Nilipokuwa sekondari form I miaka ya 70 nilikuwa sijazoea kutandika kitanda nyumbani, hivyo kila siku nilikuwa napata adhabu kwa kutokutandika kitanda, baada ya hapo mpaka kesho siwezi kuanza kufanya kitu cho chote kabla ya kutandika kitanda. Ukiongezea na zoezi la JKT ndio kabisa. Yaani hata mke wangu asipotandika atakuta mie nimeshatandika tena bila kinyongo, maana hawa wanawake wa siku hizi......Wakati mwingine nikiwa safarini kwenye lodge au hoteli najisahau na kuanza kutandika!!!Mwalimu JK alisema "Usafi ni Tabia"