Jacqueline Mengi: Maneno ya kashfa na kumchafua mume wangu yamesemwa mahakamani, sikubali usuluhishi hadi yakafutwe

Jacqueline Mengi: Maneno ya kashfa na kumchafua mume wangu yamesemwa mahakamani, sikubali usuluhishi hadi yakafutwe

Telemundo yake itaisha mda sio mrefu,yetu masikio na macho
Na hicho ndicho kinamstahili % yake tena kwa kuzingatia huo muda alioishi na Marehemu! Watoto haki yao ipo hilo wala halina shida kabisa! Ila wale waliomwamndalia wosia Mungu anawaona,sio kwa kumtapeli Mjane,leo anacheza sebene peke yake mitandaoni wao wako kimyaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wyatt Mathewson,

Mzee mbona una munkari!!! Calm down tafadhal !!! Mambo ya laana kwenye mila za kiafrika bado yana tawala maisha ya kila siku. Si kama nayaamini ila niliyasoma kwenye athropology. Sasa kama huamini si unapuuza tu !!! Na wao wenye kesi kama wanajali mila sawa kama hawajali sawa as simple as that!

Nilichosema waangalie uamuzi wa mahakama wajumuishe na busara ili waendelee na biashara zao kwa usalama.

Kuna muda usia wake ulisambaa mitandaoni. Ule utakuwa umeandikwa na mwanasheria si peke yake. Sasa kama mawazo ya marehemu hayakuwa sawa, ndio maana nimeuliza muda uliopita tangu usia ulipoandikwa hadi kudanja. Maana in between angeweza kubadili mawazo yake aka revoke. Hujaona hapo nikiuliza kuhusu muda?

Halafy unaniwekea maneno sijasema.
Mambo ya ramli nimesema wapi? Hivi unaota nini? Na kuna mahali nimesema watu
waache haki zao? Niambie wapi nimesem nataka watu wache haki zao?

Mwenzako observer tu we kama unahusika moja kwa moja na hii ishu nakupa pole ila usimwagike mapovu bila mpango na mineno sjui stupidity sjui nini.....Au ndo hivyo tena upate sifa za kadamnasi?
 
Tunamfahamu R Mengi kuliko Jacline anavyo fikiri. Ule wosia hakuandika Mengi japo alisainishwa akiwa "senile'. Na ndiyo maana bi-bidada kasimamia hapo kuwa mumewe alidhalilishwa kwa madai ya akina Benjamin kuwa Mengi hakuwa sawasawa kiakili.

Jackline alikosea sana katika kufoji wosia kwa kuwatenga kina Regina na Abdiel. Angekuwa na akili angeweka clauses zinazowapa staja especially kwenye uangalizi wa wale mapacha just in case Mengi na Jack watakuwa wamekufa. Kwa ufinyu wa akili yake eti anamuweka dada yake. Makosa ya kijinga kabisa hayo. Mengi asingeweza kuandika hivyo
Du mkuu we kweli una inside info. Ule usia umeandikwa kwa chuki sana. Kama kweli Jackline kafoji ule usia basi mahakamani uta back fire abaki akiimba crazy over you !!!
 
Hakuna cha kupenda ndugu hapa, mume akifa ndio ndugu mnaanza kujifanya mna uchungu sana. Hapo hadi sahivi imeshakula kwao, hadi wanaanza kuweweseka eti wanamuomba wayasuluhishe , hahaahaha...ndugu ni mapepo

Sent using Jamii Forums mobile app
Unaongea kama vile huna ndugu, hovyoooo!! Kwa hiyo unataka kusema mke ndiye alikuwa akimpenda sana kuliko hao ambao wamesota nae tangu utotoni? Wewe naye ni walewale tu.
 
Laana atapata Jacky sio watoto mkuu...! Hapo kuna laana za Mke mkubwa na masikitiko ya watoto...! Tupeane 10yrs Jack km atakuwa na huo ukwasi anaoulilia...!
Kitu Karma hiyo mkuu.
Hap sina comment maana sina inside info!
 
Huyu si akae kimya aache mahakama ifanye kazi yake, yaani anajifanya ana uchungu na Mengi kuliko ndugu zake waliozaliwa tumbo moja, ukoo mmoja wanamjua nje ndani.

