ITV - What's your Business Model

ITV - What's your Business Model

Logikos

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2014
Posts
15,460
Reaction score
24,233
Katika hii Biashara ya Luninga mara nyingi kipato na faida ya TV husika inategemea Matangazo (wafadhili kufadhili kipindi husika) au Subscription kwenye Pay TV...

Sasa hawa ndugu zangu naona siku hizi vipindi vinakatishwa ghafla kujiunga mahali popote kiongozi anapoongea.., yaani wanafanya zile kazi za TV ya Taifa ambayo yenyewe ni sawa ikifanya hayo sababu inaendeshwa kwa Ruzuku..,

Sio hivyo tu leo nimeona kipindi kilichotengenezwa na AZAM na wakitangaza wanatangaza ni AZAM tena cha mwaka 2017 kinarushwa leo 2019 (sijui Mr Photogenic)

Sasa nashindwa kuelewa kama hii ndio super brand inaelekea huku tutabaki tunaangalia nini ? Na kwenye kipato kama wanafanya kazi za Taifa sponsorship wanapata wapi au ni scratch my back, i will scratch yours ?
 
Mambo magumu siku hizi...

Cc: mahondaw
Kwahio ndio hawaingizi pesa ? Si ugumu utazidi...., au kufanya kazi za TBC hata bila malipo wanapata malipo indirectly.... Nipo hapa kujifunza huenda kuna njia ya tatu ya mapato..., hata kama ipo na ni ya muda mfupi inabidi waangalie wasije kushusa brand yao iliochukua miaka kuitengeneza (wasiache mbachao kwa msala upitao..)
 
Hawakosei sababu waangaliaji wengi wanafuatilia matukio ya Rais

Anaefanya biashara ya TV anatarget waangaliaji wengi kwanza ili wanaoenda kufanya biashara ya matangazo nae wawe wengi. Watu wa mitandao ya simu kwa mfano watakilipa hela nyingi kituo cha Runinga kinachoangaliwa na wengi and vice versa
 
Kiongozi akipaki gari sehemu na kuongea na watu huwa hakuna mfadhili yeyote.. (kumbuka siku hizi hayo matukio sio planned na yanatokea kama uyoga), mbaya zaidi ni kipindi fulani huwa kinakatishwa.., kwahio unless wanapata pesa toka serikalini sidhani kama itakuwa rahisi mfadhili kutoa sponsorship ya kipindi fulani ambacho hajui ni muda gani kitakatishwa kujiunga popote Mheshimiwa anapoongea..., pia nadhani hio kazi TBC wanaifanya vyema ukizingatia wanapata ruzuku hata watu wasipotangaza bado inaweza kupewa fungu ili kuonyesha yale yenye manufaa kwa taifa

Pia kumbuka ITV ilijijenga kama TV ambayo ipo neutral (haina mlengo wowote) sasa hivi naona inapoteza muelekeo
 
Mkuu wanalazimishwa kuonesha hizo ziara.....ukikataa utakiona cha mtema kuni.....
mbona Star TV hawalazimishwi ?, mi nadhani wanainvest kwenye future kama ule unjanja wa Clouds walivyokuwa wanabembeleza ukaribu na Jakaya...
 
Katika hii Biashara ya Luninga mara nyingi kipato na faida ya TV husika inategemea Matangazo (wafadhili kufadhili kipindi husika) au Subscription kwenye Pay TV...

Sasa hawa ndugu zangu naona siku hizi vipindi vinakatishwa ghafla kujiunga mahali popote kiongozi anapoongea.., yaani wanafanya zile kazi za TV ya Taifa ambayo yenyewe ni sawa ikifanya hayo sababu inaendeshwa kwa Ruzuku..,

Sio hivyo tu leo nimeona kipindi kilichotengenezwa na AZAM na wakitangaza wanatangaza ni AZAM tena cha mwaka 2017 kinarushwa leo 2019 (sijui Mr Photogenic)

