Iwe sharti wanaume kuhamisha mali kwa watoto wa mwanzo kabla ya kuoa mke mwingine ili kuepusha dhuluma kwenye urithi baada ya kufariki

Iwe sharti wanaume kuhamisha mali kwa watoto wa mwanzo kabla ya kuoa mke mwingine ili kuepusha dhuluma kwenye urithi baada ya kufariki

Haki ya mtoto kurithi mali ya marehemu baba atoe wosia baba yake, Hawa watoto wanaosubiri wazazi wafe ili warithi mali na hawafanyi bidii yoyote ya kujijengea maisha wana haki IPI. Inabidi serikali ISAIDUE IWEKE WAZI VIJANA UMRI MIAKA 22 NA KUENDELEA WAJITEGEMEE. Wafanye kazi wasingoje PENSION ya wazazi waendelee KUILA. Watoto wa sasa unawakuta hawana kazi wanazunguka tu. Wazee walitoka kwa wazazi wengine kwa kusoma na wengine kufanya kazi mbalimbali na biashara ndio wakafikia hali waliyo nayo. Sasa wengi hawa hawataki kuhangaika wapo bado wanaangalia wazazi wawasaidie hata wakiwa na UMRI ZAIDI YA MIAKA 30. HII SIO SAWASAWA. Taifa linahitaji litoe mwongozo na kufuatilia NGUVUKAZI HII INAYOPOTEA NA KUTOCHANGIA UKUAJI WA TAIFA. SIO BABA YAKE TU ANAYEPATA HASARA NA TAIFA PIA
 
Nadhani ni wakati muafaka wa washua kujifunza kugawa mali zao kabla hawajadedi ili kuzuia vurugu.

Pia suala la pre-nup n muhim katika ndoa hasa hasa za uzeeni, maana hapo bi mdogo anaingia ndani akiwa anajua kbsa atakachoondoka nacho.

Sema kibongo bongo umwinyi mwingi! Wazee vichwa ngumu
Lyatonga Mrema anao nadhani next month, anasema ana mtoto mbichi mweupe.😄😄
 
Urithi uandikwe na kifanyike kikao kila mtu a ajue, kama kupinga, pinga wakati mwenye mali yu hai. Isiwe Siri.
Wosia unaandikwa kwa ballister, kabidhi wasii au kwa viongozi wakubwa wa kiroho kama familia ni ya wacha Mungu na si vinginevyo
 
Kwa hio hii ndio sababu ya Mama wa kambo kujirithisha mali zote na kuwaacha watoto wa mwanzo wasipate chao, hebu peleka ujinga wako pembeni wewe.

Alafu kuna kitu kinaitwa generational wealth, nakushauri ufatilie hilo

What ever the case, hiki sio kisingizio cha watoto wa mwanzo kunyimwa haki yao ya urithi
Hivi kwanini uliamua kunitukana aisee, bado nasoma na narudia tena sioni hata kwanini uliamua mimi ni mjinga

Sasa kwa jinsi uzi wako unavyokwenda, subiri hadi page 5 kisha soma comments zote za watu alafu ndani ya moyo wako kwa dhati kabisa pima mimi na wewe nani mjinga.
 
Lyatonga Mrema anao nadhani next month, anasema ana mtoto mbichi mweupe.😄😄
Taikon amesema dunia inaingia equinox ambapo masika yataanza. Sasa ile baridi ya kiraracha huko nafkr mshua kapiga hesab akaona hapa mifupa itauma, subr nitafute kajoto kidogo
 
