ITV: Ripoti Maalum-Mwandishi wenu ajifunze Kiswahili sanifu

Huyu mwandishi wa ITV ana ripoti vizuri lakini kushindwa kuongea kiswahili sanifu kumenikera sana.

Huyu mwandishi anaitwa Silemu, katika kipindi cha kuwahoji hao vijana waliotapeliwa fedha na kampuni ya QNET.

Akimwuliza au kuhoji mtu, badala ya kumuuliza UMETOA KIASI GANI, yeye anauliza UMETOA BEI GANI!
Hii inatia mashaka juu ya elimu na basic training ya mwandishi.

Kama mwandishi hajui tofauti kati ya BEI na KIASI kwa maana ya fedha basi huo ni udhaifu mkubwa katika weledi wa watangazaji wa ITV.

Huku ni kuendeleza ujinga!

Hata wewe imekuwa ni vigumu kwako kutofautisha kati ya bei na thamani.

Sisemi nakosoa au kuunga mkono alichofanya mwanahabari, bali nakumbusha kwamba, tunajifunza matumizi ya lugha kwa zaidi ya miaka 20 ya makuzi na maisha yetu, lakini tunasomea taaluma ya uwanahabari kwa miaka michache sana.

Pamoja na taaluma si ajabu mara chache ukajikuta umetumia misamiati uliyozoea na bila kujua ina utofauti wa maana kwenye ufasaha wa lugha.

Na mara nyingine hata sisi wasikilizaji huwa tunahukumu watu kukosea au kupatia matumizi ya maneno kwa kipimo cha uzoefu wetu na sio usahihi. Unaweza dhani mtu amekosea kumbe ni wewe hujazoea matumizi ya neno husika.
 
Mkuu sisi wengine tumesoma kama somo lugha ya kiswahili.
Maneno na makuuzi ya mitaani hayana nafasi katika utangazaji hasa kwenye vyombo vyenye hadhi ya ku promote kiswahili kimataifa.
 
Vijana wanamatumaini ya kutoboa sana. Serikali izuie hii Qnet ni utapeli mtupu.
 
Back
Top Bottom