Ivory Coast: Wananchi maelfu waingia mtaani kumkataa Mgombea Urais wa chama tawala kugombea muhula wa nne

Ivory Coast: Wananchi maelfu waingia mtaani kumkataa Mgombea Urais wa chama tawala kugombea muhula wa nne

Huyo Laurent Gbagbo, mwenyewe ana miaka 80. Alishaongoza kwa miaka 10.

MWaka 2010 alishindwa uchaguzi, huyo Rais(Alassane Ouattara) wa sasa alishinda.
Ila jamaa akagoma , mpka jeshi linalomuunga mkono Alassane Ouattara, pamoja na majeshi ya ufaransa yalipomtoa madarakani.
Wananchi wakashangilia.

Sasa hivi kibao kimegeuka Ouattara hataki kuachia madaraka.
Wananchi wanamtaka Gbagbo.

Hivi hakuna mtu mpya huko?
Aisee acha tu Trump atuite shithole kmmk
 
Maelfu ya raia wa Ivory Coast waliingia mitaani mjini Abidjan, mji mkuu wa taifa hilo la Afrika Magharibi, kupinga kuondolewa kwa viongozi wa upinzani kwenye uchaguzi wa rais unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni.

Ivory Coast, ambayo ndiyo uchumi mkubwa zaidi katika Afrika Magharibi inayozungumza Kifaransa, inatarajia kufanya uchaguzi wa rais mwezi Oktoba. Mapema mwaka huu, viongozi wakuu wanne wa upinzani, wakiwemo Rais wa zamani Laurent Gbagbo na Mkurugenzi Mkuu wa zamani wa Benki ya Credit Suisse, Tidjane Thiam, wamezuiwa kugombea na tume ya uchaguzi.

Waandamanaji walikusanyika Jumamosi asubuhi huko Yopougon, kitongoji chenye watu wengi katika mji mkuu Abidjan, wakiwa na mabango yenye jumbe kama: “Imetosha!”, “Hakuna demokrasia ya kweli bila haki ya kweli,” na “Sisi ni mamilioni tunasema NDIO kwa Gbagbo na Thiam.” Gbagbo na Thiam waliungana mapema mwaka huu ili kumpinga Rais anayeongoza sasa, Alassane Ouattara.

Mwezi uliopita, Ouattara mwenye umri wa miaka 83 alitangaza kuwa atagombea muhula wa nne. Urais wake unapingwa baada ya kubadilisha katiba mwaka 2016 na kuondoa ukomo wa mihula ya urais.

“Hatupendi muhula wa nne, na tunataka orodha ya wapiga kura ipitiwe upya, hicho ndicho tunachodai,” alisema Sagesse Divine, mwanaharakati aliyeshiriki maandamano ya Jumamosi. “Tunataka majina ya wagombea wote yajumuishwe, na tunataka twende kwenye uchaguzi kwa amani, hicho ndicho tunachotaka.”
==================
Thousands of Ivorians took to the streets in Abidjan, the capital of the West African nation, to protest against the exclusion of opposition leaders from the upcoming presidential election.

Ivory Coast, the biggest economy of francophone West Africa, is due to hold a presidential vote in October. Earlier this year four main opposition figures, including former President Laurent Gbagbo and former Credit Suisse chief executive Tidjane Thiam, have been barred from running by the electoral commission.

Protesters gathered Saturday morning in Yopougon, a densely populated suburb of the capital Abidjan, holding banners with messages such as: “Enough is enough!”, “No true democracy without true justice,” and “We are millions saying YES to Gbagbo and Thiam.” Gbagbo and Thiam joined forces earlier this year to challenge incumbent President Alassane Ouattara.

Last month, 83-year old Ouattara announced that he would seek a fourth term. Ouattara’s candidacy is contested after he changed the constitution in 2016 to remove presidential term limits.

“We don’t want a fourth term, and we want the electoral roll revised, that’s what we are asking for,” said Sagesse Divine, an activist who participated in Saturday's march. “We want all candidates’ names included, and we want to go to the elections in peace, that’s all we want.”
Matatizo yale yale yanajirudia.
 
Political power addiction inafanya kazi katika brain the same pathway na heroine or cocaine addiction.
Usishangae hata kwa mama yenu na Jumanne Kaseja, shida inayowatesa ni political power addiction ambayo ina athiri ubongo sawa na heroine
Hatari sana
 
Wassira anateuliwa, Biden alipita kwa kura za uchaguzi mkuu na ameng'atuka pia.

Hao shida yao ni kwamba pamoja na umri wao kusogea bado wanayataka madaraka lwa kupitia dirishani.
aya kashangae umri wa Paul Biya bado hujaenda GUINEA then muone yule Gen Alli wa Uganda ambae amependekezwa kugombea ubunge
 
aya kashangae umri wa Paul Biya bado hujaenda GUINEA then muone yule Gen Alli wa Uganda ambae amependekezwa kugombea ubunge
Hivi unaelewa hata nilichomaanisha hapo??
Ishu ni kwamba pamoja na umri wako mkubwa ambao unawafanya washindwe kufanya baadhi ya majukumy bado wanajiongezea miaka ya kukaa madarakani kinyemela kwa kubadili katiba.
 
Huyo Laurent Gbagbo, mwenyewe ana miaka 80. Alishaongoza kwa miaka 10.

MWaka 2010 alishindwa uchaguzi, huyo Rais(Alassane Ouattara) wa sasa alishinda.
Ila jamaa akagoma , mpka jeshi linalomuunga mkono Alassane Ouattara, pamoja na majeshi ya ufaransa yalipomtoa madarakani.
Wananchi wakashangilia.

Sasa hivi kibao kimegeuka Ouattara hataki kuachia madaraka.
Wananchi wanamtaka Gbagbo.

Hivi hakuna mtu mpya huko?
Hawa watu wanashangaza sana. Kipindi kile Laurent Gbagbo anagoma kutoka madarakani, huyu Alassane Ouatarra alipiganiwa sana na wananchi kwa maandamano kiasi cha kusababisha mpaka mauaji!

Halafu cha kushangaza na yeye baada ya kumaliza mihula yake ya uongozi, na yeye ameamua kufuata mtindo ule ule wa kung'ang'ania madaraka!
 
Mambo ya ajabu sana.
 
Hivi unaelewa hata nilichomaanisha hapo??
Ishu ni kwamba pamoja na umri wako mkubwa ambao unawafanya washindwe kufanya baadhi ya majukumy bado wanajiongezea miaka ya kukaa madarakani kinyemela kwa kubadili katiba.
Nimekuelewa. Hivi yule Gen Alli wa Uganda unahisi anaweza kufanya kitu?
 
Back
Top Bottom