Haki ya mtoto kurithi mali ya marehemu baba atoe wosia baba yake, Hawa watoto wanaosubiri wazazi wafe ili warithi mali na hawafanyi bidii yoyote ya kujijengea maisha wana haki IPI. Inabidi serikali ISAIDUE IWEKE WAZI VIJANA UMRI MIAKA 22 NA KUENDELEA WAJITEGEMEE. Wafanye kazi wasingoje PENSION ya wazazi waendelee KUILA. Watoto wa sasa unawakuta hawana kazi wanazunguka tu. Wazee walitoka kwa wazazi wengine kwa kusoma na wengine kufanya kazi mbalimbali na biashara ndio wakafikia hali waliyo nayo. Sasa wengi hawa hawataki kuhangaika wapo bado wanaangalia wazazi wawasaidie hata wakiwa na UMRI ZAIDI YA MIAKA 30. HII SIO SAWASAWA. Taifa linahitaji litoe mwongozo na kufuatilia NGUVUKAZI HII INAYOPOTEA NA KUTOCHANGIA UKUAJI WA TAIFA. SIO BABA YAKE TU ANAYEPATA HASARA NA TAIFA PIA
Unapuyanga tu na kupotosha jamii, haki ya mtoto wako au watoto wako kurithi ni haki ya kuzaliwa hakuna mtu au chombo chochote kinachoweza kukunyang'anya.

Urithi hata mama yako mzazi anaweza kupata inategemea na mazingira halisi kila familia au msiba kuna mazingira yasiyofanana.

Issue ya watoto wa sasa kuwa tegemezi ni janga la kitaifa zaidi na si kwamba ni wazembe.

Mimi ninakumbuka wakati tupo shule nafasi za kwenda jeshini na Polisi zilikuwa zinatangazwa mashuleni, na maeneo ya viwanda Dar kulikuwa magetini nje kuna black zimeandikwa nafasi za kazi zipo, ila leo imekuwa kinyume chake.

Zamani kuzaa watoto ilikuwa ni faraja na ni utajiri pia lakini wanaume tumekuwa kama mahanisi tunaogopa kuzaa watoto wengi kwa sababu ya gharama za kutunza familia hasa shule zimekuwa juu sana.

Zamani jukumu la kusomesha lilikuwa ni jukumu la serikali na madaftari tulipewa bure.

Ukiwasimanga kizazi kipya bila kujuwa kiini cha tatizo utakuwa hutendi haki.
 
HAKUNA CHOMBO CHOCHOTE KINAWEZA KUKUAMRISHA KUMRITHISHA MTOTO. Je nikiuza mali yangu nikaamua kukaa ktk nyumba za kupanga atarithi nini? Mtoto akifikisha miaka 18 anatakiwa ajijue ni wajibu wake KUJITEGEMEA LABDA KAMA ANAENDELEA NA MASOMO. Lakini miaka 30 a asubiria nini? NINA HAKI YA KUUZA MALI YANGU KWA MANUFAA YANGU HASA NINAVYOKUWA MZEE. Mfano nauza nyumba ya mjini naenda shamba kwenye maisha rahisi huyo mtoto atazuia?
 
Wazee wa kiswahili hawanaga tamaduni
Ya kufanya hivyo

Ova
 
Siku vijana mkijua kuwa mali za baba yako sio zako na unajukumu la kutafuta zako dunia itakuwa sehemu salama sana.

Mtajifunza kuwa watafutaji.

Baba amehangaika kutafuta mali mwacheni aamue yeye atampa nani urithi wake.

Vijana wengi huwa mkiwa wakubwa mnaungana na mama kumnyanyapaa baba, anakuwa mnyonge sana katika mji wake.

Kama binadamu anatafuta faraja mahali akipata mtu anaemjali anahamishia mapenzi yake huko, siku akifa mnaanza nongwa.

Si mliaminishwa na mama kuwa baba ni mbaya mkamtenga?

Hakuna na hayupo baba ambae ana mapenzi na upendo kwa familia yake akifa akaacha kuwarithisha mali!
Kuna watoto wanawadharau baba zao na wakati mwengine hata kuwatusi .
Kutegemea baba huyu atakuachia urithi ni kujidanganya.
 
Binafsi naamini ni busara kufa nikiwa nimewaachia watoto Mali.

