Iwe sharti wanaume kuhamisha mali kwa watoto wa mwanzo kabla ya kuoa mke mwingine ili kuepusha dhuluma kwenye urithi baada ya kufariki

Ishu kuu ni hawa mama wa kambo kuchota kila kitu huku, watoto wa mwanzo wanaambulia patupu...Je ni haki hawa mama wa kambo kuzoa kila kitu?

Binafsi nimeona kabla mwanaume hajaoa mwanamke mwengine (hasa hawa wazee wanao oa mabinti) , ingependeza haya mambo ya urithi yawe wazi ili kuepusha shari huko mbele, hii itakuwa kama bima ya kuwakinga watoto wa mwanzo kudhulumiwa urithi wao.

Siku hizi pia kumekua na trend ya wazee wanaoamua kuoa mabinti wadogo wakidhani wamepata kumbe wao ndio wamepatikana, binti anakua amehapiga hesabu zake anajua kabisa huyu mzee ni tajiri na havuki miaka 10 kwisha habari, Hapa binti atamzuzuzua kwa mapenzi moto moto huyo mzee mpaka mzee anajikuta anatoa mali zote, mzee akiwa mgumu basi anapigwa juju na malimbwata ya kumhamisha akili kushoto ili ahamishe mali kwa huyo binti.

nadhani kuwe na sheria za kuwalinda watoto wa mwanzo, kama baba anataka kuoa ni sawa haina shida lakini alazimishwe kuwajibika linapokuja swala la watoto wake wa mwanzo

Mifano ipo mingi sana ila hii ni michache.

1. Watoto wa marehemu Mengi wa mwanzo walivyotaka kunyimwa urithi, urithi karibu wote ungeenda kwa mama yao wa kambo, ilibidi wapambane sana kupata haki yao.

2. Watoto wa Marehemu Likwelile, ambao sasa wanapitia msoto, Mama yao wa kambo ni Vicky Kamata ambae kajihamishia uriithi huku watoto wa mwanzo wakiwa hoi bin taaban.

3. Watoto wa Marehemu Kimambi nao walipitia huu msoto, ilibidi wafike huko mahakamani wayamalize ila bila hivyo, mama wa kambo alikuwa anazoa kila kitu.

4. Nakumbuka mwenzetu tuliekuwa tunasomanae chuoni alikatisha masomo yake mwaka wa pili baada ya baba yake kufariki kwa sababu mali zote zilienda kwa mama yao wa kambo ambae aliacha hata kumlipia ada na kumpa hela za matunzo.

5. Mzee Mrema, pongezi kwako, nimeona habari unakaribia kuoa binti lakini jitahadhari please.

Urithi ni haki ya watoto, haki ya mtu ni haki yake haijarishi umri, Hata kama mtoto wa mwanzo anatembelea mkongojo na mtoto mwengine anatambaa, wote wana haki ya urithi wa mali za baba yao.
Umemsahau naKanali Metili
 
Unakuta mamtu mazima nayo yanagombania mali za urithi na watoto wadogo........hadi mnakuwa watu wazima mzee ameshawapa michongo yote au mmeshatafuta dili zenu, mali za urithi achieni watoto wadogo au zisimamieni kwa niaba yao.
Nonsense
 
Kimsingi mtu aliye hai hana mirathi na alithiwi.

Busara tu kwa hiyari yake akiamuwa kugawa mali zake kwa watoto akiwa hai hilo ni jambo jema zaidi.

Mfano Bakhresa ile kampuni ya Omar packaging amempa mwanae Omar Bakhresa hivyo yani.
Habar za tajir kazitafute kwa masikini...utazipata tuu
 
Aliyemaliza chuo siyo mtoto tena, atafute vyake, mie na mamake wa kufikia tutajisort wenyewe!

Mali kama ni za kampuni basi zitaendeshwa kwa taratibu za kikampuni!

Ila wazee wanafeli SANA

Pius Ng'wandu naye kwenye list
 
Tatizo baba anakuwaga mkali Sijui hivyo vimama vya kambo vinawapa nn hawa wazee!
 
Ukajiroga ukaandika urithi kwenye kikao kama hivyo na kila mnufaika akajua kwamba yeye anachukua nini, i assure you, humalizi mwaka utaondoka hapa duniani kwa namna ya kutatanisha, maana wataona kama wanachekewa kupewa urithi wao kwa kutokufa kwako
Kawaida warithi wanajulikana, mke na watoto( sheria) ila nani achukue nini. Umeona watoto wa yule mama aliekuwa na kanisa wanavyo dhalilisha,
 
Kama wanajulikana sasa unataka uite kikao cha kugawa urithi cha kazi gani sasa? Suala la nani achukue nini liwe siri yako, sio uite kikao na kuwatamanisha juu ya kile unachoahidi kuwapa, mwishowe waone unawachelewa kwa kutokufa kwako
 
