TANZIA Jackson Makwetta (Mbunge na Waziri wa zamani) afariki dunia

TANZIA Jackson Makwetta (Mbunge na Waziri wa zamani) afariki dunia

Poleni sana wafiwa. R.I.P Makweta. Tutakukumbuka sana hasa kuhusu msimomo wako kuhusu elimu bora kwa watanzania.
 
Ni aliyekuwa mbunge wa huko Njombe na waziri katika serikali ya awamu ya kwanza na ya pili Mhe. Jackson Makwetta amefariki dunia jioni ya leo.

Alazwe pema peponi

Chanzo: Ndugu wa karibu na marehemu.

R.I.P Makweta... ULIYEANZISHA MAKWETA EXAMS... Ule Mtihani wa Formm II
 
Mwenyezi Mungu ampokee mzee J.Makweta ktk ufalme wake pia nawapa pole ndugu wa marehemu kwa msiba mzito uliowakuta hasa kwa kumpoteza kiongozi wa familia,rafiki na Kiongozi wa Taifa wa zamani kwa nafasi ya ubunge na uwaziri.Pia nawapa pole ndugu na jamaa kule Njombe kwa msiba huu mzito hasa kwa kumpoteza kiongozi aliyehudumu kwa zaidi ya miaka 25 kama mbunge hivyo kuwa sehemu ya maendeleo ya jimbo.Alale mahala pahala pema peponi J.M.Makweta!
 
Umetangulia Makweta,umetimiza safari yako duniani
 
Poleni sana wafiwa. R.I.P Makweta. Tutakukumbuka sana hasa kuhusu msimomo wako kuhusu elimu bora kwa watanzania.

Poleni familia, ndugu, jamaa na marafiki wa Jackson Makweta! Mungu aiweke roho yake mahali panapostahili! ila kuhusu msimamo wake elimu bora kwa watanzania hiyo ni sera ya chama chake! na kama alifanikiwa basi huna budi kumpongeza yeye na chama chake pia!

Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni!
 
Mwenyezi MUNGU Akulaze ulipojiandalia ukiwa hai.Amen
 
Kuwa kiongozi sio lelemama! kuna sifa nyingi zinazoonyesha uongozi bora! baadhi ya sifa hizo ni:

Elimu sahihi, uadilifu, bidii, ubunifu, usikivu, ushirikiano na uwezo wa kuwasiliana!

Bila shaka Jackson Makweta huenda alikuwa na baadhi ya sifa za kuwa kiongozi! jee, kuna mtu mwenye wasifu wa Jackson Makweta atuwekee hapa?
 
Mzee huyu alikuwa ni miongoni mwa viongozi wachache wa CCM waliotumikia taifa lao kwa uadilifu na kwa uzalendo wa hali ya juu, akiwa waziri wa serikali kwa miaka 25 mfululizo (1975 - 2000), lakini hakuna mahali alitumia vibaya madaraka yake kwani inasemekana kwamba hata nyumba ya kuishi nje kidogo ya jiji la Dar-es-salaam alijengewa na wanae kabla ya kustaafu na hata hivyo haikukamilika ipasavyo; na katika kipindi karibia chote cha ustaafu wake alikuwa anaishi kwao kijijini;

Lakini kwa vile serikali yetu ya CCM haijali watu kama hawa, msiba wake utaendeshwa kinafiki tu; Misiba yenye kupewa uzito ni ile ya viongozi wasiokuwa wazalendo ambao utashi wao unapimwa kwa utajiri wao; Lakini ipo siku yote haya yatabadilika;

Poleni wafiwa; Mwenyezi mungu amlaze mahali pema peponi Mzee wetu Makweta, Amen;
Umenikumbusha mengi sn. Makweta alifanya kazi nzuri akiwa waziri wa elimu, miaka ya 1980. Rip Makweta
 
Mzee Makweta ni wachache ndani ya CCM ambao ni wasafi, lakini CCM MAFISADI iliwaangamiza. Unafiki ndio utajitokeza chini wa Rais wa misiba JK
 
Hii hapa ni taarifa rasmi ya serikali.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI*

MHE. MAKWETTA AFARIKI DUNIA.

SERIKALI inasikitika kutangaza kifo cha Bw. Jackson Makwetta kilichotokea leo saa 11 jioni katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ya jijini Dar es Salaam ambako alikuwa amelazwa.*

Msiba uko nyumbani kwake Boko kwa Wagogo. Taarifa zaidi kuhusu mipango ya mazishi zitatolewa baadaye.*Bw. Makweta aliwahi kuwa Waziri katika wizara mbalimbali zikiwemo Ofisi ya Waziri Mkuu kama Waziri wa Nchi, Elimu, Kilimo na Utumishi.*

Pia amekuwa Mbunge kwa zaidi ya miaka 35.***

IMETOLEWA NA:OFISI YA WAZIRI MKUU,DODOMA.JUMAMOSI, NOVEMBA 17, 2012
 
Back
Top Bottom