Sioni haja kwa nini watoto waje kutanga tanga baada ya Kifo changu ingali nilikuwa na nafasi ya kuwaachia kitu flani
Watoto wanatakiwa wajitafutie, wewe ni kuwawezesha TU, huna jukumu la kuwaachia Mali, ni upendo TU!!
 
Imani yangu inanielekeza KUACHA URITHI kwa Watoto kama HALI inaruhusu!
Watoto wanatakiwa wajitafutie, wewe ni kuwawezesha TU, huna jukumu la kuwaachia Mali, ni upendo TU!!
 
Haki ya mtoto kurithi mali ya marehemu baba atoe wosia baba yake, Hawa watoto wanaosubiri wazazi wafe ili warithi mali na hawafanyi bidii yoyote ya kujijengea maisha wana haki IPI. Inabidi serikali ISAIDUE IWEKE WAZI VIJANA UMRI MIAKA 22 NA KUENDELEA WAJITEGEMEE. Wafanye kazi wasingoje PENSION ya wazazi waendelee KUILA. Watoto wa sasa unawakuta hawana kazi wanazunguka tu. Wazee walitoka kwa wazazi wengine kwa kusoma na wengine kufanya kazi mbalimbali na biashara ndio wakafikia hali waliyo nayo. Sasa wengi hawa hawataki kuhangaika wapo bado wanaangalia wazazi wawasaidie hata wakiwa na UMRI ZAIDI YA MIAKA 30. HII SIO SAWASAWA. Taifa linahitaji litoe mwongozo na kufuatilia NGUVUKAZI HII INAYOPOTEA NA KUTOCHANGIA UKUAJI WA TAIFA. SIO BABA YAKE TU ANAYEPATA HASARA NA TAIFA PIA
Umeongea sukari tupu, hiki ndicho hasa ninachosema humu. Subiri mtu afariki naturally, then Urithi usomwe, mwenye kupewa apewe, ila sio kushinikiza upewe urithi mtu yuko hai, au kuombea mtu afe haraka ili urithi mali, ni ujinga kabisa huo..
 
Binafsi nimeona kabla mwanaume hajaoa mwanamke mwengine (hasa hawa wazee wanao oa mabinti) , ingependeza haya mambo ya urithi yawe wazi ili kuepusha shari huko mbele, hii itakuwa kama bima ya kuwakinga watoto wa mwanzo kudhulumiwa urithi wao.

Siku hizi pia kumekua na trend ya wazee wanaoamua kuoa mabinti wadogo wakidhani wamepata kumbe wao ndio wamepatikana, binti anakua amehapiga hesabu zake anajua kabisa huyu mzee ni tajiri na havuki miaka 10 kwisha habari, Hapa binti atamzuzuzua kwa mapenzi moto moto huyo mzee mpaka mzee anajikuta anatoa mali zote, mzee akiwa mgumu basi anapigwa juju na malimbwata ya kumhamisha akili kushoto ili ahamishe mali kwa huyo binti.

nadhani kuwe na sheria za kuwalinda watoto wa mwanzo, kama baba anataka kuoa ni sawa haina shida lakini alazimishwe kuwajibika linapokuja swala la watoto wake wa mwanzo

Mifano ipo mingi sana ila hii ni michache.

1. Watoto wa marehemu Mengi wa mwanzo walivyotaka kunyimwa urithi, urithi karibu wote ungeenda kwa mama yao wa kambo, ilibidi wapambane sana kupata haki yao.

2. Watoto wa Marehemu Likwelile, ambao sasa wanapitia msoto, Mama yao wa kambo ni Vicky Kamata ambae kajihamishia uriithi huku watoto wa mwanzo wakiwa hoi bin taaban.

3. Watoto wa Marehemu Kimambi nao walipitia huu msoto, ilibidi wafike huko mahakamani wayamalize ila bila hivyo, mama wa kambo alikuwa anazoa kila kitu.

