ITV: Ripoti Maalum-Mwandishi wenu ajifunze Kiswahili sanifu

Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2014
Posts
16,419
Reaction score
26,594
Huyu mwandishi wa ITV ana ripoti vizuri lakini kushindwa kuongea kiswahili sanifu kumenikera sana.

Huyu mwandishi anaitwa Silemu, katika kipindi cha kuwahoji hao vijana waliotapeliwa fedha na kampuni ya QNET.

Akimwuliza au kuhoji mtu, badala ya kumuuliza UMETOA KIASI GANI, yeye anauliza UMETOA BEI GANI!
Hii inatia mashaka juu ya elimu na basic training ya mwandishi.

Kama mwandishi hajui tofauti kati ya BEI na KIASI kwa maana ya fedha basi huo ni udhaifu mkubwa katika weledi wa watangazaji wa ITV.

Huku ni kuendeleza ujinga!
 
Yote kwa yote, hawa vijana wanapataje pesa zao, maana wanaaminishwa ujinga sana, sasa sijui kama wataweza kurudisha M5 zao
 
Isaya : Mlango 6​

1 Katika mwaka ule aliokufa mfalume Uzia nalimwona Bwana ameketi katika kiti cha enzi, kilicho juu sana na kuinuliwa sana,

Kuna mawili hapo, kufa kwa mfalme, huanza majira mengine mapya, ya aither, Nchi istawi na wananchi kula mema ya nchi na au wananchi kushi kwenye vilio na mateso yasiyo koma!

Anaweza kufa mfalume, nchi ikssitawi na au ikawa kinyume chake!!

Wewe unalionaje hili mwananchi mwenzangu!?

Yanapozaliwa mambo ya hovyo hovyo na kuwafanya wananchi watoe machozi, inaweza kuleta tafsri gani?
 
Jamani tunapozungumzia hao qnet, tusisahau na hii michezo ya kamari maarufu kama 'bonanza' nayo ni janga. Kuna mtoto katoroka kwao baada ya kucheza kamari hela aliyotumwa kwa mahitaji mengine.

Siku ya tatu, hajulikani yuko wapi,anakula nini na analala wapi? Na ni mtoto wa shule ya msingi. Ikiwezekana Serikali ipige marufuku hizi 'game'

Yote kwa yote hawa qnet wakianza kuuwa kama vibaka mtaani ndio serkali itashtuka

Wanatoa watoto vijijini kuja mjini kuwafunza utapeli wazi watoto wamekonda wameisha wanalala kama wafungwa na kushindia biscuits tu ,kila siku polisi tu

USSR
 
Hapo umeongelea majanga mawili kwa wakati mmoja
1.janga la waandishi kuharibu lugha limeshika kasi sana tena wengine wanafanya kusudi tu
-watangazaji
-mareporter
- mapresenter
-nk nk

2.swala la michezo ya hela (kamari na bahati nasibu) pia linatumalizia vijana na akili
-kubeti
-bonanza
-casino
-mashindano
-nk nk
 
Hawa jamaa wana imani kali zaidi ya mashahidi wa jehova.

They know one day wipl bacome rich. .na hawakati tamaa any more.

Hata huku watu wamepigwa na hakuna kitu wamepata...
 
Huyu mwandishi wa ITV ana ripoti vizuri lakini kushindwa kuongea kiswahili sanifu kumenikera sana.

Huyu mwandishi anaitwa Silemu, katika kipindi cha kuwahoji hao vijana waliotapeliwa fedha na kampuni ya QNET.

Akimwuliza au kuhoji mtu, badala ya kumuuliza UMETOA KIASI GANI, yeye anauliza UMETOA BEI GANI!
Mkuu Jidu La Mabambasi, this is too much, ni kumuonea bure Mtangazaji!. Neno kiasi gani na bei gani are the words that means the same, hakuna kosa lolote hapo!.
Kama mwandishi hajui tofauti kati ya BEI na KIASI kwa maana ya fedha basi huo ni udhaifu mkubwa katika weledi wa watangazaji wa ITV.
Sio kweli!. Hayo maneno mawili means the same.
Huku ni kuendeleza ujinga!
Sio kweli!.
P
 
Mkuu Paskali, wewe ni mwandishi nguli katika fani ya uandishi na utangazaji.
Mimi vile vile ni mdau.
Kwa mwandishi kushindwa kutofautisha BEI(value) na KIASI(amount) hapo kuna ukakasi.
Wakati BEI kama nilivyo itafsiri hata kwa lugha nyingine kama value,inavutika kimtazamo, KIASI kwa maana ya fedha au amount haivutiki, ni static.

