Money Stunna
JF-Expert Member
- Aug 9, 2011
- 13,053
- 6,304
Baada ya kutoonekana katika pozi za kimahaba kwa muda mrefu, kwa mara ya kwanza, staa wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper Massawe ‘Gambe' amenaswa ‘live' na mwanaume anayedaiwa kuwa ni mume wa mtu,
Kwa muda mrefu Wolper amekuwa makini na picha zake za kimahaba tangu alipokuwa akitoka kimapenzi na mfanyabiashara maarufu jijini Dar, Abdallah Mtoro ‘Dallas'.
Awali, chanzo makini kilipenyeza habari kuwa kuna mawasiliano yamenaswa ‘kimafia' ambayo yalitoka kwa Wolper kwenda kwa rafiki yake yakionesha anabanjuka na mwanaume huyo wa mtu aliyejulikana kwa jina moja la Gee.
Chanzo hicho kilikwenda mbali zaidi kwa kudai kwamba licha ya kuwa ni mume wa mtu, mwanaume huyo ni bwana wa rafiki yake kutokana na mawasiliano hayo yalivyosomeka.
"Mashabiki kila siku huwa wanamtetea Wolper na skendo zake, sasa nakutumia picha pamoja na ‘chating' zake alizokuwa akichati na shoga yake kuhusiana na jamaa huyo," kilisema chanzo hicho.
