Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
J. EDGAR HOOVER MKURUGENZI WA FBI NA "FILE" LA SIRI KUBWA
J. Edgar Hoover ndiye Mkurugenzi wa kwanza wa FBI na alikikalia kiti kwa nusu karne.
Lilikuwa jitu la mikasa likitisha na kuogopewa na kila mtu hadi maraisi wa Marekani wakimkalia mbali.
Alikuwa hawapendi akina Kennedy na akina Kennedy walikuwa hawampendi pia lakini wamfanye nini kwao alikuwa kidonda ndugu.
Robert Kennedy alikuwa Mwanasheria Mkuu wa serikali wakati kaka yake ndiye rais wa Marekani.
Hoover akapata fununu kuwa Robert ana mipango ya kumng'oa kwenye kiti chake.
Hoover akachukua file moja yaani jalada akampelekea Robert Kennedy akamwambia, "Soma jalada hilo na wala usipate tabu kunirudishia ukimaliza baki nalo mimi nina nakala."
Robert haraka sana alisitisha mpango wake wa kumng'oa Edgar Hoover kwenye kiti chake.
Siku moja Hoover yuko ofisini kwake anazungumza na rafiki yake mmoja akampa jalada akamwambia alisome.
Alipomaliza kulisoma akamtahadharisha vikali sana.
Akamwambia, "Eee bwana we hayo uliyosoma ala ala tafadhali usije ukamweleza mtu yeyote."
Edgar Hoover akalichukua lile file akaenda kuliweka kisha akarudia kumpa rafiki yake indhari kuhusu kutunza ile siri ndani ya lile file.
Yule jamaa akamgeukia Edgar Hoover mabega juu na mikono kamwelekezea Hoover viganja kaviweka kama anataka kupokea kitu uso umechukua sura ya mshangao mkubwa.
"File! akatamka kwa mshangao mkubwa anamtazama Hoover usoni jicho kwa jicho.
"Edgar, file gani hilo unalolizungumza?"
Kwa Kiingereza inakaa vyema.
Jamaa alisema, "File, what file?"
Edgar Hoover alibakia kucheka.
Kidagaa kabakianacho mwenyewe mfukoni.
Tuna mengi ya kujifunza kutoka kwa hawa jamaa.