4. Nakumbuka mwenzetu tuliekuwa tunasomanae chuoni alikatisha masomo yake mwaka wa pili baada ya baba yake kufariki kwa sababu mali zote zilienda kwa mama yao wa kambo ambae aliacha hata kumlipia ada na kumpa hela za matunzo.

5. Mzee Mrema, pongezi kwako, nimeona habari unakaribia kuoa binti lakini jitahadhari please.

Urithi ni haki ya watoto, haki ya mtu ni haki yake haijarishi umri, Hata kama mtoto wa mwanzo anatembelea mkongojo na mtoto mwengine anatambaa, wote wana haki ya urithi wa mali za baba yao.
Kuna mambo mengi ya kuibadili kwenye sheria ya mirathi, pia nadhani ni muda muafaka kuangalia prenuptial agreement kwenye hizi marriages ndio itasaidia kwamba mnakubaliana kuoana Ila hatarithi Mali zako Wala wewe kurithi zake na hapa ndio utaona Hawa wanapjiita strong women Kama watakubali kuolewa na vizee.

Pia Kuna masuala ya Mali ambazo mwanaume amekutwa nazo kabla ya ndoa ni vema iangaliwe upya maana tumekubali kuwepo usawa sasa isiwe urithi ni kwa mwanamke tu na wao siku hizi Wana vipato na wamesoma Sasa mambo yawe sawa tusiumize watu Ila inapokuja ishu ya pesa au Mirathi mwanamke anajifanya ni dhaifu iila mengine anajifanya anaweza.

Kimsingi hata masuala ya custody ya watoto tunawanyima haki watoto kukaa na baba zao simply wanawake wanatumia nafasi ya watoto Kama kumuadhibu mwanaumena wanajikuta wanamnyima haki mtoto. Baba anaweza kuwa mtunzaji mzuri sana wa watoto Ila unashangaa wakiachana anageuka kuambiwa hatunzi watoto lakini ukichunguza shida ipo kwa mwanamke kwanza kuhisi yeye ndio mwenye haki pekee ya kukaa na watoto, nadhani ishu ya co-parenting iwepo kwenye sheria iruhusu wazazi wawili waliotengana kutunza watoto pamoja.

Mama afike pahala aruhusu mtoto na kumhimiza mtoto kumpigia simu babake sio tu kuacha mtoto ajiamulie lazima ahimizwe kumpigia kumsalimia na kumtembelea babake au mamake.

There's a lot ya kuwa amended sababu sheria yenyewe ni ya siku nyingi, mambo mengi yamebadilika sana, Hawa wanawake sio wa enzi Ile, wa Sasa wanaenda shule, wanaajiriwa posts kubwa na mishahara mikubwa sana why Mali ya mwanaume pakee ndio iwe subjected kwenye Mirathi????

Something is not adding up.
 
Umeongea sukari tupu, hiki ndicho hasa ninachosema humu. Subiri mtu afariki naturally, then Urithi usomwe, mwenye kupewa apewe, ila sio kushinikiza upewe urithi mtu yuko hai, au kuombea mtu afe haraka ili urithi mali, ni ujinga kabisa huo..
Sheria ya urithi pia inaruhusu mtu kugawa mali kama zawadi kwa ampendae kabla hajafa. Hivyo kama baba hataki kumpa
mtoto urithi anaweza kugawa mali kama zawadi pia.
Ni vyema watoto waishi vizuri na wazazi wao (baba na mama) ili siku zao ziongezeke na pia wapate mgao, sio kuingia
bifu na baba huku wakikodolea macho mali...itakula kwao.
 
Huuu ushauri wako lazima niufanyie kazi, lazima wangu wapate haki yao Tena 80% inayobaki ndio mama yao wa kambo ili nikilala asitokee wa kuwabuguzi.
Hata mama yao ya kuwazaa. Mpe 10-30%.

Watoto ndiyo kila kitu pale ukitoweka.

Utanishukuru.
 
Back
Top Bottom