Annuity
JF-Expert Member
- Dec 17, 2013
- 338
- 198
Kwa Tanzania watu wanasema ama kwa kumaanisha au kwa kutania kuwa fani iliyokosa mwelekeo na yenye watu waliokosa la kufanya na maskini ni ualimu. Lakini Jack Ma Yun maarufu kama Jack Ma kitaaluma ni mwalimu wa kiingereza ambaye ni mwanzilishi na mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Alibaba inayojihusisha na biashara za kuuza na kununua bidhaa tandaoni (E-commerce), Jack kwa sasa ndio mtu tajiri zaidi chini China ambapo kampuni yake imefanya maajabu kwenye soko la hisa la New York Exchange nchini Marekani kwenye siku yake ya kwanza ya kuingiza hisa sokoni Initial Public Offering (IPO) ambapo imekuwa na thamani ya $21.8B, ambapo kwa sasa kampuni ya mwalimu huyo wa kiingereza ina thamani ya dola bilioni 21.8 ($21.8B) kama nilivyosema na ambayo ni sawa na thamani ya makampuni makubwa kama Ebay, Amazon na Google kwa pamoja.
Jack mwenye umri wa miaka 50 ambaye ‘kibongobongo' watu wangeweza sema kuwa ni ‘kilaza' baada ya kushindwa mtihani wake mara mbili, alijiunga na chuo cha ualimu cha Hangzhou Teacher's Institute na kuhitimu shahada ya ualimu katika somo la kiingereza, na alianzisha kampuni yake hiyo mwaka 1999 na sasa ana kampuni yenye thamani ya $21.8B, mwenyewe Jack akimiliki 7.5% ya hisa inayomfanya kuweka kibindoni dola bilioni 6 ($6B) na kumfanya kuwa mtu tajiri kuliko wote nchini china na pia kuingia rasmi kwenye list ya watu 20 matajiri zaidi duniani na kuwa mwalimu tajiri kuliko walimu wote unawafahamu duniani huku kwenye timu hiyo ya mabilionea ikiongozwa na ‘Baba Lao' Bill William Gates au Bill Gates. Jack Ma kwa sasa ni kionozi mkubwa wa biashara duniani mwenye degree ya ualimu.
My take: You can be what you want to be, what it takes is desire to success and determination.