ITV: Rais Samia afanikisha timu nne kufuzu makundi Afrika

Luca Paguro

JF-Expert Member
Joined
Mar 26, 2023
Posts
502
Reaction score
1,141
Jamani naelewa vyombo vya habari vinamuogopa huyu mama, ila hii ni too much, khaaa πŸ˜‚πŸ˜‚
===========
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameandika historia mpya kabisa, baada ya kufanikisha timu nne za mpira wa miguu Tanzania kufuzu hatua ya makundi katika mashindano ya Afrika.

Timu hizo ni Simba na Yanga zilizofuzu hatua ya makundi michuano ya Klabu Bingwa Afrika, Azam na Singida zilizofuzu hatua ya makundi michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika.

Dkt. Samia aliazisha hamasa ya Goli la Mama ambapo alikuwa analipia kila goli linalofungwa kiasi cha Tsh Milioni 5 hivyo kufanya timu kuwa na hamasa zaidi ya kupata ushindi na kuondoka na kitita hicho cha pesa.
 
Hakuna Neno kama pia wangesema amesababisha kushindwa CHAN wakati imefanyikia nyumbani na kucheza na Timu Vibonde (Grade B kutoka Mataifa Mengine)

If your are quick to take Credit, atleast be ready to take some of the Blame...
 
oktoba mapemaaaa tu,, nisiguswe tapiga mtu jitahidi usiwe mfano


oktoba natiiiiiiiiiiiiiii
 
Mama anaupiga mwingi mno πŸ˜‚

Your browser is not able to display this video.
 
Hii ndo maana halisi ya watanzania wote ni nyumbu πŸ˜‚
 
Hii no chapa Lucas Mwashambwa?
 
Ni ukweli usiopingika mama ndio kafanikisha hili kutokea, motisha ya kila goli milioni 5 imekuwa chachu kwa timu zetu kujituma
 
Tz bila kulishwa makande mabichi nchi haipendezi kabisa, hawa waandishi kunahaja ya kuwatumbua majipu nyau hawa.
 
Naomba timu zote NNE zitolewe kwenye makundi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…