Huku naona kama anatafuta huruma na kuwapa faida wambeya.
Labda unapaswa ufahamu hili, kilichopo mahakamani na kitachoamriwa ni mgogoro kuhusu uhalali wa wosia. Haya mambo mengine ya kuzuiwa kwenda makaburini, ati alikuwa na mahusiano mengine na jamaa fulani, alimpendea marehemu pesa tu n.k mahakama haiendi amua bali Jacqueline anapaswa ajibu kama ataona yafaa.

Wacha mahakama itende haki lakini Jacqueline atumie haki na uhuru wa kujieleza kwa mambo mengine ambayo si sehemu ya mgogoro wa kimahakama, si kosa yeye kufanya hivyo alimradi havunji sheria.

Yumkini mengine yasemwayo ni uongo, wacha tusikie pande mbili maana uongo ukisemwa sana unageuka ukweli.
 
BISECKO,
Atumie uhuru wa Kujieleza au kueleza mambo ya familia kwenye social networks kwa faida ya nani au ili iweje?

Mambo yapo mahakamani acha mahakama iamue ,baada ya maamuzi ya mahakama akiona ana onewa atakata rufaa.Kama akihitaji msaada wa kisheria kuna taasisi kibao za kusaidia wanawake mf TAWLA ajieleze watamsaidia.

So kama alikuwa ana muheshimu kumpenda Mengi basi aheshimu na maswala ya familia yake Mengi.Kila mtu ana uhuru wa kujieleza lkn si kwa mambo ya kifamilia,wewe huoni sasa hivi anawapa faida watu,thread hii sasa hivi inaenda page ya 30,bado hujaingia Insta,Twitter,Fb ,hujaingia vijiweni huko wana izungumzia hii kesi.

Maswala ya kifamilia sio siasa kila sehemu una bwabwaja,kisa uhuru wa kujieleza huo UPUUZI.Kapewa platform ya kujieleza ambayo mahakama akajielezee huko na si huku mitandaoni.

Kama unadai haki utaipata tu ,kwani yeye Jack Mengi ni mme wake,ila Mengi ana watoto ambao ndio wanao ziendesha kampuni kila siku tokea kuanzishwa kwake kabla na baada ya Mengi kuaga dunia.

So watoto wa Mengi wana haki na Jack ana haki pamoja na mapacha wake.Sasa swala la maamuzi kujua yupi atapata kipi ni la mahakama.

Ila huu anao ufanya social networks ni ujinga na upuuzi wa hali ya juu,sasa huko Instagram aka changanyikeni anabishana na kila mtu si UCHIZI huu.

87478548_191521428745130_3017182410690570137_n.jpg
 
Bufa,
Jack anatafuta msaada na hajui wapi pa kupata!!!...rejea Mali ilikua 50/50 baba na mama watoto wakubwa wamechukua 50 ya mama, Sasa ya baba iko wapi?!!...kuna mengi family trust ambayo Reginald Ana 1% share!!!..Sasa ukifukua haya mambo jack atakufa kwa bp kwasababu hakujua chochote
 
Zanzibar-ASP,
Wewe hujui wachaga kabisa!!!.. Mengi alikua na Mtu anaitwa Nguma Sasa mama mercy 50%!!!...Mengi na huyo Nguma nao ni 50/50!!..Sasa Rudi kwenye mstari!!!..Nguma kashafariki!!!...Mengi kabaki na 50%...Mama Mercy Ana 50% ukichukua na 25% ya Nguma Anakua na 75%!!!..

Mengi nae 75% ajabu ni kwamba Reginald kwa kujua kwamba anaenda kusababisha Mgogoro kakubali watoto wa kubwa wachukue Mali zote za Mama Yao alafu Yeye,kawapa za kwake 50%...kabaki na 25%...

Jack kwa kutokujua Mila na desturi kwamba Abdiel ndio mrithi wa Mali zote za Mengi!!!..Sasa kuna Reginald Mengi family trust ambayo Reginald mwenyewe Ana 1% share nyingine zote ni za watoto wakubwa!!!
 
Burnaboy,

Anthropology inafundisha eti kuna laana?

