mwallu
JF-Expert Member
- Sep 5, 2013
- 6,787
- 4,210
Ni saa tano na nusu bado nimejilaza hapa kitandani.Naangaza kila pembe ya chumba changu lakini sioni mabadiliko yoyote chumbani.Moyo unanidunda dunda sana japo najua siumwi.
Mara ''ngo ngo ngo,sister mwallu watoto wamefika''
Ni sauti ya doto,mtawa mwenzangu....kha! ndo nakumbuka nina jukumu la kuwasimamia watoto kwenye mazoezi ya nyimbo na maigizo maana kesho kutwa tuna ugeni mzito hapa parokiani.
Apa najishauri sana kuamka,moyo bado unadunda dunda.
.
Nakumbuka juzi mchana alikuja mkaka hapa OLA (Our Lady of Apostles)..alikuja direct kama mgeni wangu,akiwa na vifaa vya mazoezi vya watoto (kwa maneno ya mtawa doto huyo kijana amejitolea kuwasaidia watoto japo naanza kupata mashaka if that was the only reason)
Ile salaam tu,nilisikia moyo ukipiga paa na kizunguzungu kwa mbaali,nikajikuta na ng'wenya ng'wenya tuu..akajitambulisha majina yake,kazi yake na mahali alikotoka..cha ajabu vyote hivyo nimevisahau, sijui kwa kua nilikua namuangalia tuu nafurahia vile anaongea ?
Sasa najiuliza kwa nini hali hii inipate baada ya kumuona yeye tu? maana ata situlii,moyo unadunda dunda tuu toka juzi,halafu watawa wenzangu wanadai huyu mkaka huwa anakuja saana parokiani..hakosi hata wiki moja,mbona mi sijawahi kumuona?
Aaagh! ngoja tu nijiandae nikafanye mazoezi na watoto. Na huu mdundo wa moyo uache matendo shitukizi,kurupushi,tetemeshi na ushindwe kabisa.
Ila kwa mbaali tena natamani huyo mkaka aje tena,safari hii nitakua makini nipate details zake vizuri.
Hivo Kaizer nakuomba unisaidie kitu kimoja,tupange semina ya vijana hapa,kila kijana atakaekuja kwenye maungamo mhamasishe ahudhurie semina hiyo,tarehe na mwezi tutapanga.naamini nitamtambua tu hata kwa sauti,hivyo kila mhudhuriaji atakua mchangiaji.na wasemaji wakuu nitaomba Heaven on earth na Mentor Asprin na Mamndenyi wasimamie:
NB:Naupenda sana utawa,na sitoacha wito huu,
ilaaa...niko tu curious kumfaham huyu mkaka-hata sielewi kama ndo najaribiwa au la.
copy kwa: @Ladyfurahia DEMBA Arushaone Kaizer shansarie kiwatengu Erickb52 Baba V Chocs Lady doctor na woooteeeee