Jacob Zuma: Sioni haja ya kwenda jela kipindi hiki cha mlipuko wa COVID-19

Jacob Zuma: Sioni haja ya kwenda jela kipindi hiki cha mlipuko wa COVID-19

Sam Gidori

Senior Member
Joined
Sep 7, 2020
Posts
165
Reaction score
417
Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Jacob Zuma amesema hana haja tena ya kwenda jela baada ya Mahakama ya Kikatiba iliyotoa hukuku ya kifungo cha miezi 15 jela kukubali kusikiliza rufaa yake.

Akizungumza na waandishi wa habari nyumbani kwake siku ya Jumapili, Zuma amesema hakuna sheria inayomlenga Jacob Zuma pekee ambayo haitumiki kwa watu wengine.

Mkutano wa Zuma na waandishi wa habari unafuatia siku kadhaa za maandamano nje ya nyumba yake ambapo mamia ya wafuasi wake walikusanyika, wakivunja sheria zote za COVID-19, kutengeneza ‘uzio wa watu’ ili kuzuia kukamatwa kwake, ambapo alitakiwa kukamatwa usiku wa siku ya Jumapili.

Awali, Naibu Jaji Mkuu wa Afrika Kusini, Raymond Zondo, alisema Zuma lazima akumbane na mkono wa sheria vinginevyo kutakuwa na vurugu katika mahakama za nchini humo. Hata hivyo Zuma amemlaumu Zondo kwa kuwa na kinyongo binafsi na yeye, akisisitiza kutokuwa na hatia na kuwa mashtaka dhidi yake ni ya kutengenezwa.

Kesi ya Zuma itasikilizwa tena Julai 12. Wachambuzi wa sheria wanasema si rahisi kwa Zuma kukwepa kifungo cha gerezani, hata kama ni chini ya kifungo cha miezi 15 kama ilivyotangazwa awali.

1625465510263.png


More: Jacob Zuma: Supporters form 'human shield' to stop ex-president's arrest
 
Aende jela huyo boya, aache porojo.
 
Kama ameweza kwenda kukata rufaa huko Mahakamani kwanini hakwenda alipoitwa?yaani baada ya kusikia anatakiwa kukamatwa ndio anaanza harakati za Pimbi?
 
Back
Top Bottom