Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
MHE. JAFARI WAMBURA - SIMAMIENI FEDHA VIZURI MSISUBIRI RIPOTI YA CAG
Mbunge wa Rorya Mkoa wa Mara, Mhe. Jafari Wambura Chege tarehe 18 Aprili, 2023 amechangia bajeti ya TAMISEMI ya Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 Bungeni Jijini Dodoma
Mhe. Jafari amesema Rais anatimiza wajibu wake kazi ya Wabunge, viongozi wa kisiasa pamoja watumishi kuhakikisha fedha zinazopelekwa kwenye miradi inasimamiwa ipasavyo na kuzaa matunda.
Hivyo, Bunge halitakuwa na matunda mazuri kama kila wanaposimama wanamsifia Rais anavyopeleka fedha lakini inapokwenda hakuna usimamizi mzuri pasipo kusubiri taarifa ya CAG.