Kwa ufupi tu naomba kusema yafuatayo, mpaka sasa mifumo yetu ya kiuchumi ishafeli sana, tumejaza watendaji ambao ni majizi, wabinafsi, wapenda rushwa, afu hawana ideas kabisa za kuisaidia hii nchi na si wazalendo hata kidogo.
Ukiangalia tunamapolicy mazuri kweli kwenye makabrasha ambayo ukiwapatia nchi ambayo iko serious inapiga hatua kubwa sana, Tanzania imebarikiwa kuwa na rasilimali watu wengi sana ingawa iyo rasilimali watu aina sifa za kijipambania yenyewe,kwa maaana ya mitahala yaelimu ni mibovu sana, kingine tuna ardhi kubwa sana na yenye rutuba lkn watekelezaji wa Sera kwa maaana ya wizara na idara zinazohusika ni wategemea mishahara mwisho was mwezi na marupurupu kibao, hawewezi kufikiria nje ya box, namna ya kuikwamua nchi kiuchumi kupitia kilimo, na mwisho chains nzima ikaenda kwenye viwanda....tukazalisha na kutengeneza ajira kwa kwa watu wetu kiwango kikubwa sana, Tanzania imezungukwa na nchi ambazo zinaitaji chakula kwa kiwango kikubwa sana,lkn mwisho was siku tunategemea misaada na mikopo nafuu kwa ajili ya kuendesha serikali, kumbe tunaweza kufanya uwekezaji ambao unakuja kufanya mapinduzi makubwa ya kilimo sambamba na viwanda vya uzalishaji Mali kwa manufaa ya nchi nzima vizazi vijavyo, tumezungukwa na mito na maziwa tunafeli wapi kuanzisha vilimo vya umwagiliziaji....
Tuunde taskforce ya watu wa kada ya uchumi na biashara pamoja na kilimo,ipewewe pesa km mtaji na waanzishe project kubwa nchini has a kikanda kimkakati zaidi, kuzalisha mazao amvayo tutayatumia nchini km chakula, kingine tuuze nje ya nchi na kupata fedha za kigeni, zingine ziingie kwenye viwanda vyetu vya ndani km maligafi.
Kwa mfano tuanze kuzalisha nini....kikanda zaidi....
Kanda moja izalishe mazao km mahindi, mtama,uwele, ufuta, alzeti.
Kanda yapili...pamba,alizeti, mpunga, mihogo...
Kanda nyingine, Korosho, choroko,dengu, karanga,
Kanda zingine katani,tangawizi,na viungo vyote,viazi, vitunguu swahumu,vitunguu maji...
Mazao yote ya mikakati yazalishwe kupitia iyo taskforce ndani ya muda Fulani waliopewa na mwisho tunakuja kupima ni wapi tumefika na wapi tunakwama, kumbuka tutatengeneza ajira kubwa sana kupitia kilimo kwa kuajiri watu...ndani ya hizo project.
Kufikia apo tutaweza kulisha viwanda vyetu vya ndani na kuondokana na uhaba wa bidhaa km mchele,sukari,mafuta ya kula,nk....natamani kuendelea lkn ngoja niishie apo...ninayo mengi sana hata mengine nashindwa kuaandika apa kwa lugha nyepesi