SoC01 Iundwe idara ya ambulance na uokoaji ili kusaidia kwenye dharura na uokoaji kuepusha vifo vinavyoepukika kwa kuwahi matibabu

SoC01 Iundwe idara ya ambulance na uokoaji ili kusaidia kwenye dharura na uokoaji kuepusha vifo vinavyoepukika kwa kuwahi matibabu

Stories of Change - 2021 Competition

buffalo44

JF-Expert Member
Joined
May 8, 2016
Posts
4,678
Reaction score
11,357
Salaam wakuu.

file-20210428-23-vm7bbd.jpg

Nchi hii ni yetu sote, matatizo yetu tunaweza kuyatatua kwa rasimali kidogo tulizonazo. Hapa Tanzania suala la Ambulance hata hatuelewi linafanyaje kazi. Mara nyingi ambulance zinasafirisha referred patient (Wagonjwa pendekezwa kwenda hospital nyingine).

Kwa matatizo ya dharura hatujui jinsi ya kuipata ambulance kama ipo hatujui namba vizuri.

Katika kuongeza upatikanaji bora wa huduma za afya ikiwemo wakati wa dharura. Napendekeza iunde idara ya ambulance kama ilivyo jeshi la zimamoto na uokoaji. Iitwe Idara ya dharura na uokoaji. Iwe connected na hospital zote kwa wagonjwa wenye bima. Popote hospital iliyokaribu unapelekwa.

Hii itasaidia.
• Kuongeza ufanisi wa mfumo wa afya wa nchi (Health System).
• Itapunguza vifo vya wajawazito na wagonjwa wa dharura wanaopoteza maisha kwa kuchelewa hospitalini.
• Itasaidia nchi kupiga hatua kwenye maendeleo ya watu.

Naamini serikali ikiwa inaweza kununua MAV8 Sidhani kama watashindwa kuongeza ambulance kwenye idara ya dharura kukiwa na nia ya dhati.

Idara ikishaundwa kuwe na namba maalumu na nimetoa uzi wangu kuhusu suala la UZEMBE ukifanyiwa kazi nadhani hili la ambulance laweza kufanikiwa ikiwa tutapigia ambulance inaweza fika kwa wakati kuwahisha wagonjwa. Itasaidia kujenga imani ya wananchi kwa serikali. Kingine kuendeleza huduma za afya kuokoa vifo vinavyoepukika.

Ahsante sana wote mliosoma.
Nashukuru Uongozi wa JamiiForums kwa nafsi hii.
 
Upvote 0
Back
Top Bottom