Unaweza kuwa na Dollar 1000 mkononi, KIASI chake kitabaki kuwa Dollar 1000, lakini BEI yake kwa hela ya kiTanzania itacheza. Huu ni mfano tu.

Hivyo BEI itabaki kuwa ni uthamani wa kitu kwa wakati uliopo na inabadilika , wakati KIASI cha fedha inabaki ile ile.

BEI na KIASI cha fedha ni vitu viwili tofauti.
 
Huyu mwandishi wa ITV ana ripoti vizuri lakini kushindwa kuongea kiswahili sanifu kumenikera sana.

Huyu mwandishi anaitwa Silemu, katika kipindi cha kuwahoji hao vijana waliotapeliwa fedha na kampuni ya QNET.

Akimwuliza au kuhoji mtu, badala ya kumuuliza UMETOA KIASI GANI, yeye anauliza UMETOA BEI GANI!
Hii inatia mashaka juu ya elimu na basic training ya mwandishi.

Kama mwandishi hajui tofauti kati ya BEI na KIASI kwa maana ya fedha basi huo ni udhaifu mkubwa katika weledi wa watangazaji wa ITV.

Huku ni kuendeleza ujinga!

Kuna njia nyingi za kupata uelewa mpana wa maana za maneno. Moja ya hizo njia ni kuangalia definitions za equivalent words za hayo maneno katika lugha nyingine.

Bei (nomino) kwa lugha ya Waingereza ni price (noun). Hili nadhani halina ubishani. Ukiangalia definitions za neno price utaona kwamba moja ya definitions za neno price linapotumika kama noun ni hii ifuatayo:

[the amount of money expected, required, or given in payment for something.]

Obviously, mwandishi alipowauliza wametoa bei gani, hakufanya uchafuzi wowote wa lugha ya Kiswahili. Hapo alikuwa anawauliza juu ya “the amount of money given in payment for something”, kitu ambacho hakikinzani na definition ya neno price kama inavyoonekana hapo juu.

Phrase “kiasi gani” doesn’t necessarily mean price. Unaweza kutoa hicho kiasi na bado kikawa sio bei. Neno bei linatumika pale kunapokuwa na expection of something in return. Mtu akitoa kwako kiasi cha 500/= kama zawadi, hapo hatuwezi kusema kwamba amelipa bei ya 500/=, kwasababu there’s nothing expected in return.

Kwa hiyo, uwe na amani tu; hakuna uchafuzi wowote wa lugha ya Kiswahili uliotokea hapo!
 
Huyu mwandishi wa ITV ana ripoti vizuri lakini kushindwa kuongea kiswahili sanifu kumenikera sana.

Huyu mwandishi anaitwa Silemu, katika kipindi cha kuwahoji hao vijana waliotapeliwa fedha na kampuni ya QNET.

Akimwuliza au kuhoji mtu, badala ya kumuuliza UMETOA KIASI GANI, yeye anauliza UMETOA BEI GANI!
Hii inatia mashaka juu ya elimu na basic training ya mwandishi.

Kama mwandishi hajui tofauti kati ya BEI na KIASI kwa maana ya fedha basi huo ni udhaifu mkubwa katika weledi wa watangazaji wa ITV.

Huku ni kuendeleza ujinga!
Mojawapo ya vitu vilivyomsababisha SABAYA akonekana mbaya huko HAI ni pamoja na kuipinga hadharani hiyo Q-Net.

Sasa ndio mambo yanaanza kuonyesha matundu taratibu.
 
Mkuu Paskali, wewe ni mwandishi nguli katika fani ya uandishi na utangazaji.
Mimi vile vile ni mdau.
Kwa mwandishi kushindwa kutofautisha BEI(value) na KIASI(amount) hapo kuna ukakasi.
Wakati BEI kama nilivyo itafsiri hata kwa lugha nyingine kama value,inavutika kimtazamo, KIASI kwa maana ya fedha au amount haivutiki, ni static.

Unaweza kuwa na Dollar 1000 mkononi, KIASI chake kitabaki kuwa Dollar 1000, lakini BEI yake kwa hela ya kiTanzania itacheza. Huu ni mfano tu.

Hivyo BEI itabaki kuwa ni uthamani wa kitu kwa wakati uliopo na inabadilika , wakati KIASI cha fedha inabaki ile ile.

BEI na KIASI cha fedha ni vitu viwili tofauti.

