Jabali kuu la TFF kuumbuliwa na PISIBIBI hivi punde

Jabali kuu la TFF kuumbuliwa na PISIBIBI hivi punde

Kwa NYETI nilizozidaka hivi punde na tena zenye chembe chembe za uhakika wake kwa 99.9999% ni kwamba pisibibi wameshamaliza kazi yao na ndani ya hizo saa 240 nchi ya Tanzania itasimama kwa TAARIFA ambayo kwa sisi WAPIGANIA HAKI na UKWELI katika medani ya Michezo hasa mpira wa miguu naamini tutaifurahia mno ila kwa JABALI lao mwenyewe pamoja na TEAM yake najua wataumia sana.

NYETI zinazidi kusema kuwa tayari sasa JABALI anaandaliwa gereza lake MAALUM ili aende akapumzishe AKILI zake huko na kujutia kitendo kibaya cha upangaji wa matokeo alichokifanya kwa TAMAA zake.

NYETI hizo bado zinaendelea kusema kuwa japokuwa leo JABALI limeendelea tena kufanya USANII wake uliozoeleka wa KUWAHAMISHA Watu kutoka Ofisi moja kwenda nyingine ili KUKWEPESHA ushahidi juu ya sakata zima la Tabora na Kigoma lakini tayari ameshashikwa pabaya.

Ukweli ni kwamba wenye dhamana ya kufanya uchunguzi " pisibibi " wameshamaliza kazi yao na sasa wanasubiri tu mambo kadha wa kadha tu ya Kiofisi kisha waitishe press conference WATEME CHECHE.

Bwana Wallace Karia kuanzia sasa anza kupanga SAFU yako ya kumaliza miaka yenu iliyobaki kwani JABALI hutakuwa nalo tena hapo mitaa ya karume na mchikichini muda wowote kuanzia sasa.

Nimalizie tu kwa kutoa ombi kwa Mheshimiwa Waziri husika kuwa wale jamaa wawili ambao sauti zao ndizo zimesikika mno naomba jitahidi kadri uwezavyo kukamata pasi zao za kusafiria kwani kwa NYETI nilizozipata wao tayari wameshajua kuwa na wao wameingia " nyavuni " kwa pisibibi hivyo sasa wanajiandaa kukimbia nchi kwenda kujificha.

Hongereni sana pisibibi na hakika sasa ndiyo nimeanza kuona UELEDI wenu katika kutenda kazi na nawatakieni kila la kheri katika kutangaza uozo wa JABALI huku mkimuelekeza gereza la kwenda kupumzika ili iwe fundisho kwa Watendaji wengine wenye tabia kama zake.

Furaha yangu ni kubwa ni kwamba nilichokipigania KIMEZAA MATUNDA hivyo najiona ni MSHINDI Mimi na wale wenzangu wote tulioguswa na kitendo kile kibaya cha UPANGWAJI MATOKEO MICHEZONI ambacho kiukweli ndicho kimedidimiza kabisa Soka letu la Tanzania kupelekea kila siku tunapiga " mark time " tu huku wenye mipango, ueledi, mikakati, mbinu na uthubutu wakitupita.
Hujisikii vibaya mwana jf mwenzetu kwenda lupango??!
 
Mpira umekua kichaka cha kukimbilia kutafuta uongozi hasa ukizingatia hata kupiga danadana tano MTU hawezi lakini ndio kiongozi anaongoza soka letu.kwahiyo unategemea nn kama sio madudu.
 
Back
Top Bottom