Karibu sana. Natumia wasaa huu pia kwa ajili ya walio na hali kama yako.
1.Tumia muda mwingi kuendelea kujifunza hasa kama una kipaji eneo fulani kama muziki, mchezo, au fani nyingineyo.
2.Ajira ni chache lakini fursa ni nyingi hasa kwenye ujasiriamali. Angalia eneo lenye uhitaji zaidi uingie hapo jikite zaidi kwenye namna ya kuuza (sales).
Kwa mfano unaweza kununua vitu kwa jumla ukauza kwa mtu mmoja mmoja.
3. Kutoa huduma. Huduma kama usafiri, ufundi, ushonaji,maji, usafi, uoshaji wa magari. Mnaweza kujiunga na wengine mkafanya.
4. Kilimo na ufugaji: hapa sio lazma ulime shamba au ufuge kuku. Unaweza kuongezea thamani mazao ya kilimo ukauza mf pilipili, korosho, ndizi, etc.
5. Mafunzo ya muda mfupi: tembelea sido pamoja na veta au taasisi nyinginezo pata mafunzo. Haya yanaweza kuwa akiba baadae ukaja kuyatumia. Mf screen printing, ufinyanzi, usindikaji, uokaji, sanaa za mikono. Etc.
6. Huduma ya taaluma. Kusanya madogo wa karibu na home. Piga pindi. Kusanya jero jero zako. Tena wakati wa likizo huo hapo. Ongea na wazazi wao. ( hii ni nzuri na niliwahi kuifanya)
7. Wadau watajazia, atakuja mtu atakwambia kaanga mihogo, pika sambusa, tengeneza kashata. Kata mshipa wa aibu fanya. Hakuna mtu atakupa hata mia jamaa yangu .