Jacob Zuma akata rufaa kuhusu uamuzi wa kurejeshwa kwake jela

Jacob Zuma akata rufaa kuhusu uamuzi wa kurejeshwa kwake jela

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma ameiomba Mahakama ya Juu nchini humo kubatilisha uamuzi unaomtaka arejeshwe jela ili kutumikia kifungo cha miezi 15, hatua ambayo hapo awali ilisababisha maandamano na uporaji katika jimbo lake la KwaZulu Natal hadi mjini Johanesbourg.

Zuma mwenye umri wa miaka 80 aliachiliwa kutokana na sababu za kimatibabu, miezi miwili tu baada ya hukumu hiyo, kwa kosa la kuwapuuza wachunguzi wa kupambana na rushwa.

Mnamo mwezi Desemba, Mahakama Kuu ilibatilisha uamuzi wa kuachiliwa kwake, ikielezea uamuzi huo kuwa "kinyume cha sheria."

Zuma ambaye bado ana ushawishi katika chama tawala cha ANC, aliingia madarakani mwaka 2009 na kuondolewa miaka 9 baadaye huku muhula wake ukigubikwa na kashfa za ufisadi.
 
Back
Top Bottom