanao kujihusisha na vitendo viovu basi makanye hima usimtetee.

Ndoa jukumu la wote, usimwachie mmoja jukumu la kulea watoto. Angalieni maendeleo yao kielimu na shirikianeni kuwasidia kila inapobidi.

Chunga sna marafiki waovu, huja kama malaika wakakushauri na mwisho hupoteza ndoa yako. Usiwasikilize sana, usiwe bendera kufuata upepo.

Elewa kuwa ndoa ina shida na raha, furaha na huzuni, amani na mateso. Kumbuka neno hili daima yote yatapita..

Kutafuta maisha kusifanye usahau ndoa, ukasahau kumhudumia mwenzako kwa kadri ya mahitaji ya mwili wake. Usipofanya hivyo wamkaribisha shetani

Msisahau kuomba pamoja, muabudu pamoja na kumshukuru Mungu kwa kila kitu. Muombe mkiwa na watoto wenu pamoja..

Mwisho..
Ndoa ni nzuri ukijua kuna shida na raha, wengi wanawaaza raha tu ndio maana ndoa ngumu..
Kuombeana mema ni muhimu zaidi
Love smart
Jicho lionalo mbali


King..
 

Attachments

  • FB_IMG_15187746824841746.jpg
    FB_IMG_15187746824841746.jpg
    45 KB · Views: 38
Back
Top Bottom