Vtu vingne aviitaji ata sheria kuna ujinga na ulimbukeni wa wanaume
Umetengana na mkeo kakuachia watoto umeamua kuoa mke mwingne sasa unashindwaje kutambua kua utakua na watoto wa wamama wawili tofauti ukapanga utaratbu mzuri w mali
Kuna kitu inaitwa ukewenza(mkemwenza) huu hauishiagi kwa manawake tuu hii inaendaga ad kwa watoto pia
Mambo mengne ni ujinga na ulimbukeni tu wa sisi wanaume
 
Ishu kuu ni hawa mama wa kambo kuchota kila kitu huku, watoto wa mwanzo wanaambulia patupu...Je ni haki hawa mama wa kambo kuzoa kila kitu?

Binafsi nimeona kabla mwanaume hajaoa mwanamke mwengine (hasa hawa wazee wanao oa mabinti) , ingependeza haya mambo ya urithi yawe wazi ili kuepusha shari huko mbele, hii itakuwa kama bima ya kuwakinga watoto wa mwanzo kudhulumiwa urithi wao.

Siku hizi pia kumekua na trend ya wazee wanaoamua kuoa mabinti wadogo wakidhani wamepata kumbe wao ndio wamepatikana, binti anakua amehapiga hesabu zake anajua kabisa huyu mzee ni tajiri na havuki miaka 10 kwisha habari, Hapa binti atamzuzuzua kwa mapenzi moto moto huyo mzee mpaka mzee anajikuta anatoa mali zote, mzee akiwa mgumu basi anapigwa juju na malimbwata ya kumhamisha akili kushoto ili ahamishe mali kwa huyo binti.

nadhani kuwe na sheria za kuwalinda watoto wa mwanzo, kama baba anataka kuoa ni sawa haina shida lakini alazimishwe kuwajibika linapokuja swala la watoto wake wa mwanzo

Mifano ipo mingi sana ila hii ni michache.

1. Watoto wa marehemu Mengi wa mwanzo walivyotaka kunyimwa urithi, urithi karibu wote ungeenda kwa mama yao wa kambo, ilibidi wapambane sana kupata haki yao.

2. Watoto wa Marehemu Likwelile, ambao sasa wanapitia msoto, Mama yao wa kambo ni Vicky Kamata ambae kajihamishia uriithi huku watoto wa mwanzo wakiwa hoi bin taaban.

3. Watoto wa Marehemu Kimambi nao walipitia huu msoto, ilibidi wafike huko mahakamani wayamalize ila bila hivyo, mama wa kambo alikuwa anazoa kila kitu.

4. Nakumbuka mwenzetu tuliekuwa tunasomanae chuoni alikatisha masomo yake mwaka wa pili baada ya baba yake kufariki kwa sababu mali zote zilienda kwa mama yao wa kambo ambae aliacha hata kumlipia ada na kumpa hela za matunzo.

5. Mzee Mrema, pongezi kwako, nimeona habari unakaribia kuoa binti lakini jitahadhari please.

Urithi ni haki ya watoto, haki ya mtu ni haki yake haijarishi umri, Hata kama mtoto wa mwanzo anatembelea mkongojo na mtoto mwengine anatambaa, wote wana haki ya urithi wa mali za baba yao.
Kama huyu mzee
IMG-20220321-WA0040.jpg
 
Kama wanajulikana sasa unataka uite kikao cha kugawa urithi cha kazi gani sasa? Suala la nani achukue nini liwe siri yako, sio uite kikao na kuwatamanisha juu ya kile unachoahidi kuwapa, mwishowe waone unawachelewa kwa kutokufa kwako
Bila kuwa wazi nani anachukua nini, ndio ugomvi unatokea kama watoto wA askofu lwakatare
 
Nimesoma comment za wadau nimetoka na conclusion/impression hizi.

Familia zetu zitachukua muda mrefu sana kuwa na mwendelezo wa kibiashara/uchumi kutoka kizazi kimoja kwenda kingine . Inaonekana kila generation inatakiwa iteseke from scratch .

Familia nyingi hazina utaratibu wa kuongea juu ya mipango ya familia kiujumla. Hii inapelekea mkuu wa familia kupambana mwenyewe akihisi anaipambania familia ...huku nyumbani watoto na mama yao some times hawaelewi mzee ana-vision gani hivyo huunda side B ndani ya familia ...So mzee akifariki ...hakuna anayejua kwa undani uendeshaji wa kazi za mzee. Means hata kama kuna mali zitaisha then watoto nao watalazimika kuanzia chini.

NB: Sio lazima kila kizazi kianzie from scratch ..."hustling is not for everyone" ukiweza kutafuta mali tujitahidi na kuweka succesion plan.
 
Back
Top Bottom