Nikujibu kama ifuatavyo:
Wakati wengi wa kipato cha chini ambao wengi wao huanzia na laki moja na wanaweza kuyamudu maisha, wakati we huna anayekutegemea ila ni kupiga kitabu tu, kama utafikiria kwamba mchumia juani hulia kivulini unaweza kukubaliana nami kuwa kwa mahitaji muhimu na ya lazima inatosha na kubaki ziada ya kurudufia material.
Mimi wakati mwingine nilipokuwa chuo tulikuwa tuna share baadhi ya mambo, mimi nikirudufu leo, tunashea na rafiki yangu ambaye yeye atarudufu kesho. Kuna ubaya gani wakati ukifiki nikishahitimu nitafanya nitakavyo?
Yakhe, achana na ziada ya viyoyozi, fridge, na vinginevyo vya kuwastarehesha marafiki wakike kwani si wakati wake, asiyekubali urafiki kwa vile tu huna virutubisho hivyo ni mtafutaji.