ITV ilipofunguliwa mwaka 1994

Aisee umetisha
 
Enzi hizo kuna kipindi radio one kinaitwa the heat sikosei, utasikia bongo fleva zote kipindi hicho Mr 2 ndio anatoka na nyimbo zake za Yamenikuta, Utaitwaje tozi shule kama huwezi imba mistari ya sugu? Hahahhaa
Kuna ile nani zaidi, Jumapili hapo, Alipambanishwa Buju Banto na Shaba Ranks Asee kete zote za moto pambano likawa droo ikabidi lirudiwe tena Siku nyingine Mnaikumbuka hii?
Radio station za siku hzi ukifungulia stori tuuu za watangazaji hazina mvuto tena.
 
Kulikuwepo pia kipindi kizuri sana cha CAPTAIN kilichokuwa kinaitwa BEYOND 2000. RENAGADE pia ya akina Rhino Ranks na Richmond Branscombe! Usisahau na VITIMBI kutoka KBC ambayo nayo pia ilikuwa inarushwa kupitia ITV
 
Acapulco bay na mdada Rachel Kama sikosei..kitambo Sana aisee
 
Seki bwana yupo wapi?

Kile kipindi chake cha mtaani mara kala miwa ya barabarani, mara kahoji watu chanzo cha jina la mtaa wa KAWE kumbe ni - Cow Way

Mara kahoji madeni wakaleee wa Jangwani..

Nipo Kijijini kwa mwenyekiti wa kijiji ndo mwenye Tv nasema moyoni huko Dsm ni Mbingu nyingine sijui kama nitakuja kufika [emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]


Wapi alipo SEKI wa chanel 5
Dr. Roy Maganga wa R.F.A
Mtoto wa Mama Sabuni wa R.F.A
 
Juzi nimekereka nimetune Wasafi F.M barabarani nasikia Juma Lokole kama sikosei anaeleza kwamba ile haki ya kitunguu ukikata kinakutoa machozi wale ni bacteria fulani ambao naturaly wako katika vitunguu!


Nilijikuta nataman nipewe sheria niende nimukwapue redion akae mtaani aache kupotosha kizazi, wakisema hata wasome basic education upate uelewa wa mambo wanakunja uso.
 
Umeisahau Rino Lenzi mkuu, ile jingle yake wakati tamthlia inaanza inapigwa mpaka kesho Radio One
Baba yangu aliniita hili jina Rino Lenzi.
Alikuaga ni mpenzi wa movies sana,
Kwa sasa ni marehemu , amefariki 09 / 01 mwaka huu

Unaweza ukanijuza mengi kuhusiana na hili jina la tamthilia lakini sipati info zake kwenye Google
 
Mpaka leo nikitaka kutupia jicho channel za ndan upande wa habari ni itv 😃
Wakaja na itv 2 channel 5 badae ikawa eatv
Mimi nimeikuta channel 5.
Enzi hizo tunavizia ngoma kali, then tunaicopy kwenye ile mitofali.
Na ukichelewa kusyopisha itarecord hadi matangazo halafu wimbo uishe vibaya.
Kwahiyo mnakua attention kichizi, wimbo ukiisha tu chap mnaistopisha kurecord.

Ile mitofali tulikua tunachagua zile ambazo mzee anapenda na sisi hatupendi, zile nyimbo za kina defao, pepe kale, mbutalikasu and the likes.

Channel 5 ndo lilikua ting'a la vijana, huku RFA kila asubuhi ni lazima nisikilize.
Aisee namiss sana kipindi kile, ndo kipindi nilikua nina furaha ya kweli sio saivi nafake hadi furaha kudadadeki.
 
Mimi naikumbuka Panasonic top dome, nilinunua laki tatu na sitini mwaka ' 93 nilikuwa naangalia KBC kenya, itv ilikuja baadae, na kupata itv ilibidi ufunge kitu kinaitwa crystal!

Sent from my SM-T285 using JamiiForums mobile app
Kila Nchi ilikuwa na Frequency tufauti ya Sauti. Tanzania ni 6.0 MHz. So TV nyingi japo zilikuwa na system ya PAL sauti zilikuwa azina 6MHz so ilikuwa either uibadike cystal ya 6.0MHz au huiweke juu ya iliyokuja na TV. Henzi hizo spear korofi ya TV ilikuwa fly back transformer (FBT) na Duka kubwa la spear lilikuwa nyuma ya Jengo la Ushirika mnazi mmoja jamaa anaitwa Rushna. Tulipiga sana hela those days- na jamaa angu kuna mitaa alimwelewa Binti ikawa kila siku anatuaga workshop eti anaenda rekebisha Antenna imekaa Vibaya😂 kwenye nyumba hiyo hiyo kila siku.Si akamtia mimba Binti ya Mwenye Nyumba ! Mpaka Leo Tayari wana wajukuu- jamaa aliozwa ndoa ya Mkeka
 

Attachments

  • 6C6BEE9D-711A-43DA-9F41-CBECCE353F7D.jpeg
    6.6 KB · Views: 16
  • 7538B6B7-D8E8-4AB6-A319-8462BAA66C63.jpeg
    12.7 KB · Views: 20
Baba yangu aliniita hili jina Rino Lenzi.
Alikuaga ni mpenzi wa movies sana,
Kwa sasa ni marehemu , amefariki 09 / 01 mwaka huu

Unaweza ukanijuza mengi kuhusiana na hili jina la tamthilia lakini sipati info zake kwenye Google
Wewe unaitwa Rino Lenzi?

Ukisikiliza Radio One mpaka kesho mida ya mchana hua wanapiga Jingle ya hio tamthlia, kila tamthlia inapoanza Jamaa Lino alikua anatembea kwenye bonge moja la PikiPiki amejitanua alafu kuna kale kajingle kanapiga, alikua mbabe kwenye ile tamthlia, uki Google haiji maana ni ya zamani, sijajua kwa nini
 
Walikuwa na tamthilia moja inaitwa Beast Master nilikuwa naipenda sana
 
Nimekumbuka picha Moja hivi ilikuwa inaitwa "Mortal Combat"


Duuh... long time Sana.
 
Enzi hizo hakuna flash wala CD, video mnaangalia kwa kutumia mikanda inataka kufanana na biblia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…