Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Mbunge wa Jimbo la Kisarawe na Waziri wa zamani, Suleiman Jafo, amewasilisha pendekezo la kiubunifu bungeni lenye lengo la kutatua changamoto ya ajira kwa vijana nchini Tanzania.
Katika mchango wake, Jafo amesisitiza kuwa bado kuna haja ya kuwa na mpango mahususi wa muda mrefu wa kuingiza vijana wengi zaidi katika mfumo wa kazi.
Katika mchango wake, Jafo amesisitiza kuwa bado kuna haja ya kuwa na mpango mahususi wa muda mrefu wa kuingiza vijana wengi zaidi katika mfumo wa kazi.
Hoja Kuu ya Mpango huo:
Jafo amependekeza kuanzishwa kwa mfumo wa ajira za muda (Part-time Employment) kwa vijana wahitimu wa vyuo vikuu na vyuo vya kati kwa mikataba ya miaka mitatu. Mpango huu unalenga:- Idadi ya Vijana: Kuchukua vijana 50,000 kila mwaka.
- Mgawanyo: 20% wawe wahitimu wa stashahada (Diploma) na 80% wawe wahitimu wa shahada (Degree).
- Malipo (Alawansi): Wahitimu wa Diploma kulipwa Tsh 500,000kwa mwezi.
- Wahitimu wa Degree kulipwa Tsh 700,000 kwa mwezi.
Gharama na Chanzo cha Mapato:
Kwa mujibu wa mahesabu ya Jafo, mpango huu utagharimu takriban Tsh. Bilioni 396 kwa mwaka. Amependekeza vyanzo vya mapato viwe ni pamoja na:- Asilimia 10 ya mapato ya ndani ya halmashauri (Own Source).
- Asilimia 10 ya gawio kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na mashirika mengine ya serikali ambayo yamekuwa yakikusanya zaidi ya trilioni moja kila mwaka.
Sababu za Mpango Huu:
Jafo amebainisha kuwa vijana wengi, wakiwemo wahitimu wa Shahada za Uzamili (Masters), kwa sasa wanafanya kazi za udereva wa bodaboda kutokana na ukosefu wa fursa rasmi. Ameeleza kuwa mpango huu utawasaidia vijana:- Kupata uzoefu wa kazi (Work experience).
- Kuwa na kipato cha uhakika kwa miaka mitatu.
- Kuondoa msongo wa mawazo (Frustration) kwa wahitimu.
