Iwapo tunapunguza Utoaji Huduma (kubinafsisha); kwanini Kodi hazipungui? Je, tunaongeza kumbana Mwananchi ili kutoa (huduma) gani?

Logikos

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2014
Posts
15,460
Reaction score
24,233
Kodi ni muhimu sana ili kufadhili shughuli za serikali, huduma kwa umma kama vile barabara na mashule, Usalama wa Jamii, Afya na Mengineyo.

Sasa kama hata hayo kuanzia Elimu (Mikopo na Shule Binafsi); Afya tuna BIMA ya Afya na kulipia Private; Kuhakikisha wafanyakazi wanalipwa ujira stahiki hilo pia limekwenda kwenye free market...; Usafiri tuna watu binafsi n.k.; Ujenzi wa Barabara tunafanya PPPs which means hata gharama ya kulipia hio Miradi tutalipa kwa levies na tolls.

Mbaya zaidi huduma nyingi za watu binafsi gharama imekuwa kubwa sababu ya Tozo za Serikali (mfano bila Tozo, bundle, kutuma miamala na hata mafuta yangekuwa bei rahisi zaidi).

Unaweza kusema watu wameongezeka wanaohitaji huduma sio kama zamani nami takujibu kwamba hata watoaji pia wameongezeka na pia huduma siku hizi watu hawapati kama mwanzo bali wanailipia.

Vilevile kuna Makusanyo ambayo awamu za zamani walikuwa hawama mfano VAT, hii alikuja nayo Mkapa hivyo kabla ya hapo Serikali ilikuwa haina hili fungu la 18 Percent.

Soma Pia: Kodi za Mapato: Kabla hatujawaza kuzidi kukamuana, tuangalie kuziba Pakacha
 
Hallooo. They cant hear you unfortunately
Ina maana hata wananchi nao hawasikii ? Nina uhakika labda wengi hatujaelewa connection ya makusanyo na kwanini kuna makusanyo, sababu nina uhakika hiki kibano cha kitaa ni wengi kinawakumba.

Kwahio tujiulize iwapo zamani wakati makusanyo yalikuwa machache / madogo na serikali ilitoa huduma zaidi, iweje leo huduma zimepungua (per unit) alafu makato / kodi zimeongezeka (per unit). Ni wapi Pakacha linavuja?
 
Wananchi uwa wanasikia na wanaijibu serikali kwa mgomo baridi wanarudi mezani kurekebisha . Niliwahi kukuta mgomo wa guest house na Hotel baada ya halmashauri kuongeza fedha na ndo njia imekuwa ikitumika ingawa inawaumiza wananchi
 
Wananchi uwa wanasikia na wanaijibu serikali kwa mgomo baridi wanarudi mezani kurekebisha . Niliwahi kukuta mgomo wa guest house na Hotel baada ya halmashauri kuongeza fedha na ndo njia imekuwa ikitumika ingawa inawaumiza wananchi
Kitaa ndio balaa kuanzia FIRE, Service Levy, Taka zote hizo mtu unalipia; Leseni; TRA Kodi na bado hapo kila hatua mzigo unapigwa VAT, Ndio maana biashara kitaa zinakufa kila leo, mbaya zaidi Serikali kuajiri haiwezi tena na watu kitaa wanaojitahidi kuajiri wanawakamua bila hata kuwapa lishe.
 
💯✔️
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…