Bei sio value, bali ni price. Price na value sio lazima zifanane. Wewe ukimuuzia rafiki yako kipenzi gari kwa discounted price ya $5,000 badala ya market price ya $10,000, price ya hiyo gari kwake inatofautiana na value yake. Rafiki yako atakuwa amelipa bei ya $5,000 na amepata gari ya thamani ya $10,000. Haitakuwa sahihi kusema kwamba value (thamani) ya hiyo gari ni $5,000 aliyokulipa rafiki yako!

Afadhali useme bei ni cost (gharama) badala ya kusema value (thamani).
 
Mkuu Jidu La Mabambasi, this is too much, ni kumuonea bure Mtangazaji!. Neno kiasi gani na bei gani are the words that means the same, hakuna kosa lolote hapo!.

Sio kweli!. Hayo maneno mawili means the same.

Sio kweli!.
P
Mayala wewe nawe lugha huwa inakuwa shida sana. Kiswahili na kiingereza. Kiasi - amount
Price - bei
Huwezi sema umetoa bei gani ukimaanisha umetoa kiasi gani. Kama unauza unaweza sema umeuziwa kwa bei gani. Lakini kama umelipa si sawa kusema umelipa bei gani. Hii lugha ina wenyewe msiharibu halafu mkielekezwa mnashupaza shingo.
 
Huyu mwandishi wa ITV ana ripoti vizuri lakini kushindwa kuongea kiswahili sanifu kumenikera sana.

Huyu mwandishi anaitwa Silemu, katika kipindi cha kuwahoji hao vijana waliotapeliwa fedha na kampuni ya QNET.

Akimwuliza au kuhoji mtu, badala ya kumuuliza UMETOA KIASI GANI, yeye anauliza UMETOA BEI GANI!
Hii inatia mashaka juu ya elimu na basic training ya mwandishi.

Kama mwandishi hajui tofauti kati ya BEI na KIASI kwa maana ya fedha basi huo ni udhaifu mkubwa katika weledi wa watangazaji wa ITV.

Huku ni kuendeleza ujinga!
Watanzania wengi wanaongea kiswahili cha kusikia mitaani, hilo tatizo si kwa huyo tu bali watangazaji wengi ndivyo walivyo.
 
Isaya : Mlango 6​

1 Katika mwaka ule aliokufa mfalume Uzia nalimwona Bwana ameketi katika kiti cha enzi, kilicho juu sana na kuinuliwa sana,

Kuna mawili hapo, kufa kwa mfalme, huanza majira mengine mapya, ya aither, Nchi istawi na wananchi kula mema ya nchi na au wananchi kushi kwenye vilio na mateso yasiyo koma!

Anaweza kufa mfalume, nchi ikssitawi na au ikawa kinyume chake!!

Wewe unalionaje hili mwananchi mwenzangu!?

Yanapozaliwa mambo ya hovyo hovyo na kuwafanya wananchi watoe machozi, inaweza kuleta tafsri gani?
QNET Ni yakitambo na watu wengi walilizwa hata kabla ya kifo cha Mfalme Uzia.
 
Bei sio value, bali ni price. Price na value sio lazima zifanane. Wewe ukimuuzia rafiki yako kipenzi gari kwa discounted price ya $5,000 badala ya market price ya $10,000, price ya hiyo gari kwake inatofautiana na value yake. Rafiki yako atakuwa amelipa bei ya $5,000 na amepata gari ya thamani ya $10,000. Haitakuwa sahihi kusema kwamba value (thamani) ya hiyo gari ni $5,000 aliyokulipa rafiki yako!

Afadhali useme bei ni cost (gharama) badala ya kusema value (thamani).
Sikubaliani na mtazamo wako ingawaje ni kweli bei ni sawa na price.
Na mfano uliotoa sidhani kama unaenda kuelezea tofauti ya bei(inayovutika na si static), na kiasi( ambayo ni static na haivutiki).
Ukiniambia mfukoni nia bei gani ni kosa kubwa.
Lakini sahihi ni nina kiasi gani mfukoni-a fixed amount.
 
Mkuu Jidu La Mabambasi, this is too much, ni kumuonea bure Mtangazaji!. Neno kiasi gani na bei gani are the words that means the same, hakuna kosa lolote hapo!.

Sio kweli!. Hayo maneno mawili means the same.

Sio kweli!.
P
...Ni maneno yaana Moja lakini inategemea unayatumia vipi katika Sentensi Yako.
Unaweza ukalitumia Moja kwenye Sentensi Moja lakini kwenye Sentensi nyingine ukawa umeharibu Kwa kulitumia Hilo!
Hamuonei. Mtangazaji amekosea kulitumia Hilo wakati angweza kutumia Hilo lingine... Kama anavyoanisha Bwana Jidula.
Mayala, Umeanza kusahau Fani??
 
Back
Top Bottom