tweenty4seven
JF-Expert Member
- Sep 21, 2013
- 15,863
- 19,626
Na hicho ndicho kinamstahili % yake tena kwa kuzingatia huo muda alioishi na Marehemu! Watoto haki yao ipo hilo wala halina shida kabisa! Ila wale waliomwamndalia wosia Mungu anawaona,sio kwa kumtapeli Mjane,leo anacheza sebene peke yake mitandaoni wao wako kimyaa
Du mkuu we kweli una inside info. Ule usia umeandikwa kwa chuki sana. Kama kweli Jackline kafoji ule usia basi mahakamani uta back fire abaki akiimba crazy over you !!!Tunamfahamu R Mengi kuliko Jacline anavyo fikiri. Ule wosia hakuandika Mengi japo alisainishwa akiwa "senile'. Na ndiyo maana bi-bidada kasimamia hapo kuwa mumewe alidhalilishwa kwa madai ya akina Benjamin kuwa Mengi hakuwa sawasawa kiakili.
Jackline alikosea sana katika kufoji wosia kwa kuwatenga kina Regina na Abdiel. Angekuwa na akili angeweka clauses zinazowapa staja especially kwenye uangalizi wa wale mapacha just in case Mengi na Jack watakuwa wamekufa. Kwa ufinyu wa akili yake eti anamuweka dada yake. Makosa ya kijinga kabisa hayo. Mengi asingeweza kuandika hivyo
Unaongea kama vile huna ndugu, hovyoooo!! Kwa hiyo unataka kusema mke ndiye alikuwa akimpenda sana kuliko hao ambao wamesota nae tangu utotoni? Wewe naye ni walewale tu.Hakuna cha kupenda ndugu hapa, mume akifa ndio ndugu mnaanza kujifanya mna uchungu sana. Hapo hadi sahivi imeshakula kwao, hadi wanaanza kuweweseka eti wanamuomba wayasuluhishe , hahaahaha...ndugu ni mapepo
Sent using Jamii Forums mobile app
Kitu Karma hiyo mkuu.Laana atapata Jacky sio watoto mkuu...! Hapo kuna laana za Mke mkubwa na masikitiko ya watoto...! Tupeane 10yrs Jack km atakuwa na huo ukwasi anaoulilia...!
Labda unapaswa ufahamu hili, kilichopo mahakamani na kitachoamriwa ni mgogoro kuhusu uhalali wa wosia. Haya mambo mengine ya kuzuiwa kwenda makaburini, ati alikuwa na mahusiano mengine na jamaa fulani, alimpendea marehemu pesa tu n.k mahakama haiendi amua bali Jacqueline anapaswa ajibu kama ataona yafaa.Huyu si akae kimya aache mahakama ifanye kazi yake, yaani anajifanya ana uchungu na Mengi kuliko ndugu zake waliozaliwa tumbo moja, ukoo mmoja wanamjua nje ndani.
Huku naona kama anatafuta huruma na kuwapa faida wambeya.
Mkuu hebu fafanua kidogo hapa,maana sijakuelewa kwamba total ni 150%? (Mercy 50%,Mengi 50% na Nguma 50%) Au ulimaanisha Mercy 50% (Mengi na Nguma kwa pamoja walikuwa na 50%) ambayo inaleta 100%?
Otherwise mengine tuko pamoja kabisa,hakuna janja ya kuvuna asiponda huyu Mjane wa mwendokasi,asubiri haki yake inayomstahili na siyo hiyo ya wosia wa kitapeli aliouandaa!
Halafu usome hapo juu (#483) Frama akielezea kuhusu role ya mila kuhusu hii mambo. Naona umesahau kumuuliza scientific proof ya mila !!!