Sasa nashindwa kuelewa kama hii ndio super brand inaelekea huku tutabaki tunaangalia nini ? Na kwenye kipato kama wanafanya kazi za Taifa sponsorship wanapata wapi au ni scratch my back, i will scratch yours ?
ina maana hujui kwamba live tv content zinazomuhusu jiwe zinawatazamaji wengi?.

sio kwamba watz wanampenda sana, la hasha. ni ile tabia yake ya kuja na matukio ya papo kwa papo ya kushangaza. kwa hiyo anapokuwa live kwenye tv, wananchi hutazama ili kusuburi atakuja na tukio gani.

tv zote kuanzia azamtv na itv walishalibaini hilo. so wanawapa wateja wao ile kitu wanataka.
 
mbona Star TV hawalazimishwi ?, mi nadhani wanainvest kwenye future kama ule unjanja wa Clouds walivyokuwa wanabembeleza ukaribu na Jakaya...

Unapigiwa simu kutoa support ya kurusha event....kumbuka “A king’s request is always a command”......we unadhan Harmonize ameamua tu mwenyewe kutoa nyimbo ya sifa?
 
ina maana hujui kwamba live tv content zinazomuhusu jiwe zinawatazamaji wengi?.

sio kwamba watz wanampenda sana, la hasha. ni ile tabia yake ya kuja na matukio ya papo kwa papo ya kushangaza. kwa hiyo anapokuwa live kwenye tv, wananchi hutazama ili kusuburi atakuja na tukio gani.
kwenye zile hafla huwa hakuna tangazo lolote apart from kuonyesha ITV Mubashara; akaunti yao ya Facebook na Twitter.., kumbuka nyingi zinatokea mchana, sasa mtu ameitwa kuja kwenye Meza Huru ili auze sura..., ghafla tunajiunga sijui wapi au mtu anaangalia zake IRIS ghafla anajiunga kwingineko..., kumbuka kama ni kumuona tu watu wangecheki TBC alafu this day and age wangeweza kuweka haya matukio hata huko Youtube...

Pili TV za sasa inabidi kuwa mbunifu kutoa vitu original sio kazi ya kuripoti tu.., ningewaona wa maana kama wangekuwa hizo ziara wanazidadavua na kutoa news behind the news yaani pande zote za shilingi.., sasa kama wanafanya kazi ambayo naweza kuona toka kwa Milad Ayo Yuotube, kuna umuhimu kweli wa kuwa na wanahabari magwiji na wachambuzi ?
 
Kwahio ndio hawaingizi pesa ? Si ugumu utazidi...., au kufanya kazi za TBC hata bila malipo wanapata malipo indirectly.... Nipo hapa kujifunza huenda kuna njia ya tatu ya mapato..., hata kama ipo na ni ya muda mfupi inabidi waangalie wasije kushusa brand yao iliochukua miaka kuitengeneza (wasiache mbachao kwa msala upitao..)
Wanalipwa na kurugenzi ya habari chini ya msigwa.

So hakuna cha bure pale.
 
Wanalipwa na kurugenzi ya habari chini ya msigwa.

So hakuna cha bure pale.
hilo ndio lilikuwa swali langu sasa kwanini wasiboreshe TBC kuliko kuharibu Kodi zetu kwa kutuharibia alternatives au kama vipi wainunue kabisa iwe TBC Alternative
 
Unapigiwa simu kutoa support ya kurusha event....kumbuka “A king’s request is always a command”......we unadhan Harmonize ameamua tu mwenyewe kutoa nyimbo ya

kijana napenda sana unavyoimba ningefurahi kama siku mojja ungetunga kawimbo cha kupongeza juhudi za serikali ya awamu ya tano ah ah ah......
 
Mkuu wanalazimishwa kuonesha hizo ziara.....ukikataa utakiona cha mtema kuni.....
Je wembe bado ni ule ule ? Kuna Mechi ya mpira ilisitishwa hapo nyuma na wengine kubadilisha mechi kuwa mkutano wa kisiasa hao walilazimishwa au tumegeukwa kuwa jumuia ya machawa ?
 
Back
Top Bottom