Jackson Group na wadau wengine tunaomba tumuandalie kijana wetu Mwakinyo mapambano haya

Jackson Group na wadau wengine tunaomba tumuandalie kijana wetu Mwakinyo mapambano haya

Airmanula

JF-Expert Member
Joined
Nov 30, 2016
Posts
3,527
Reaction score
5,762
Nitoe pongezi kwa wadau wa masumbwi nchini kwa kuendelea kutupa furaha tena sisi wapenda masumbwi nchini. Kwa kipindi fulani unaweza kudhani kua mchezo wa masumbwi kama vile ulikua umesahaulika kama si kutokua na amsha amsha tena.

Pongezi ziwafikie Jackson Group na wadau wengine ambao mnaendelea kutengeneza mazingira mazuri ya kuinua kwa kasi mchezo wa Boxing.

Naomba kutoa pendekezo embu tumuandalie kijana wetu Mwakinyo na wengine mapambano haya, tunaweza na najua inawezekana kabisa.

Kwa Mwakinyo si mbaya kama atapigana na hawa jamaa ambao ndio current champions katika uzito wake. Hapa naanza na picha ya kwanza Patrick Teixeira kutoka Brazil ambaye ni Bingwa WBO Super Welterweight, picha ya pili ni Jermell Charlo wa Marekani yeye ni Bingwa wa IBF, WBC, na WBA uzito wa Super Welterweight.

Hakuna kisichowezekana, embu wadau wa masumbwi tufanye mambo wanamasumbwi tufurahi.

Screenshot_20201115-173922_1.png
Screenshot_20201115-174014_1.png
 
Tatizo ranking alikuwa wa 62 kaporomoka mpaka 86, inabidi apambane sana hao machamp hawawezi kucheza na mtu wa chini sana labda apewe dau kubwa sana.
 
Tatizo ranking alikuwa wa 62 kaporomoka mpaka 86, inabidi apambane sana hao machamp hawawezi kucheza na mtu wa chini sana labda apewe dau kubwa sana.
Nahisi mwakinyo kuna sehemu aliteleza maana baada ya kumdunda sam alikuwa kwenye rank nzuri tu
 
Hujiulizi kwanini ranking imeshuka ..tatizo wabongo hamfanyi research, mnaona akipigana nao watamuumiza,
Anatakiwa apmbane na mabondia haswa watakampandisha ranking za kidunia katika uzito wake wa super welterweight
Watanzania tupendane lengo lako nini kwa kijana mwenzio?
 
Back
Top Bottom