Uchaguzi 2020 ITV achaneni na mikutano ya upinzani mjikite kwenye mikutano ya CCM

Hismastersvoice

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2013
Posts
21,741
Reaction score
26,735
Leo kwenye taarifa ya habari mmeonesha mkutano wa CHADEMA kwa muda usiozidi dakika moja! Mlitumia zaidi ya dakika tano kwa kuonesha mikakati ya Polepole na kumsaidia kuweka picha za mikutano iliyopita hapo yeye si mgombea mkiwaacha wapinzani waliofanya mikutano leo!

Pia mmeitengenezea baraza la wazee wa CCM taarifa kwenye habari za biashara kwa kigezo cha biashara wakati hakukua na biashara yoyote iliyofanyika!
 
ITV hamuipendi, TBC mnaponda sijui mnataka nini. Tafuteni akina Spencer Lamek wawatangazie mafuriko feki mfurahi
 
Ccm leo hawakuwa na kampeni ndio maana habari ya 1 ikawa ya chadema! Kwa hiyo chadema ikionyeshwa nyie ccm mnaumia sana!
 
Leo kwenye taarifa ya habari mmeonesha mkutano wa Chadema kwa muda usiozidi dakika moja! Mlitumia zaidi ya dakika tano kwa kuonesha mikakati ya Polepole na kumsaidia kuweka picha za mikutano iliyopita hapo yeye si mgombea mkiwaacha wapinzani waliofanya mikutano leo! Pia mmeitengenezea baraza la wazee wa CCM taarifa kwenye habari za biashara kwa kigezo cha biashara wakati hakukua na biashara yoyote iliyofanyika!

Hivi huwa mkisema uhuru haki na maendeleo huwa mna maanisha nini ikiwa amuwezi kuvumilia wengine? Hivi mbona ninyi ni maditeta sana?
 
Akili yako imeganda kwenye Chadema tu, sijui tutajadiliana nini wakati bandiko linaelezea vyama vyote vya siasa vinavyofanya mikutano.
 
Tatizo Chadema mnatumia asilimia 95% ya mikutano yetu kutoa lugha za fedheha, kuhamasisha vurugu, kutoa vitisho na kuwananga vyombo vya habari. Kwa maana hiyo vyombo hivi vya habari vinakosa mtiririko mnzuri wa kuripoti habari zenu kwa kufuata sheria na maadili. Badilikeni aiseee
 
Leo kwenye taarifa ya habari mmeonesha mkutano wa Chadema kwa muda usiozidi dakika moja! Mlitumia zaidi ya dakika tano kwa kuonesha mikakati ya Polepole na kumsaidia kuweka picha za mikutano iliyopita hapo yeye si mgombea mkiwaacha wapinzani waliofanya mikutano leo! Pia mmeitengenezea baraza la wazee wa CCM taarifa kwenye habari za biashara kwa kigezo cha biashara wakati hakukua na biashara yoyote iliyofanyika!
VYOMBO VYA HABARI TZ VIMEVUNJWA UTI WA MGONGO
 
...
Pia mmeitengenezea baraza la wazee wa CCM taarifa kwenye habari za biashara kwa kigezo cha biashara wakati hakukua na biashara yoyote iliyofanyika!
Hicho kipengele ☝️ sina mbavu aseee...

But kila mtu ana hofu na maisha yake, nadhani tunafaham kwa sasa hali tunayoishi so tusiwalaumu maana ndipo tulipo.
 
Hiyo inaitwa mtumikie Kafir upate mradi wako.
 
Awamu hii unafiki ndiyo umetamalaki. Vyombo vya habari karibia vyote vimeamua kuweka weledi wa kazi zao pembeni, na kuamua kuisujudia ccm na mungu mtu wao.
 
ITV hamuipendi, TBC mnaponda sijui mnataka nini. Tafuteni akina Spencer Lamek wawatangazie mafuriko feki mfurahi
Ma-ccm Mungu Anawaona Kutuambia Kuwa Mgombea Wenu Ni Mpole na Msikivu Na Mnyenyekevu. Mmetukosea Sana Sisi WananChi Hasa Wabukoba na Mtwara.

Kwa kweli sisi wananchi tunaojitambua Tumehuzunishwa Sana kwa Slow slow kuudanganya Uuma!! Eti! Meko ni mpole na Msikivu ,kama hizo sifa ni za kweli basi Asingetukashifu sisi WanaNchi Wa BUKOBA Pindi tulipo Patwa na Majanga

Badala yake Meko anatuambia SERIKARI yake haikureta tetemeko.
 
Leo kwenye taarifa ya habari mmeonesha mkutano wa CHADEMA kwa muda usiozidi dakika moja! Mlitumia zaidi ya dakika tano kwa kuonesha mikakati ya Polepole na kumsaidia kuweka picha za mikutano iliyopita hapo yeye si mgombea mkiwaacha wapinzani waliofanya mikutano leo!

Pia mmeitengenezea baraza la wazee wa CCM taarifa kwenye habari za biashara kwa kigezo cha biashara wakati hakukua na biashara yoyote iliyofanyika!
Anzisheni tv yenu,kwani unawalipa wewe mishahara?
mmeingia kwenye kampeni kama mmestukizwa,hamjajipanga,uhusiano mbivu na media,pesa hamna matokeo yake ndio hayo kuhesabiana dakika utadhani unafanya uhakiki wa malipo ya matangazo ya biashara yaliokwenda hewani
 
Leo kwenye taarifa ya habari mmeonesha mkutano wa CHADEMA kwa muda usiozidi dakika moja! Mlitumia zaidi ya dakika tano kwa kuonesha mikakati ya Polepole na kumsaidia kuweka picha za mikutano iliyopita hapo yeye si mgombea mkiwaacha wapinzani waliofanya mikutano leo!

Pia mmeitengenezea baraza la wazee wa CCM taarifa kwenye habari za biashara kwa kigezo cha biashara wakati hakukua na biashara yoyote iliyofanyika!

Naona mwandishi umeenda mbali sana.
Kwani kwenye taarifa ya habari lazima taarifa zote ziwe na urefu na muda unaolingana?
Embu acheni kutafuta visingizio visivyo na Msingi, Fanyeni kampeni
 
Back
Top Bottom