ITV ilipofunguliwa mwaka 1994

ITV ilipofunguliwa mwaka 1994

chizcom

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2016
Posts
8,680
Reaction score
18,035
Kampuni ya IPP Limited mwaka 1994 inatambulisha chaneli ya Analog kwa jina ITV kupitia masafa ya mawimbi ya kawaida kipindi hiko.

Na kipindi hiko ndio mtaa mzima tumenunua TV ya PANASONIC TX iliyotoka 1993 sikumbuki model ikiwa ya rangi.

Kipindi hiko Tv inafunguliwa saa 8 au 10 sikumbuki ila inafungwa saa sita usiku.

Ndipo nilipo jua series kama:
*Family Matters
*Perfect Strangers
*fresh prince of bel air
*The V

Na matangazo kama :
*Revlon
*cocal cola

Kipindi hiko unaamka usiku kushuhudia ngumi za Mike Tyson.

Ila kuna dada mmoja ni kama mwarabu au muhindi fulani alikuwa ndo mtu wa kwanza ITV wanafungua ndo anaonekana sana. Hivi yupo wapi miaka 30 sasa.

Wenye kuijua ITV vizuri

[mention]pasco mayala [/mention] ni moja ya watu wenye kuijua ITV
 
Nimekumbuka the bold and the beautiful hiyo miaka ya 90, kulikuwa na tamthlia ya sunset beach, mara acapulco bay.

Mwendo wa kugeuza antena hapo, inaonyesha, geuza huko huko, aaaaah umeharibu rudisha upande wa mwanzo bado.

Pia sitosahau RFA walipozindua masafa ya FM nilikuwa bado mdogo sana nakumbuka bro wangu anaongea na rafiki yake kuhusu RFA na FM sikujua hata ni kitu gani ila kuanzia siku hiyo nikawa nasikia redio inazungumza vizuri.
 
Nimekumbuka the bold and the beautiful hiyo miaka ya 90, kulikuwa na tamthlia ya sunset beach, mara acapulco bay.
Mwendo wa kugeuza antena hapo, inaonyesha...
Mwenye ungo kipindi hiko anaogopeka. Sisi tuliokulia mitaa ya Sinza inayoanzia kijiweni kwenda mpaka mlimani na Mikocheni tulikuwa tunawaona watu matajiri sana.
 
Itv wanastahili kupewa super brand, maana ilifika wakati ikawa kama tv ya taifa kwa ubora wa muonekano na vipindi japo baadaye ikaja star tv na tvt. Kwa sasa itv bado iko vizuri ila hakuna mabadiliko makubwa kidigitali kama azam tv waliokuja kwa kasi ya ajabu kwenye soko la media. Azam kaongeza chaneli nyingi kuliko itv. Hata hivyo itv bado inatazamwa na watazamaji wengi wa taarifa ya habari
 
Back
Top Bottom