Acha hilo darasa kalime

Huwezi kaa darasani mnasoma concept za uchawi as if kuna scientific proof kua zina exist!Hakuna kitu kama hicho!

Africa kuna laana,nani kakwambia na una proof?

Sio unachukua magonjwa ya depression unayageuza eti ni “laana”!

Sijakuwekea maneno,nimekuita mpiga ramli pale ulipojigeuza unajua kila kitu eti Mengi ndio kaandika Will na eti alikua na Hasira nakadhalika wakati vitu hivi huna proof navyo beyond reasonable doubt!
 
frama,
Mkuu hebu fafanua kidogo hapa,maana sijakuelewa kwamba total ni 150%? (Mercy 50%,Mengi 50% na Nguma 50%) Au ulimaanisha Mercy 50% (Mengi na Nguma kwa pamoja walikuwa na 50%) ambayo inaleta 100%?

Otherwise mengine tuko pamoja kabisa,hakuna janja ya kuvuna asiponda huyu Mjane wa mwendokasi,asubiri haki yake inayomstahili na siyo hiyo ya wosia wa kitapeli aliouandaa!
 
Wyatt Mathewson,
Mkuu kama hujui anthropology inafundisha nini jielimishe kwanza. Haya we unadhani anthropology inafundisha nini?

Sijasema najua kila kitu. Usia ukishaandikwa una stand kama ulivyo unless otherwise unapingwa kuhusu uhalali wake. Ndio hivyo ilivyo si kwamba mi mjuzi zaidi. Maana kama si hivyo kusingekuwa na haja ya kuandika usia au usingekuwepo kabisa!

Sasa mtu akiandika usia wake akaacha watoto wake wawili wapendwa wakubwa na cha zaidi akasema hata wakienda mahakamani na kushinda wapate sijui buku buku, we huoni hiyo ni chuki kubwa sana??? Unahitaji ujuzi wowote kuona hii ni chuki kubwa? Watu hapa wamesema ule usia ume fojiwa na jackie, sawa hiyo inawezemana. Na kama ni hivyo si mahakama itaamua? Punguza munkare!
 
Mkuu hebu fafanua kidogo hapa,maana sijakuelewa kwamba total ni 150%? (Mercy 50%,Mengi 50% na Nguma 50%) Au ulimaanisha Mercy 50% (Mengi na Nguma kwa pamoja walikuwa na 50%) ambayo inaleta 100%?

Otherwise mengine tuko pamoja kabisa,hakuna janja ya kuvuna asiponda huyu Mjane wa mwendokasi,asubiri haki yake inayomstahili na siyo hiyo ya wosia wa kitapeli aliouandaa!

hahah!
Hivi alisema hata wakishinda wapewe shilingi 1/= ??
Dah!
Ule wosia ni purely MENGI kaandika, maana hii stahili ya 1/= ni yake kama alivyompeleka Rostam Mahakamani akaenda kudai 1/=.
 
Halafu usome hapo juu (#483) Frama akielezea kuhusu role ya mila kuhusu hii mambo. Naona umesahau kumuuliza scientific proof ya mila !!!

Tofautisha “MILA” na “UCHAWI”!

Two different things,get that in your head mzee!

Unachanganya changanya concepts tu hapa!
 
Burnaboy,

Kumbe mgao wa buku ni chuki kubwa?

Nashindwa kuelewa,ulikuepo hapo uka-verify hiyo chuki?

Ishu ni kwamba “unahisi”,proof hakuna!

Hisia hazibebi weight kwenye court mzee,ni kujazia jazia maelezo tu!

Ndio maana wakati unaandika ni vizuri ungesema “nahisi” alikua na chuki kwa wanawe,ili watu tujue cha kukuchukulia!
 
Kibanga Ampiga Mkoloni,
Duh Kumbe ni 1000/=

"Wosia huo unaeleza kuwa kwa makusudi Dr. Mengi ameacha kutoa urithi kwa baadhi ya warithi wake na kutoorodhesha majina yao kwa makusudi na yeyote atakayepinga wosia huo na kufanikiwa basi apewe shilingi elfu moja (1,000). "
 
Back
Top Bottom