Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
- Thread starter
- #21
Uzalendo...Mzee wetu leo nikupongeze kwa kutoandika simulizi za Waislamu na Uislamu
Kwani unakereka kusoma historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika na kuona mchango wa masheikh akina Sheikh Hassan bin Ameir, Sheikh Yusuf Badi, Sheikh Suleiman Takadir, Sheikh Rashid Sembe kwa kuwataja wachache?
Majina haya wewe yanakuudhi kuwamo kwenye historia ya TANU?
Unataka niamini majina haya yalifutwa kwenye historia ya uhuru kwa kuwa hamkuyapenda?
Ungekasirika kama Kadinali Rugambwa au Pengo wangekuwa na historia ya kupigania uhuru bega kwa bega na Julius Nyerere?